Pre GE2025 Kutokana na tofauti za uongozi ndani ya CHADEMA, inawezekana kuna mtu kati yao anahusika na matukio ya utekaji?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Si bure, kuna kitu kinachoendelea ndani ya chama hiki kikongwe cha siasa kilichojizolea umaarufu mkubwa wa kisiasa miaka ya nyuma.

Vyombo vya kiuchunguzi wana kila sababu ya kukifanyia uchunguzi wa kina wa kiusalama chama hiki cha siasa, viongozi wake waandamizi na wananchama wake mashuhuri dhidi ya kuhusika kwao kwenye mambo haya, na vyanzo vya taarifa za kihalifu walizonazo hususani kwenye hili la watu kupotea na baadae kukutwa wakiwa wafu. kwa hakika uchunguzi huo unaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutuliza hali ya taharuki wanazoibua chadema kwa jamii na tashwishwi za kiusalama kwa wananchi.

Je, ni kweli wao kama chadema hawahusiki na utekaji huo? ni vizuri kijiridhisha isije ikatokea Shakahola ya kisiasa ndani ya chadema Tanazania? are these not stage managed political schemes of silencing challengers in party elections?

Pia soma: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Ndani ya chama hicho cha siasa hakuko salama na hakuana utulivu wa kisiasa, joto la uchaguzi ni kali lipo juu mno, taharuki na hali ya kutoaminiani imetanda pakubwa.

Je, hii haiwezi kuwa sababu ya kunyamazishana katika jitihada za kugombania nafasi za uongozi kwa ambao wamekosa uhalali, hoja na hawataki changamoto kwenye sanduku la kura?

Kwa maoni yangu na bilashaka yoyote uchunguzi wa kiusalama ukifanyika ndani ya chama hiki, taharuki hizi zote wanazoibua wenyewe zitakoma, kwasababu kuna wasiwasi na viashiria vya moja kwa moja kwa chama hiki kuhusika, lakini ili kujiridhisha ni muhimu sana kuchunguza.

Mungu Ibariki Tanzania.

Matukio mengine ya utekaji yakihusisha watu wasiyojulikama soma Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Vipi DC wa longido?
 
Ungerudia kuusoma uzi wako huu uliondika labda kuna sehemu umechapia
 
Ficha ujinga basi
 
Hata namna ya uzungumzaji wako ni dhahiri unaujua ukweli kwamba chadema hawawezi kuhusika na ujinga wa kiasi hiki.
Kama chadema ama taasisi ama mtu au kikundi kinaweza kuratibu utekaji na kisha kuua watu kwenye nchi yenye vyombo vingi vya usalama basi hio nchi uwepo wake ni wa mashaka sana, ni kusema nchi hio imeshafitinika.
 
Hebu tuache ujinga nyie!!

Chadema Wana dola walioshinda!!?

Ina maana utekaji was hao unaowataja una baraka za Dola ambayo ccm ndio imeshika!!?

Nini kazi ya jeshi la police kulinda raia!!?

Acheni hizi mambo nyie !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…