Kutokea Bwawani mpaka Chalinze, kipande cha Ubena Zomozi, Mwidu, Mdaula huwa kitamu sana

PureView zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Posts
10,786
Reaction score
35,916
Omba MUNGU upite eneo hili kama hakuna foleni ya malori, hapa utashuhudia madereva wa crown, Brevis, Mark X, Subaru, Alteza wakitunisha misuli dhidi ya V8.

Hapa nakumbuka mwaka Juzi kuna mwendawazimu alinipita Volkswagen Amarok kama risasi nahisi Yule mwehu anatumia bangi kali sana. Hiki ni kipande ambacho kama gari yako haina uwezo isibishane kabisaa ni Bora uwe mpole na speed yako 60 ili kila anayekupita asijisifie ya kuwa unashindana nae.

Nawakumbusha madereva wenzangu kuwa huu mwezi December ni mwezi wa kila MTU anasifiri hivyo jitahid Sana kufanya safari yako bila kuangalia madereva wenzio watakuonaje.

 
Hayo Ni Maeneo Hatari Sana Tena Unatakiwa Kuwa Makini Mno. Maeneo Ya Ajali Sana Kuna Kipindi Cha Jiwe Utawala Wake Ulitaka Kumfuta Kazi RPC PWANI Akawa Halali Maana Oops
 
Mwendo kasi unaua
Mwendokasi ni. Neno pana sana, simply distance / time, kwa maana hata 10km/ h ni mwendokasi!!, unaposema mwendokasi unaua i intakiwa haswa uweke specific speed ambayo ni hatari, ukiendesha barabara za sourh Africa N1 kwa mfano kuna vipande vingi tu ambavyo 120km/h, ni legal na imesisitizwa kwa vibao kabisa
 
Sasa madereva akili mbovu ndio wanajibanika wenyewe kama mishikaki ya samaki nchanga ama kwa magari mengine,makorongo ,miti ama kwa kumbirita mara sabini.Kisa barabara wanaona wanaimudu na vigari vyao.
 
Kwa kifupi Tanzania tuna miundombinu mibovu tu
 
Hii kapeti unaichapa 180km/h chini 120km/h ila sasa kina historia mbaya sana, umakini mkubwa

Moja ya mabosi wa taasis kubwa aliaga dunia kwamwendo mkali sana maeneo hayo akiwa na VX V8 na mwingine siku nne baada ya kuteuliwa na hardtop ilisagika sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…