Kutokuendelea na mkataba na mpangaji wa nyumba

Magehema

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Posts
428
Reaction score
28
Kuna mpangaji wangu wa nyumba nataka kutokuendelea nae na mkataba. Kwa mujibu wa mkataba wetu tunalipana kwa miezi sita sita na pia kuna room ya kuongeza kodi baada ya kujadiliana nae. Mwezi huu nategemea kupokea kodi ya nyumba ya miezi sita, ila kutokana na usumbufu wake nataka baada ya kulipana tu kwa miezi sita ijayo nisiongeze mkataba mwingine. Je anahitaji kuzipata hizi taarifa muda gani kabla ya kusitisha mkataba?
 
ndugu ngoja wataalamu wa sheria watakuja kukufahamisha.
Ila nyie wenye nyumba mnamatatizo(si wote) kuna jamaa yangu alitakiwa alipe kodi mpya wiki moja kabla ya tarehe 2 augost,ilipofika tarehe 18 Mwenye nyumba akampa barua kuwa amepandisha kodi toka Lak 1 ya awali hadi lak na nusu,ongezeko hilo ilitakiwa anzekulipa mkataba mpya,sababu eti ni gharama za maisha kupanda.mimi na rafiki yangu tukajiuliza kwanini kupanda siku chache kuelekea kulipa?hiyo badget imetoka wapi wakati ulikua umeandaa lak kwa mwezi then ghafla unambiwa kwa lakin na nusu?kwa kweli tusio na nyumba tunapata tabu sana
 
ukishakamata mshiko wako unampa notisi ya kusitisha mkataba, ila sasa inabidi akae miezi 3 bure ili apate muda mrefu wa kutafuta nyumba na kuondoka
 
mpe notisi akiwa ndani ya kodi yake! Yaani kama amekulipa miezi 6 kutoka hv sasa! Wewe mpe nots mwez wa 11 na ikifika mwezi wa pili kodi yake itakuwa imeisha! Na hapo hapo ile amri ya sheria itakuwa imefanya kazi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…