Kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito

ministrant

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
754
Reaction score
1,478
Habari za jumapili wana jukwaa. Kwa wale walio wakristu nawatakia maandalizi mema kwa kuanza juma kuu ikiwa leo ni jumapili ya matawi na jumapili ya mwisho ya kwaresma kuelekea sikukuu ya Pasaka.

Napenda kuchukua nafasi hii kuomba ushari na maoni yenu aidha unaotokana na taaluma zenu kama vile udaktari ha kadhalika uzoefu wenu hasa kwa wale ambao tayari ni wazazi.

Nimepokea taarifa za kunishangaza kidogo kutoka kwa mtu wangu wa karibu ya kuwa mke wake huwa anatokwa na damu ukeni wakati wa tendo la ndoa au pindi anapokuwa anafanya kazi ngumu kama vile kuchota maji.

Walijaribu kufika kituo cha afya na baada ya vipimo daktari alibaini kuwa ana UTI kali hivyo aliandikiwa sindano 5 ambazo alichomwa kwenye mishipa pamoja na vidonge ambavyo alitumia kwa muda wa siku tatu.

Cha kushangaza ni kuwa hali bado haijakoma na mara ya mwisho aliposhiriki tendo la ndoa na mke wake hali ya kutoka damu ukeni ilijirudia.

Kitu kinachompa wasiwasi zaidi hali ya mtoto kucheza tumboni inazidi kupungua tofauti na hapo awali. Umri wa ujauzito ni miezi 3.
Ushauri wenu tafadhali.
 
...awahi kwa gaino wake, ingawa sio dokta ila kuna kila dalili za miscarriage, wife alipoteza ujauzito kwa kutoka damu, take it serious na wahi hospitali tena kwa gaino...
 
...awahi kwa gaino wake, ingawa sio dokta ila kuna kila dalili za miscarriage, wife alipoteza ujauzito kwa kutoka damu, take it serious na wahi hospitali tena kwa gaino...

Nashukuru mkuu kwa ushauri
 

Mshauri jamaa yako aende kwa specialist wa wanawake haraka sana. Thats a serious issue(its a danger sign actually), i did not see the patient ila hiyo diagnosis ya UTI kwa hiyo dalili ya kutokwa damu baada ya sex naona si sahihi.
Halafu miezi mitatu keshaanza kusikia mtoto akicheza?? Anyways,mshauri as i told u, aende kwa specialist amuevaluate vizuri asije kupoteza hiyo mimba.
 
Hilo tatizo baya sana kwani lilimtokea mke wangu na tukapoteza mtoto
 
Miezi 3 ya ujauzito mbona mapema sana kwa mtoto kuanza kucheza tumboni. Mtoto huanza kucheza tumboni juma la 20 tangu kutungwa kwa mimba ni sawa na miezi 5, na ndo wakath moyo wa mtoto huanza kufanya kazi ya kusukuma damu.
 
Kipindi cha uja uzito ni kipindi cha kuwa papmpered na kupata matunzo mazuri kwa kujiandaa kumleta kiumb mwingine duniani.

Ni kipindi cha kufanya vikazi vyepesi, mazoezi mepesi na kula vizuri.

Kuchota maji ni big NO. Ni wazi kuwa tendo la ndoa linamuathiri.

Huyo baba nae si aache kwani lazima???
 
Wanasema hivi Kama anasikia maumivu makali tumboni na mimba say ni miezi 2,aende aka pime ultrasound kujua Hali ya mimba ikoje,mi jirani yangu imemtokea Kama hiyo,wengine husema mimba ikiwa chini ya miezi 3 hakuna mapito yoyote ya moyo,wengine husema hizo ni dalili mbaya ya mimba muweza kutoka,wengine husema huenda ni dalili za mapacha,apige ultrasound then Kama wasilione chichote akae baada ya wiki 2 aende tena kupiga ultrasound ili kujua ukuaji wa mimba Kama inakua au kiumbe hakuna uhai!wenye uzoefu mnaweza kuchangia Pia Mzizi Mkavu et all.....
 
Tatizo bado linaendelea au amepata tiba? Tuwasiliane kama bado, kuna dawa anaweza akatengeneza mwenyewe akawa anakunywa kama juisi ili kuzuia kutoka mimba!
 

pumzikeni kufanya sex kwanza,mpeleke hospital akachekiwe,breed kipindi cha ujauzito si kitu kizuri..kucheza kwa mtoto miezi mitatu duh???!!mi najua miezi 5 wengne huwahi mitano kasoro...
 
Aende hospitali
Afanye utrasound
subchoronic hemmorage (sina uhakika na spelling ) SCH pia huleta bleeding kwa wajawazito
 
Mimba itakua imetishia kutoka. mwambie asifanye kazi ngumu, ashiriki kwa umakini tendo la ndoa.
 
Kutokwa na damu ukeni wakati wa mimba changa

Hii ni hali inayoweza kujitokeza kwa mama mjamzito hasa katika kipindi cha umri wa mimba chini ya wiki ya 28. Baadhi ya sababu zinazoweza sababisha ni

i) Kutoka kwa mimba\

ii) Mimba nje ya mji wa uzazi

iii) Uvimbe ktk kondo la nyuma(placenta)

iv) Sababu za kienyeji

Leo ningependa tuiongelee kidogo maada ya utokaji wa mimba (Abortion) ikiwa ni moja ya sababu ya utokaji damu kwa mwanamke kwenye mimba changa.

