Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Process ilienda vizuri tu kwanzia kuomba ushauri kwa wahispania hadi kwenye kuandaa katiba mpya iliyoendana na mfumo mpya wa mabadiliko, hii katiba ilipitishwa na wanachama wote wa klabu ya Yanga siku ya mkutano mkuu na pia serikali iliipitisha hiyo katiba sasa sijui ni nini kilitokea hadi isisajiliwe RITA wakati kila kitu kilikuwa sawa? Hapa ndipo kwenye udhaifu na ndipo kwenye hoja za akina Magoma maana inaonekana hadi sasa katiba inayopaswa kutumika ni ya mwaka 2010.
Kingine naona pia kuna wazee waliopo kwenye hizi timu za kariakoo wana mawazo ya kuendeleza hizi timu kwenye umaskini wa kutembeza bakuli. Alikuwa Kilomoni na kundi lake kasumbua sana mchakato wa Simba ilihali hao wazee wakiachiwa timu hakuna maendeleo yeyote yale. Leo hii Simba na Yanga zitaonekana tishio Africa na wanakuwa na muendelezo mzuri mashindano ya kimataifa kutokana na uwepo wa hawa wadhamini ila wao ni kukazanai kukwamisha hawa wadhamini na wawekezaji ili mradi tu vipate ulaji kwenye hizi timu.