Kuna mpangaji wangu wa nyumba nataka kutokuendelea nae na mkataba. Kwa mujibu wa mkataba wetu tunalipana kwa miezi sita sita na pia kuna room ya kuongeza kodi baada ya kujadiliana nae. Mwezi huu nategemea kupokea kodi ya nyumba ya miezi sita, ila kutokana na usumbufu wake nataka baada ya kulipana tu kwa miezi sita ijayo nisiongeze mkataba mwingine. Je anahitaji kuzipata hizi taarifa muda gani kabla ya kusitisha mkataba?