Kutokana na utabiri wa TMA kuhusu uhaba wa mvua; je, bwawa la Mwalimu Nyerere litajaa na kuanza kuzalisha umeme mwakani?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nauliza tu kwa wataalamu wa Hydro power je tuendelee kutumaini umeme mpya kutoka Bwawa la Nyerere katikati ya mwaka ujao kama tulivyoahidiwa?

TMA wametabiri mvua chache sana mwishoni mwa mwaka.
 
Utaratibu Mzuri Umewekwa Litajaa Tu Tena Mpaka Pomoni (Kufurika)
 
Makamba na team yake wamepata sbb za kuwapa songas mkataba wa kuzalisha umeme
 
Nauliza tu kwa wataalamu wa Hydro power je tuendelee kutumaini umeme mpya kutoka Bwawa la Nyerere katikati ya mwaka ujao kama tulivyoahidiwa?

TMA wametabiri mvua chache sana mwishoni mwa mwaka.
Haliwezi kujaa kwa hiyo tusitishe ujenzi wake kuokoa fedha!

Hayo naoni ya watu myopic ambao ni wengi miongoni mwetu leo! Rais Kikwete alitupumbaza sana kutunyima uwezo wa kuona mbali, ambao ulikuwa umeaza kujengwa na Mkapa. Tuliporudishwa kwenye msitali tukalalamika sana na sasa tumemrudia Kikwete tena tumeanza kuwa tunaona mambo myopically.

Kuna watu waliuliza kwa nini serikali inanunua ndege, badala ya kugawa fedha hizo mitaani!
 
Nauliza tu kwa wataalamu wa Hydro power je tuendelee kutumaini umeme mpya kutoka Bwawa la Nyerere katikati ya mwaka ujao kama tulivyoahidiwa?

TMA wametabiri mvua chache sana mwishoni mwa mwaka.
Kwa mujibu wa wataalam kama mvua zipo za kutosha bwawa linajaa kwa muda wa miezi mitatu. Kama mvua hakuna kama walivyotabiri TMA sijui litajaa kwa miezi mingapi. Ukubwa wa eneo la mradi ni 1,350 km 2 (135,000 hectares).
 
Siasa ni tatizo...

Kila niliposikia litakamilika ndani ya miaka 3 nilikuwa nacheka tu. Hawa jamaa wapo serious kweli? Anyways, hata SGR Dar Moro tuliambiwa inakamilika 2019, tunaelekea 2022 bado nikipita pale Gerezani daraja bado
 
Wanasiasa wetu ni waongo hakuna mfano:

Mmoja alituambia jiwe ni mzima, yuko ofisini anachapa kazi -kumbe aliisha RIP kitambo

Huyo huyo akakutuambia SGR Moro-Dar itaanza kazi 8/19. Leo ni 10/21 hakuna cha kuanza kazi wala kumalizika

Mwaka juzi hilo bwawa la JNHEP lilisombwa na maji hakuna mwanasiasa wa ccm aliyesema lolote, zaidi ya ZZK wa ACT wazalendo.

Kwa hiyo swala la jnhepp kujazwa maji ni maneno tu...na kwa mwaka huu labda watalijaza hewa..maana mvua hamna
Hata ikichelewa itakamilika itajaa. Isipokuwa bwawa hili litaathiriwa na uhaba wa mvua na ukame sawa na mabwawa yote. Ujenzi ulikuwa azimio la kisiasa la kupuuza wataalamu wengi, bila ushirikiano wa umma. Tutaona.

Mzee aliamua kupuuza mradi wa gesi, hivyo "the pipeline – which has consumed Sh2.7 trillion of taxpayers’ money - is only utilised by about seven percent of its capacity, according to a past audit by the Controller and Auditor General."

“What is going on in the country at present is that we are paying the price of putting all our concentration and resources only on the Julius Nyerere Hydropower project,”
(Citizen 19.11.21)
 
Mkuu,
Hata uwekezaji wa gesi wazungu walipiga kelele kwenye zabuni ya ujenzi wa bomba kwamba kwanini wapewe Wachina? Mataifa makubwa duniani yamekuwa kwa miaka mingi yakipigana kuhusu fursa hasa barani Afrika ndiyo maana Mwl Nyerere aliasisi dhana ya siasa za kutofungamana na upande wowote. Rufiji pia wamelaumu kwanini zabuni wamepewa Misri? Bagamoyo EPZ nayo watakuja kulaumu kwanini wamepewa Wachina mkataba ukisainiwa.

Gesi ni madini yaliyoko pande kadhaa za sayari, Urusi ikiongoza dunia kwa futi za ujazo 1,688 trilioni (sawa na futi za ujazo quadrilioni 1.6), katika Afrika Msumbiji ina deposit kubwa ya gesi ya futi za ujazo 125 trilioni, Tanzania ina futi za ujazo 2.17 trilioni. Kwa mantiki ya takwimu hizo, Tz tunahitaji kubuni vyanzo vingine mbadala. Hata hivyo, tangu tumeanza kuchimba gesi kwanini hatukuwa na mpango wa kusindika humu humu ili tuwe na uchumi wa gesi badala ya uchumi wa umeme wa maji kama wengine wanavyotaka ili eti tuachane na JNHEPP? Leo hii gesi ya Tz inasafirishwa nje ya Afrika kuchakatwa kuwa hatua ya mwisho ya ulaji na kurudishwa Tz kuuzwa badala yake bei ya gesi ni kubwa kwa watumiaji wengine achilia viwanda. Duniani kote, umeme wa maji (Hydro Power) ndiyo uwekezaji/uzalishaji rahisi kuliko wa vyanzo vingine vyote vilivyopo.

