Uchaguzi 2020 Kutokuwasiliana kwa viongozi wakuu wa ACT-Wazalendo na CHADEMA kumewapa mwanya CCM kufanya watakavyo

Uchaguzi 2020 Kutokuwasiliana kwa viongozi wakuu wa ACT-Wazalendo na CHADEMA kumewapa mwanya CCM kufanya watakavyo

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,947
Reaction score
7,939
Kutokuwasiliana kwa viongozi wakuu wa ACT Wazalendo na CHADEMA kumewapa mwanya CCM kufanya watakavyo. Suala la mapingamizi ni suala nyeti hivyo linahitaji nguvu kubwa.

Kipindi Cha Korona mbowe alichachamaa Kila siku mfululizo na speech zake zilipatikana kirahisi kwenye social media. Iweje leo amekaa kimya . Iweje wagombea waende tume peke yao badala ya kwenda na viongozi wao.

Inawezekanaje kupata muda wa kuridhiana na TBC mkashindwa kupata muda wa kuweka presha kubwa kwa tume. Au Mbowe na Chadema mmekubali udhalimu huu wa kuengua wagombea?

Kazhia hii sio ya kushughulikiwa na chama kimoja. Zitto Mbowe ondoeni tofauti zenu kwa maslahi ya upinzani demokrasia na utu ustaarabu na maendeleo ya taifa.

Nawaagiza Mbowe Seif Lisu, Zitto kaeni pamoja itisheni mkutano na media. Pelekeni malalamiko yenu balozi na jumuiya za kimataifa . Toeni siku moja msifanye kampeni nendeni DODOMA kuwasilisha uhitaji wa majibu ya rufaa .

Mbowe kama mwenyekiti hukupaswa kugombea ubunge . Kugombea kwako kunaathiri sana mikakati na utekelezaji wa kampeni. Next time achia Jimbo Kama Mnyika.
 
Haya CCM yamewatega Wapinzani katika hilo. Wakilegeza tu katika hili basi hata matokeo ya wabunge yataibiwa kimabavu.
 
Kuna sehemu nimesoma matamako kadhaa ya Lissu kama ifuatavyo:


“Tume ya Uchaguzi isimamie Uchaguzi wenye wagombea wa CCM na wa Vyama vingine, kuengua Watu namna hii hakujengi Nchi kutabomoa Nchi, kama Tume haitowarudisha wagombea tutaungana na ACT Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nchi nzima" -LISSU


"Malawi ni ka-Nchi kadogo Wagombea hawaenguliwi, wanasaidiwa na Tume kujaza fomu, pale ambapo Mtu haelewi Msimamizi anamsaidia kujaza fomu, hakuna anayeenguliwa Malawi,Kenya na Nchi nyingine zenye Demokrasia, Tume iwarudishe walioenguliwa" -LISSU




Kuonyesha kuwa Lissu naye ameamini wagombea wao hawakujaza fomu vizui ila anataka Tume iwasaidie kujaza formu hizo.

Anasahau kuwa yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kwenda kuweka mapingamizi dhidi ya fomu za Magufuli na Lipumba.

Sheria za Malawi na kenya siyo zinazofanya kazi Tanzania; nadhani hapa Lissu haimbi wimbo wa mkuki kwa nguruwe!
 
CCM wameshaanza kukata tamaa,hilo halina mjadala maana hata wale waliojiaminisha wamepita bila kupingwa wameanza kukurupuka ,hisia zimewapelekea kuona hali si shwari tena,watu wakishakula mziki wa bure hawasubiri mjumbe ahutubie.
 
Propaganda mfu jinsi Lissu alivyokuwa anawasaidia Mabeberu watuibie raslimali?
Ndio tunawaambia tafuteni propaganda nyingine kwani hiyo imebuma na watanzania wameipuuza.

Pikeni uongo mwingine!
 
Haya CCM yamewatega wapinzani ktk hilo. Wakilegeza tu ktk hili basi hata matokeo ya wabunge yataibiwa kimabavu.
Umeona mbali CCM wanatazama reaction . Mpaka Sasa hakuna reaction watu wamejiloga kwenye Mikutano ya Lisu na kusahau wajibu mkubwa . Utakataje watu 500 kizembezembe na ikapita hivihivi. Waende Dodoma watoe siku moja .

Inaonekana Zitto hawezi kukaa na Mbowe na inawezekana Mbowe anafurahia ACT kupokwa viti Pemba akiwinda kuwa KUB.

Ukweli Ni Kwamba wakiacha haya yatokee yatakuja maovu zaidi kwani hata huo ubunge hawatatangazwa kamwe.
 
Majibu ya rufaa ya mapingamizi yatatolewa tarehe 10/09/2020 ngoja tusubili itakuwaje
 
Inaonekana Zitto hawezi kukaa na Mbowe na inawezekana Mbowe anafurahia ACT kupokwa viti Pemba akiwinda kuwa KUB.
Kama hili lina ukweli basi ni tatizo kubwa ktk ukombozi wa nchi yetu.
 
Kuna sehemu nimesoma matamako kadhaa ya Lissu kama ifuatavyo:

Kuonyesha kuwa Lissu naye ameamini wagombea wao hawakujaza fomu vizui ila anataka Tume iwasaidie kujaza formu hizo. Anasahau kuwa yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kwenda kuweka mapingamizi dhidi ya fomu za Magufuli na Lipumba. Sheria za Malawi na kenya siyo zinazofanya kazi Tanzania; nadhani hapa Lissu haimbi wimbo wa mkuki kwa nguruwe!
Dah hili bandiko lako limebifanya niwaze na kuelewa mantiki yako. Tundu Lissu kama mgombea wa Urais Mara kadhaa kaonekana akisisitiza kwamba Tume ilipaswa kuwaongoza wateuliza katika ujazaji form lakini pia anasisitiza huruma ingetendeka.

Lakini hapo hapo yeye aliongozo kuwawekea wagombea wa CCM na CUF mapingamizi tena kwa vitu ambavyo ni vidogo tu kama sahihi na picha, sasa kama chama kilichokaa madarakani, tena mgombea ambae n rais mwenye wasaidizi lukuki kwa muktadha wake kaona anaweza kosea ujazaji form, kwann iwe kitu cha ajabu kwa mgombea udiwani tena aliyeko kijinini asiye na wasaidizi.

Hivyo basi Lissu anakosa Moral Rights ya kuwatetea walionguliwa kwa kukosea kujaza vitu vidogo na huruma haipaswi kutumika bali sheria kama yeye alivyowawekea mapingamizi wagombea wa vyama vingine.
 
Wamiliki wa hivi vyama Zito na Mbowe walitumuana kwa aibu kubwa walipokuwa pamoja.kila mtu apambane kivyake,CCM daima.
 
Shida pingamizi wamewekeana wao kwa wao,kwa mfano mgombea wa CHADEMA ubungo kawekewa Pingamizi na ACT Wazalendo
 
Back
Top Bottom