Kutokwa na jasho mwilini

Kutokwa na jasho mwilini

Victor Bravo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
265
Reaction score
241
Habari wakuu wa jukwaa hili
Nimejitokeza hapa nina walau maswali mawili, moja ivi nini kinasababisha mtu kutokwa na jasho saana hasa maeneo ya kwapa wengine mgongoni.. Yaani unakuta mtu katembea tu umbali mfupi saana lakin mgongo wote umeloa au kwapa lote limeloa, naomba kujua je ni mwili unakua na shida au ni kawaida tu ya maumbile

NB. Jasho hili linakua la kawaida tu sie lile la harufu kaali, hili hata ukikaa naye usikii kikwapa wala harufu ya kukera.

Swali la pili
Inatokea mtu ni smart sana anaoga vizuri hata mara tatu kutwa au zaidi na anajisugua vyema kabisa lakini kwenye nywele za kwapa au sehemu za siri kunakua na zile nywele zenye utando utando mweupe ivi, japo na zenyewe hazitoi harufu ya kuukera I mean kikwapa. Je shida ni nini inawezekana tatizo hili likaisha?
Shukrani.
 
Hapo inategemea mtu na mtu aisee...kwa ufafanuzi zaidi ngoja wataalam waje
 
Hihiiiiiiii kwapa limekuwa la kihenga mvi kibaooo, ila kwa upande wa kwapa, dawa ni kunyoa mara kwa mara tu mkuu, kwa jasho jingi makwapani, hayo ni maumbile tu mkuu ya ntu na ntu
 
Tuwasubiri wataalamu.

ila mimi kuna shati nikivaa tu hata kabla ya kutoka huwa linalowa jasho makwapani ila nikivaa nguo nyingine hata nitembee kwenye jua vipi nakuwa poa tu huwa nashindwa kuelewa tatizo ni nini?
 
Tuwasubiri wataalamu.

ila mimi kuna shati nikivaa tu hata kabla ya kutoka huwa linalowa jasho makwapani ila nikivaa nguo nyingine hata nitembee kwenye jua vipi nakuwa poa tu huwa nashindwa kuelewa tatizo ni nini?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mashati ya kubana hayoo
 
Back
Top Bottom