johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Makamba na team yake wamepata sbb za kuwapa songas mkataba wa kuzalisha umeme
Basi hata kama hakuna mvua tupate japo nusu yake2115 MW sio masihara...
Haliwezi kujaa kwa hiyo tusitishe ujenzi wake kuokoa fedha!Nauliza tu kwa wataalamu wa Hydro power je tuendelee kutumaini umeme mpya kutoka Bwawa la Nyerere katikati ya mwaka ujao kama tulivyoahidiwa?
TMA wametabiri mvua chache sana mwishoni mwa mwaka.
Kwa mujibu wa wataalam kama mvua zipo za kutosha bwawa linajaa kwa muda wa miezi mitatu. Kama mvua hakuna kama walivyotabiri TMA sijui litajaa kwa miezi mingapi. Ukubwa wa eneo la mradi ni 1,350 km 2 (135,000 hectares).Nauliza tu kwa wataalamu wa Hydro power je tuendelee kutumaini umeme mpya kutoka Bwawa la Nyerere katikati ya mwaka ujao kama tulivyoahidiwa?
TMA wametabiri mvua chache sana mwishoni mwa mwaka.
Kutoka wapi?Basi hata kama hakuna mvua tupate japo nusu yake
Ujinga gani mama D?Ule ujinga wa 2005 hautakubalika. Watanzania walishafunguka akili
Tanzania ni tajiri💣🔥
Au nasema uongo ndugu yangu
Ujinga gani mama D?
Mtakuwa likizo bwashee!Kwa hiyo ss tunaopiga mishe za kilimo itakuwaje mwaka huu
NdioooooUle ujinga wa 2005 hautakubalika. Watanzania walishafunguka akili
Tanzania ni tajiri[emoji378][emoji91]
Au nasema uongo ndugu yangu
Hata ikichelewa itakamilika itajaa. Isipokuwa bwawa hili litaathiriwa na uhaba wa mvua na ukame sawa na mabwawa yote. Ujenzi ulikuwa azimio la kisiasa la kupuuza wataalamu wengi, bila ushirikiano wa umma. Tutaona.Wanasiasa wetu ni waongo hakuna mfano:
Mmoja alituambia jiwe ni mzima, yuko ofisini anachapa kazi -kumbe aliisha RIP kitambo
Huyo huyo akakutuambia SGR Moro-Dar itaanza kazi 8/19. Leo ni 10/21 hakuna cha kuanza kazi wala kumalizika
Mwaka juzi hilo bwawa la JNHEP lilisombwa na maji hakuna mwanasiasa wa ccm aliyesema lolote, zaidi ya ZZK wa ACT wazalendo.
Kwa hiyo swala la jnhepp kujazwa maji ni maneno tu...na kwa mwaka huu labda watalijaza hewa..maana mvua hamna
Mkuu,Hata ikichelewa itakamilika itajaa. Isipokuwa bwawa hili litaathiriwa na uhaba wa mvua na ukame sawa na mabwawa yote. Ujenzi ulikuwa azimio la kisiasa la kupuuza wataalamu wengi, bila ushirikiano wa umma. Tutaona.
Mzee aliamua kupuuza mradi wa gesi, hivyo "the pipeline – which has consumed Sh2.7 trillion of taxpayers’ money - is only utilised by about seven percent of its capacity, according to a past audit by the Controller and Auditor General."
“What is going on in the country at present is that we are paying the price of putting all our concentration and resources only on the Julius Nyerere Hydropower project,”
(Citizen 19.11.21)
| Hydroelectric power station | Coordinates | Capacity |
| Agbinika Power Station | 3.5000°N 31.1200°E | 20 MW |
| Ayago Power Station | 2.3630°N 31.9200°E | 600 MW |
| Bugoye Power Station | 0.3000°N 30.1005°E | 13 MW |
| Bujagali Power Station | 0.4975°N 33.1400°E | 250 MW |
| Buseruka Power Station | 1.5550°N 31.1500°E | 9.0 MW |
| Isimba Power Station | 0.9400°N 32.9650°E | 140 MW |
| Kanungu Power Station | 0.9306°S 29.7311°E | 6.6 MW |
| Karuma Power Station | 2.2430°N 32.2450°E | 600 MW |
| Kiira Power Station | 0.4506°N 33.1858°E | 200 MW |
| Mpanga Power Station | 0.0810°N 30.3810°E | 18 MW |
| Mubuku I Power Station | 0.318610°N 30.100000°E | 5 MW |
| Mubuku III Power Station | 0.263340°N 30.120000°E | 10 MW |
| Muzizi Power Station | 0.9650°N 30.5450°E | 26 MW |
| Nalubaale Power Station | 0.443611°N 33.185°E | 180 MW |
| Nyagak Power Station | 2.4310°N 30.9745°E | 3.5 MW |
| Nyagak II Power Station | 2.5000°N 30.9900°E | 5 MW |
| Nyagak III Power Station | 2.4500°N 30.9800°E | 4.36 MW |
| Kisiizi Power Station | 0.9956°S 29.9625°E | 0.3MW |
| Waki Power Station | 1.7660°N 31.3660°E | 5 MW |
| Gwere-Luzira Power Station | 3.6700°S 31.7810°E | 0.5KW |
| Kikagati Power Station | 1.0300°S 30.6800°E | 16MW |
Mkuu kama ulisoma mchango wangu, sikugusa swali la mazingira. Nina mashaka kwamba katika Tanzania umemaji una uhakika wa kutosha.Mkuu,
Hata uwekezaji wa gesi wazungu walipiga kelele kwenye zabuni ya ujenzi wa bomba kwamba kwanini wapewe Wachina? Mataifa makubwa duniani yamekuwa kwa miaka mingi yakipigana kuhusu fursa hasa barani Afrika ndiyo maana Mwl Nyerere aliasisi dhana ya siasa za kutofungamana na upande wowote. Rufiji pia wamelaumu kwanini zabuni wamepewa Misri? Bagamoyo EPZ nayo watakuja kulaumu kwanini wamepewa Wachina mkataba ukisainiwa.
