SI KWELI Kutokufanya tendo la ndoa Kwa muda mrefu husababisha kutokwa na chunusi?

SI KWELI Kutokufanya tendo la ndoa Kwa muda mrefu husababisha kutokwa na chunusi?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Baada ya kufatilia mitandao tofauti tofauti ya kijamii nimekutana na madai kuwa kutokufanya mapenzi kwa muda mrefu husababisha kutokwa na chunusi.

je, kuna uhusiano gani kati ya chunusi na kutokufanya mapenzi kwa muda mrefu?
Screenshot_20260727-102804.png

1785137586528.png
 
Tunachokijua
Chunusi ni tatizo la ngozi linalotokea pale vinyweleo vya ngozi vinapoziba kwa mafuta na seli za ngozi zilizokufa. Hali hii husababisha kutokea kwa vichwa vyeupe (whiteheads), vichwa vyeusi (blackheads), au chunusi zenye uvimbe (pimples). Chunusi huwapata zaidi vijana balehe, lakini zinaweza kuwatokea watu wa rika zote. Jina la kitabibu ni acne vulgaris.

Sababu za chunusi


Chunusi hutokea pale ambapo vinyweleo vya ngozi huziba. Je, ni zipi sababu za kuziba kwa vinyweleo hivyo vya ngozi. Zifuatazo ndizo sababu,

  • Mafuta ya ngozi (sebum): Mafuta ya asili yanayolinda ngozi, lakini yakizidi yanaweza kuziba matundu.
  • Bakteria: Bakteria wanaoishi kwa kawaida kwenye ngozi wanaweza kuongezeka na kuziba vinyweleo.
  • Seli za ngozi zilizokufa: Ngozi hujibadilisha mara kwa mara, na seli zilizokufa zinaweza kujikusanya na kuziba vinyweleo.
Vinyweleo vinapoziba, hutengeneza chunusi na kusababisha uvimbe (inflammation). Uvimbe huu unaweza kuambatana na maumivu, kuvimba na wekundu kwenye eneo lililoathirika.

Mambo yanayoweza kuchochea zaidi chunusi.

Yapo baadhi ya mambo ambayo yameanishwa na makala mbalimbali ambayo yanaweza kuzidisha ama kuifanya hali hiyo kuwa mbaya zaidi;

  • Kuvaa nguo au vifaa vinavyobana, kama vile kofia, helmeti za michezo au vifaa vingine vinavyobana ngozi.
  • Uchafuzi wa hewa na hali ya hewa, hasa maeneo yenye unyevunyevu mwingi.
  • Kutumia bidhaa zenye mafuta mengi, kama losheni na krimu nzito, au kufanya kazi katika mazingira yenye mafuta mengi, kwa mfano jikoni au migahawani.
  • Msongo wa mawazo (stress), ambao huongeza kiwango cha homoni ya cortisol, inayoweza kuchochea chunusi.

Baadhi ya dawa, ambazo zinaweza kuwa na athari ya kusababisha au kuongeza chunusi.

Kubonyeza au kuchezea chunusi, jambo ambalo linaweza kuzifanya ziongezeke, kuvimba zaidi au kuacha makovu.

Je, kutokufanya mapenzi kunachangia kupata chunusi?

Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu uhusiano wa kutokufanya mapenzi na kupata chunusi. Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii kumeibuka msemo wa;

“Upo single zaidi ya mwaka mmoja na hauna chunusi.” Je, madai haya yana uhalisia kiasi gani?

Tovuti ya skincare inaeleza kuwa bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kisayansi unaonesha kuwa kutokufanya mapenzi kwa muda inaweza kuwa sababu ya chunusi.

Inaeleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa wakifanya mapenzi wamekuwa wakiona ngozi zao ziking’aa baada ya kufanya mapenzi lakini hali hiyo haimaanishi kuwa kufanya au kutofanya ngono ndiyo chanzo cha chunusi.

Ufafanuzi wa Daktari kuhusu uhusiano wa kutokujihusisha na tendo la ndoa na kupata chunusi.

Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Ndani, Elisha Osati anafafanua kuwa hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha madai haya.

"Kwa ufupi: Hapana, hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaothibitisha kuwa kutojihusisha na tendo la ndoa kunasababisha machunusi usoni.

Hii ni dhana potofu zinazojulikana sana kuhusu afya ya ngozi. Chunusi husababishwa zaidi na mambo makuu manne ambayo hayahusiani kabisa na kufanya au kutofanya tendo la ndoa."


Je, ni wapi ilipotokea dhana hii? Kwa mujibu wa Dkt. Elisha

Daktari Elisha anaeleza kuwa;

Wazo la kwamba kutofanya tendo la ndoa kunasababisha chunusi—au kwamba kufanya tendo hilo kunaweza kuondoa chunusi, hutokana na uelewa mdogo kuhusu hormone:
  • Kuingiliana kwa Umri wa Balehe: Kipindi cha balehe ndipo hormone za uzazi (kama testosterone na estrogen) zinapoongezeka kwa kasi, jambo linalopelekea kuongezeka kwa hamu ya tendo la ndoa pamoja na kuongezeka kwa chunusi. Kwa sababu mambo haya mawili hutokea katika umri mmoja, watu kihistoria walitengeneza UHUSIANO wa UONGO kati ya mambo hayo.
  • Tendo la ndoa husaidia kutoa hormone za oxytocin na endorphins huku zikipunguza cortisol (hormone kuu ya msongo wa mawazo). Kiwango kikubwa cha cortisol kinaweza kuchochea chunusi kwa kuongeza uzalishaji wa mafuta kwenye ngozi.
Ingawa kupunguza msongo wa mawazo kunaweza kusaidia afya ya ngozi kwa ujumla, kufanya TENDO LA NDOA SI TIBA ya chunusi, wala kutofanya tendo hilo hakuidhuru ngozi yako.
Back
Top Bottom