Kutokwa na damu bila mpangilio ukeni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Tatizo hili huwasumbua wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa na baadhi ya wanawake ambao tayari wameshafikia ukomo wa kuzaa.
Kwa mwanamke aliyekwishafunga kupata hedhi kuendelea kupata damu ya hedhi au kutokwa na damu ukeni bila ya mpangilio siyo hali ya kawaida.

Mwanamke anaanza kuvunja ungo kuanzia umri wa miaka 12 na hufikia ukomo kuanzia umri wa miaka 45. Kupatwa na damu ukeni chini ya umri wa miaka 40 kuna vyanzo vingi kama tutakavyoona.


Chanzo cha tatizo
Damu kutoka bila ya mpangilio kwa mwanamke ambaye hajakoma hedhi husababishwa na mabadiliko katika mfumo wa homoni endapo hazipo sawa Hormonal Inmbalance.' Uwepo wa uvimbe katika kizazi na matumizi ya dawa za homoni mfano sindano au vipandikizi. Kuweka kitanzi katika kizazi pia huwafanya wanawake wengine wapate hali hii ya kutokwa na damu bila mpangilio.

Mabadiliko ya mfumo wa homoni huweza pia kusababishwa na mshtuko wa mwili au hali ya mabadiliko ya mazingira.
Kuharibika kwa mimba pia ni mojawapo ya sababu kubwa. Mwanamke mwenye umri wa zaidi ya miaka 45 kupata damu ukeni bila ya mpangilio ni vema kuchunguza kwa undani kwani wana uwezekano mkubwa wa kuwa na saratani ya kizazi au shingo ya uzazi.







Dalili za tatizo

Mwanamke hulalamika kuona siku za hedhi zaidi kuliko kawaida yake, au kuona katikati ya mzunguko yaani aliona, ikaacha sasa inaanza tena.


Damu inaweza kuwa nyingi na mwanamke akabadilisha pedi mara nyingi kuliko kawaida yake au akapata kidogokidogo lakini kwa muda mrefu.

Damu inaweza kuwa nyepesi au nyeusi au nzito na mabonge. Hutoa harufu isiyo ya kawaida endapo ata-bleed kwa muda mrefu.
Ikiwa na mabonge huambatana na maumivu.

Mgonjwa huchukua muda mrefu hata zaidi ya majuma mawili akiwa anatokwa na damu, endapo hatapata tiba haraka huanza kuumwa tumbo chini ya kitovu ikiwa ni dalili za kupatwa na maambukizi ya kizazi kwa kuwa bakteria hupenda sana mazingira ya damu.


Hali inapoendelea mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba na huathiri uzazi kwani hushindwa kufanya tendo la ndoa, homoni zinavurugika na maambukizi ya kizazi huathiri mirija ya mayai.

Uvimbe wa Fibroid ukiwa ndani ya kizazi husababisha damu zitoke bila ya mpangilio na kuzuia mimba kukua na hata ikiingia inaweza isiendelee.

Uchunguzi
Tatizo hili ni sugu na huleta athari kubwa katika mfumo wa uzazi wa mwanamke hivyo ni vema uchunguzi wa kina ukafanyika katika hospitali kubwa. Vipimo vya damu kuangalia mfumo wa homoni, kipimo cha Ultrasound kuangalia kizazi na vifuko vya mayai pia hufanyika.

Ushauri
Usidharau tatizo hili la kutokwa na damu bila mpangilio ukeni ukiwa bado binti au mtu mzima kwani madhara yake ni makubwa. Muone haraka daktari kwa uchunguzi na tiba.

Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App +905013460377
 
Asante MziziMkavu kwa somo zuri,vipi na kama mtu ana tabia ya kuruka miezi? Anaweza kukaa miezi 2 au 3 bila kupata kisha akija kupata anaweza akaenda muda mrefu sana au mfupi sana
 
Last edited by a moderator:
Mzizi mkavu vpi kama mtu alipata mimba ikaharibika kashika nyingne stil ana bleed tu tatizo nini mana my wii ana hlo tatizo alipga na ultra sound wakampa antio biotic ya kukausha sijue ni viumbe
 
asante sna doctor somo zuri linatusaidia kujitambua zaid
 
Mzizi mkavu vpi kama mtu alipata mimba ikaharibika kashika nyingne stil ana bleed tu tatizo nini mana my wii ana hlo tatizo alipga na ultra sound wakampa antio biotic ya kukausha sijue ni viumbe
Muache kwanza atumie hiyo Antibiotic isipo msaidia utaniona kwa wakati wako ninaweza kuisimamisha hiyo damu yake inayoendelea kutoka.
 