Gesi ni madini yaliyoko pande kadhaa za sayari, Urusi ikiongoza dunia kwa futi za ujazo 1,688 trilioni (sawa na futi za ujazo quadrilioni 1.6), katika Afrika Msumbiji ina deposit kubwa ya gesi ya futi za ujazo 125 trilioni, Tanzania ina futi za ujazo 2.17 trilioni. Kwa mantiki ya takwimu hizo, Tz tunahitaji kubuni vyanzo vingine mbadala. Hata hivyo, tangu tumeanza kuchimba gesi kwanini hatukuwa na mpango wa kusindika humu humu ili tuwe na uchumi wa gesi badala ya uchumi wa umeme wa maji kama wengine wanavyotaka ili eti tuachane na JNHEPP? Leo hii gesi ya Tz inasafirishwa nje ya Afrika kuchakatwa kuwa hatua ya mwisho ya ulaji na kurudishwa Tz kuuzwa badala yake bei ya gesi ni kubwa kwa watumiaji wengine achilia viwanda. Duniani kote, umeme wa maji (Hydro Power) ndiyo uwekezaji/uzalishaji rahisi kuliko wa vyanzo vingine vyote vilivyopo.
Lawama za mradi kama wa JNHEPP ziko maeneo mengi Afrika kiasi kwamba hazifai kutuyumbisha. DR Congo Waziri Mkuu Patrice Lumumba alibuni mradi wa umeme wa maji Enger Dam Hydro-Power Project na moja ya sababu zilizofanya akauawa ni hiyo (JPM yeye alikufa kwa tatizo la umeme wa moyo), leo hii Rais Mstaafu Kabila Jr ameufufua upya akamkabidhi Rais Tshisekedi auendeleze. Uwezo wa Enger Dam ni 40% ya mahitaji ya umeme Afrika. Unatekelezwa kwa awamu tatu za: Mradi wa kwanza 4,800MW. Mradi wa pili ni 40,000MW. Watu 60,000 wanatarajiwa kuhamishwa. Kama kawaida, mataifa makubwa yanaaendelea tangu enzi za Patrice Lumumba kupinga mradi huu kwa kigezo kile kile cha mazingira kama wanavyofanya kwa JNHEPP.
The Case for Uganda.
Uganda imewekeza kwenye uzalishaji wa umeme wa maji kwa kiwango kikubwa hadi kuleta mgogoro baina yake na nchi za Nile (Nile Countries), vifuatazo ni vituo vya kuzalisha umeme wa maji nchini Uganda:-
Hydroelectric power station Coordinates Capacity Agbinika Power Station 3.5000°N 31.1200°E 20 MW Ayago Power Station 2.3630°N 31.9200°E 600 MW Bugoye Power Station 0.3000°N 30.1005°E 13 MW Bujagali Power Station 0.4975°N 33.1400°E 250 MW Buseruka Power Station 1.5550°N 31.1500°E 9.0 MW Isimba Power Station 0.9400°N 32.9650°E 140 MW Kanungu Power Station 0.9306°S 29.7311°E 6.6 MW Karuma Power Station 2.2430°N 32.2450°E 600 MW Kiira Power Station 0.4506°N 33.1858°E 200 MW Mpanga Power Station 0.0810°N 30.3810°E 18 MW Mubuku I Power Station 0.318610°N 30.100000°E 5 MW Mubuku III Power Station 0.263340°N 30.120000°E 10 MW Muzizi Power Station 0.9650°N 30.5450°E 26 MW Nalubaale Power Station 0.443611°N 33.185°E 180 MW Nyagak Power Station 2.4310°N 30.9745°E 3.5 MW Nyagak II Power Station 2.5000°N 30.9900°E 5 MW Nyagak III Power Station 2.4500°N 30.9800°E 4.36 MW Kisiizi Power Station 0.9956°S 29.9625°E 0.3MW Waki Power Station 1.7660°N 31.3660°E 5 MW Gwere-Luzira Power Station 3.6700°S 31.7810°E 0.5KW Kikagati Power Station 1.0300°S 30.6800°E 16MW
NB.
Sioni sababu ya Tz kuogopa kujenga mradi wa JNHEPP kwasababu wawekezaji wa kigeni wanapotamani kuja kukamata fursa Afrika wanataka waje wawekeze bila nishati ya uhakika? Au wanataka waje watuuzie mafuta kama nishati kwa ajili ya uwekezaji? Uganda waliziba masikio wakajenga, DR Congo walisita baada ya Lumumba kuuawa sasa wameamka, Tz tusibweteke.
JNHEPP Kazi iendelee....
Taswira zote kwa hisani ya google.