Lawama za mradi kama wa JNHEPP ziko maeneo mengi Afrika kiasi kwamba hazifai kutuyumbisha. DR Congo Waziri Mkuu Patrice Lumumba alibuni mradi wa umeme wa maji Enger Dam Hydro-Power Project na moja ya sababu zilizofanya akauawa ni hiyo (JPM yeye alikufa kwa tatizo la umeme wa moyo), leo hii Rais Mstaafu Kabila Jr ameufufua upya akamkabidhi Rais Tshisekedi auendeleze. Uwezo wa Enger Dam ni 40% ya mahitaji ya umeme Afrika. Unatekelezwa kwa awamu tatu za: Mradi wa kwanza 4,800MW. Mradi wa pili ni 40,000MW. Watu 60,000 wanatarajiwa kuhamishwa. Kama kawaida, mataifa makubwa yanaaendelea tangu enzi za Patrice Lumumba kupinga mradi huu kwa kigezo kile kile cha mazingira kama wanavyofanya kwa JNHEPP.

maxresdefault.jpg

thumbs_b_c_2964924ee68f77b5008b2ad2f3c3bc35.jpg

The Case for Uganda.
Uganda imewekeza kwenye uzalishaji wa umeme wa maji kwa kiwango kikubwa hadi kuleta mgogoro baina yake na nchi za Nile (Nile Countries), vifuatazo ni vituo vya kuzalisha umeme wa maji nchini Uganda:-

Hydroelectric power stationCoordinatesCapacity
Agbinika Power Station3.5000°N 31.1200°E20 MW
Ayago Power Station2.3630°N 31.9200°E600 MW
Bugoye Power Station0.3000°N 30.1005°E13 MW
Bujagali Power Station0.4975°N 33.1400°E250 MW
Buseruka Power Station1.5550°N 31.1500°E9.0 MW
Isimba Power Station0.9400°N 32.9650°E140 MW
Kanungu Power Station0.9306°S 29.7311°E6.6 MW
Karuma Power Station2.2430°N 32.2450°E600 MW
Kiira Power Station0.4506°N 33.1858°E200 MW
Mpanga Power Station0.0810°N 30.3810°E18 MW
Mubuku I Power Station0.318610°N 30.100000°E5 MW
Mubuku III Power Station0.263340°N 30.120000°E10 MW
Muzizi Power Station0.9650°N 30.5450°E26 MW
Nalubaale Power Station0.443611°N 33.185°E180 MW
Nyagak Power Station2.4310°N 30.9745°E3.5 MW
Nyagak II Power Station2.5000°N 30.9900°E5 MW
Nyagak III Power Station2.4500°N 30.9800°E4.36 MW
Kisiizi Power Station0.9956°S 29.9625°E0.3MW
Waki Power Station1.7660°N 31.3660°E5 MW
Gwere-Luzira Power Station3.6700°S 31.7810°E0.5KW
Kikagati Power Station1.0300°S 30.6800°E16MW

NB.
Sioni sababu ya Tz kuogopa kujenga mradi wa JNHEPP kwasababu wawekezaji wa kigeni wanapotamani kuja kukamata fursa Afrika wanataka waje wawekeze bila nishati ya uhakika? Au wanataka waje watuuzie mafuta kama nishati kwa ajili ya uwekezaji? Uganda waliziba masikio wakajenga, DR Congo walisita baada ya Lumumba kuuawa sasa wameamka, Tz tusibweteke.

JNHEPP Kazi iendelee....

137D63D7-D3AE-4522-A5CD-EE32F34B49C6.jpg

Taswira zote kwa hisani ya google.
 
Mkuu kama ulisoma mchango wangu, sikugusa swali la mazingira. Nina mashaka kwamba katika Tanzania umemaji una uhakika wa kutosha.
Je, wakati wa kujengwa kwa Kidatu na malambo mengine, ulisikia wasiwasi kwamba ukame unaweza kuzuia uzalishaji? Hapana? Sawa, labda wapangaji hawapendi kuonyesha mashaka?
Je inawezekana wapangaji wa mradi wa JNHEPP wanafuata nyayo zao?

Je hujaona taarifa ya Citizen ya tar. 29.10.21 ("Tanzania ‘to have most climate migrants in Lake Victoria Basin’ - Dar es Salaam. Tanzania is projected to have the highest number of internal climate migrants in the Lake Victoria Basin by 2050 as the continent is hit hardest by climate change, with up to 86 million Africans forced to migrate within their own countries by 2050, the World Bank has revealed.")

Maanake ukame utaongezeka. Maeneo makubwa ya bara yatakuwa pakavu zaidi na kulazimisha watu kuhama. Tayari siku hizi imetokea kwamba Ruaha Mkuu imekosa maji kutokana na miradi mingi ya umwagiliaji kwenye nyanda za kusini, pamoja na Usangu Flats.
Tena kila bwawa katika mazingira ya joto linapoteza maji kutokana na uvukizaji.

kama bwawa kule Kongo linawezekana? Labda, huko tabianchi ni tofauti sana na Tanganyika, nchi yenye historia ya ukame mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom