Kutokwa na mkojo bila mpangilio

Kutokwa na mkojo bila mpangilio

delako

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2012
Posts
2,902
Reaction score
1,875
Habari wana JF,

Naomba msaada wenu tafadhali, kwani mke wangu ni mjamzito wa miezi saba sasa. Ameanza kutokwa na mkojo bila mpangilio leo hii na wala haumuumi! Je ni hali tu ya kawaida au kuna tatizo hapo? Ni uzazi wake wa 3 sasa na ana miaka 35.

Naombeni msaada na ushauri pia.
 
Ni vigumu kujua tatizo kwa maelezo ya sentensi moja. Sidhani kama ni Fistula maana mara nyingi Fistula hutokea baada ya kujifungua ( kwa njia ya kawaida, sio operation), lakini huyu bado ni mja mzito. Mpeleke Hospitali kwa uchunguzi kaka.
 
Ni vigumu kujua tatizo kwa maelezo ya sentensi moja. Sidhani kama ni Fistula maana mara nyingi Fistula hutokea baada ya kujifungua ( kwa njia ya kawaida, sio operation), lakini huyu bado ni mja mzito. Mpeleke Hospitali kwa uchunguzi kaka.

Ahsante kwa ushauri.
 
Kweli kitu cha kwanza kbs mpeleke hosp,.ila hiyo kitu pia inatokana na kuzaa mfano zaid ya watoto watatu wanawake wengi misuli ya uke inalegea,hata kama mwanamke hana mimba anakua anakojoa kojoa mara kwa mara mara anajikuta vikojo vimetoka kabla hajafika chooni,hilo tatizo pia linawatokea wanawake wengi wajawazito mimba ikiwa kubwa but mimi sio dokta kwahiyo cjui zaidi sababu za kitaalam hiyo ni kutokana na uzoefu wangu kwani hata dada yangu alikua hivyo tena yeye kila mara anabanwa mkojo n mkojo unaotoka ni mdogo
 
Mrejesho,
Nawashukuru wote mlionipa ushauri na namshukuru mungu amejifungua salama mtoto wa kike.alijifungua juzi tarehe 14/02/2015
Ahsanteni sana
 
Back
Top Bottom