Kutoka/kutolewa mimba (Abortion)

Hiki ni kitendo cha kutoa mimba kabla haijafikisha wiki ya 28 kutokana na sababu mbalimbali. Ikumbukwe kuwa katik anchi yetu kitendo cha kutoa mimba kwa makusudi ni kosa la jinai.

Ili kuzitambua sababu za kutoka kwa mimba ni vyema tukajua kwanza aina za utokaji wa mimba na ndipo tutajua na sababu zake.

Aina

Mimba inayotishia kutoka (Threatened abortion)

Hii ni mimba inayotihia tu kutoka ila haitatoka kama tahadhari zitachukuliwa mapema. Hii huwa na sifa zifuatazo;kutoka damu kidogo ukeeni na maumivu ya tumbo lakini njia (cervix) inakuwa haijafunguka.

Aina hii mara baada ya kuigundua inatakiwa mama huyu awe na mapumziko (bed rest) atumie dawa ya kutuliza maumivu na asifanye mapenzi.

Mimba ambayo ni lazima itoke( Inevitable abortion)

Hii ni mimba ambayo kwa namna yoyote ni lazima itatoka kwani njia ya kizazi huwa tayari imekwisha funguka na hivyo inaweza pelekea masalia ya mimba kutoka yote au kubakiza baadhi.


Mimba iliyotoka lakini imebakiza masalia yake (Incomplete abortion)

Huwa na sifa zifuatazo kwasababu ya yale masalia yaliyobakia;kutoka damu ya mabonge ukeni,maumivu ya tumbo,njia huwa imefunguka na mfuko wa uzazi huwa ni mdogo kuliko umri wa mimba

Mimba iliyotoka yote (Complete abortion)

Hii huwa imetoka yote bila kubakiza kitu

Mimba iliyotoka na kubaki uchafu ambayo imeshambuliwa na wadudu hususani bakteria (Septic abortion)

Hii inaweza tokana na mabaki ya mimba ambayo hajatolewa kitaalamu au kufanyika katika mazingira machafu na hivyo mama huyu atakuwa na homa, kutokwa damu kwa wingi, njia ya kizazi itakuwa wazi na atakuwa anatokwa na uchafu wenye harufu sehemu za siri.

Mimba kutoka mara kwa mara zenyewe ( Arbitual abortion)

Aina hii mara nyingi mimba zinakuwa zinatoka zenyewe na ni lazima iwe imejirudia zaidi ya mara 3 ktk historia ya mama.Ni muhimu sana kwa kila mama mjamzito kuhudhuria kliniki bila kujali hadhi yako.

Mimba ambayo imepoteza dalili zake ( missed abortion)

Inatokea kwa mama mjamzito kupoteza dalili za mimba wakati alikuwa mjamzito na tumbo lake la uzazi likawa dogo kuliko umri wa mimba.

Mimba inayotolewa kwa utaratibu wa kitiba ( therapeutic arbotion)

Hizi ni mimba ambazo zinatolewa kwa kitiba ili kunusuru maisha ya mama ama kutokana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaonekana kuhatarisha maisha ya mama. Hii inategemea sana maamuzi ya daktari na jinsi alivyoona.

Utoaji mimba usio salama/jinai/ (Unsafe/criminal abortion)

Utoji mimba hauruhusiwi katika nchi yetu na ndo maana unaitwa jinai lkini kitaalamu tunaita utoaji usio salama. Aina hii hufanyika kwa njia mbalimbali ambazo sitazitaja hapa kwasababu za kimaadili.

Makundi makubwa wanao fanya aina hii ambayo ni hatari kwa mtoaji na mtolewaji huwa ni wake za watu wasio waaminifu kwa ndoa zao, wanafunzi, wanaotumia vibaya uzazi wa mpango, waajiriwa wapya kama masharti ya kazi yamekataa, wanaotoka familia zenye misimamo mikali ya kidini lakini wao wamekiuka imani zao na wale wa mimbba zisizotarajiwa.

Hatari za utoaji mimba

zinazofahamika ikiwa ni pamoja na kupasua tumbo la uzazi, kutokwa damu nyingi na kupata maambukizi

Matibabu

Ni muhimu sana kumwona daktari hospitali au kliniki inayofahamika kisheria na utaratibu na si maduka ya madawa​


[h=1]Topic: Kutokwa na damu ukeni wakati wa mimba changa[/h]
 
Pole Mkuu.Wahi hospital Nina imani shemeji atakuwa na Daktari wake.
 
Habari za leo wapendw, napenda kuchukua nafas hii kuomba ushauri kwa wataalam wa mambo ya uzazi. Nina mdogo wangu alikuwa na mimba ya miez mitatu (3) ghafla akatokwa na damu sehem za siri ikabid twende hospital wakampeleka kweny kioo ikaonekan mimba imeharibika akapewa dawa ya misoprost baada ya mda ikawa imetoka akasafishwa, wakamrudisha tena kwenye kioo ikaonekana kuna uchafu bado ikabid apewe dawa ya kutumia kuweka sehem ya siri, imeandikwa cytotec, baada ya hap kuna uchafu ulikuwa unaendelea kutoka. Na damu kidogo imechukua mwezi, ikabid arudi hospital akamuulezea doctor wakamwandikia dawa ya ciproth, doxycycline na metro, akatumia. Lakn kuna wakat uchaf unatoka mweus mda mwingne damu inaweza kukata kwa siku kama mbili ya tatu ikarud tena damu kwa mda wa dakika 1 ikakata na damu kidogo Sana. Naombeni ushauri nimeshindwa kwann hali hii haikomi miezi miwili sasa inaelekea kuisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…