Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Fuatilia jamii za wakulima na wafugaji. Utaona wakulima ni wafupi sana. Watu warefu kabisa Afrika wote ni wafugaji. Wadinka na wasudan kusini wengine, Wamasai, Watutsi, wahausa n.k, na hata kwa kawaida wabantu si warefu (sababu ya lishe duni), lakini Wukuma na Wakurya ni warefu sababu ya kupiga maziwa.
Cheki wakulima, waluguru, wakinga, wapare, wangoni, n.k, wengi wao wafupi wafupi, shida ni hawapati maziwa.
Mtu kuwa mrefu inambidi kuwa na mifupa mirefu na imara. Na mifupo hiyo hutengenezwa na madini ya Calcium. Na maziwa ni moja ya chakula, kama siyo kinachoongoza kuwa na calcium kwa wingi. Pia mifupa imara inahitaji vitamin D kwa wingi, maziwa yanayo ya kutosha. Wafugaji wanapiga pia nyama ambazo zinawasaidia kupata protini za kujenga mwili.
Mwandishi mmoja alisema kuwa binadamu alipoanza kulima afya na lishe yake vilianza kuzorota. Anasema walioishi kwa kuwinda na kukusanya kama walivyo mabushmen, walikuwa na Afya njema kuliko wakulima.
Tujitahidi kunywa maziwa kuepuka ufupi.