Naomba msaada ninamdogo wangu anaumri wa miaka 28 alikuwa na mimba ikaharibika mwezi wa kumi na mbili na akasafishwa akapona ila tangu hapo zikifika tarehe zake zakuingia period anaumwa sana tu kwa muda wa siku 3 au 4 ila damu haitoki ameenda hospital akafanyiwa utrasound nakuonekana hamna tatizo na akapewa dawa za kurekebisha hormone ila bado hazijamsaidia anaumwa sana tumbo zikifika tarehe yake na hapati msaada.Tafadhali naomba msaada wako ili aweze kupata period.Please mzizimkavu.ASANTE SANA
 
TIBA YA HEDHI ISIYOTOKA VIZURI:

Chukua Jirjir (rocket) kijiko kimoja ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje. Kunywa

kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara tatu kwa muda wa siku 3.
 
nina tatizo ambalo linaanza kunitisha. Lilianza mwaka 2012 ambapo nlipata period kwa siku 17 nikafanya vipimo nikagundulika ni hormonal imbalance. Nikapewa dawa ikastop
mwaka 2013 ikanktokea kitu cha ajabu baada ya siku 15 ya mzunguko wangu, instead of getting discharges rangi nyeupe nikawa napata na some blood kidogo. Nilifanya vipimo ila hakuna kilichoonekana nikashauriwa nisitumie dawa. Ile hali ikaisha baada ya wiki mbili.
Hivi karibuni tena imenitokea juzi siku ya 15 ya mzunguko nimeona damu kidogo.
Naombeni ushauri maana naanza kujipanic. Nilipiga ultra sound 3 times.

Preta Mzizi mkavu
 
Last edited by a moderator:
Nenda tena kafanye vipimo tena kuhakikisha huna matatizo yaliyokutokea hapo mwanzo.
 
Naomba msaada doctor ....Mimi Nina umri wa miaka 26 ...tatizo langu siku zangu za hedhi hazipo kama zaman...zamani ilikuwa 28 days ...lakin sasa Mara nyingi ni siku 21....na hili tatizo limeanza mwaka 2013 mwanzoni...je nifanyeje niweze kurudia mzunguko Wang wa mwanzo...na je ni athali gani naweza pata tatizo likiendelea......!?
 
Ni kawaida kwa mwanamke kutokea kwa mabadiliko ya siku zako inaweza kuwa unawahi siku zako au zinachelewa . Ningekushauri uende hospitali kuangalia isije kuwa una matatizo ya Hormone.Wahi muone Daktari doch
 
Last edited by a moderator:
asante doctor Mzizi Mkavu..nimejifungua mirz mitano iliyopita..tangu nimejifungua sijaona siku zangu ila inafika wakati naona vitone vya damu kwa siku kama 2 vinakata na narud kawaida na huwa sina maumivu yeyote..tangu imenitokea ni kama miez 2 imepita.sasa juzi imetokea tena na jana vitone vya damu baadae ikaisha sasa nipo safi.Je; inawezekana nina tatizo lolote? na je lini naweza kuziona siku zangu kawaida.?
 
Nenda kamuone Daktari akupime ndipo itajulikana afya yako.
 
Kuna Dada yangu ana miaka 47 bado anapata hedhi mpaka sasa hivi na anasema kila baada ya siku 28 anaona siku zake lakini wakati mwingine anaenda mpaka siku 10 ana breed, mwezi uliopita alienda siku kama 6 ila sasa hivi kunawakati anasikia vimaji vyeupe vinatoka ukeni lakini havina harufu mbaya, sasa anauliza au anataka kukoma hedhi kwa hizo dalali? Na anasema anatokwa sana na jasho usiku wakati amelala na huwa anakosa usingizi na kichwa kinamuuma.
Ahsante doctor
 
Ndio Dalili ya kukoma hedhi ila ninamshauri aende kumuona Daktari ikiwezekana.
 
mimi nina tatizo ambalo limeanza mwezi wa tisa, mwezi wa tisa nilichoma sindano ikaisha mwezi wa 12 tar 22 sikuchoma tena, mwezi huo wa 12 nilipata siku zangu kawaida ila kwa muda mrefu kidogo nikaenda hospital nikaambiwa ni kawaida ila nilipewa antibiotics, mwezi huu wa kwanza nilpata siku zangu tena tar 26 jan, kawaida tu siku 4, ikakata ila ilikuwa ni mabongebonge, cha ajabu tar 6 feb tena nikapata siku zangu kwa siku 8 damu nyeusi nikaenda kwa docter akanambia nisubiire kwanza, na sikupewa dawa yoyote sasa najiuliza tatizo ni nn? maana nina wasiwasi ndo kwanza nina mtoto mmoja na umri wangu ni miaka 28
 
This
Mkuu naomba nipate namba yako
 
Cervix cancer is on the go
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…