Kutolewa Ureno WC26, Mambo haya Matatu Yamewaponza

Kutolewa Ureno WC26, Mambo haya Matatu Yamewaponza

Kwa sababu sikusema kabla ya mashindano kwahiyo ni kubali Roberto Martinez ni kocha mzuri au CR7 anafaa kuanza kikosi cha kwanza.?
Hata Argentina akitolewa mtakuja na ngonjera mpya
 
Kumbuka pia timu nyingi zimeonesha ushindani wa hali ya juu saana ktk hili kombe.

Game ya jana, Ureno walidhibitiwa kila sehemu na Spain. Spain angekuwa na namba 9 nzuri, Portugal alikuwa anakufa hata goli 3 mapema tu.

Pedri, Rodri na Olmo wameonesha uwezo mkubwa sana dhidi ya wapinzani. So tuone pia ubora wa Spain dhidi ya Portugal ni chanzo cha kudondoka kwa Portugal jana.
Siongelei mechi ya jana tuu.
Ni mechi zote 5 walizocheza, Portugal hawajacheza vizuri kabisa.
 
Hata Argentina akitolewa mtakuja na ngonjera mpya
Hata Ufaransa akitolewa zitatafutwa sababu na zitasemwa.

Hivyo ndivyo watu wenye malengo ya mbali wanafanya hivyo.

Ukishindwa mahali unakaa chini unaangalia ni wapi umekosea.
Ili isijirudie tena.
Na hiki ndicho tunafanya kuchambua mambo ambayo yamepelekea Portugal kutokufanya vizuri licha ya kuwa na wachezaji wazuri.
Hakuna ubaya wala kosa kufanya hivyo.
 
Wengi waliwapa Ureno kufanya vizuri kutokana na kuwa na wachezaji ambao walikuwa na misimu mizuri kwenye ligi zao.

Nuno mendes, Vitihna, Gomes, Bruno, Ruben Dias.
Lakini matokeo yake uamekuja tofauti na matarajio ya wengi sababu kwangu ni hizi.

1. Kocha mbovu.
huyu kocha unaweza kujiuliza inakuwaje anapewa nafasi ya kufundisha timu kubwa hizi.
Hana historia uoyote nzuri.
Kafundisha timu kama Swansea, Wigan na Everton.
Mafanikio yake ni kuchukua FA Cup huko England.

Mwaka 2016 akapewa kizazi cha dhahabu kile cha wakina Hazard, Debruyne, Vicenty Kompany, Jan Vertonghen na Toby Alderweired, Lukaku, Witsel, Fellain, Dembele n.k
Hiki kizazi hakikuchukua hata Euro.

Huyu kocha alikuwa hajui nini anafanya.

Mara Wareno nao wakampa timu.
Matekeo yake ni kucheza mpira haueleweki.
Timu iko slow kutengeneza mashambulizi.

2. Wachezaji wengi wakubwa hawajaonyesha viwango vyao tunavyovijua.
Watu kama Nuno Mendes l, Bruno, Vitihna wameshindwa kabisa kufurukuta.
Na inaweza kuwa ni sababunya kuwa na kocha mbovu.

3. Ureno mechi zote wamecheza wakiwa pungufu.
wAlikuwa na namba tisa wa ovyo sana.

Nimemaliza.
Mimi nasema hiviii: ni bora mara 10wangemchukua kocha Klivu Bakari wa Mnyama.

Simba ya sasa inacheza vizuri kuliko Barcelona, PSG au Manjesta united.
 
Tupe sababu 3 pia na timu zingine kutolewa. Hizi za ureno ni kama za timu zote tu kwahiyo sio kitu kigeni
 
Tatizo kubwa la Ureno ni Kocha mbovu, timu ilikua inashindwa hata kutengeneza mashambulizi, mda wote ipo chini. Kuna wachezaji hawakutakiwa kabisa kucheza, tukianza na Bruno, felix, neto sio wakuanza kabisa.
 
Hata Ufaransa akitolewa zitatafutwa sababu na zitasemwa.

Hivyo ndivyo watu wenye malengo ya mbali wanafanya hivyo.

Ukishindwa mahali unakaa chini unaangalia ni wapi umekosea.
Ili isijirudie tena.
Na hiki ndicho tunafanya kuchambua mambo ambayo yamepelekea Portugal kutokufanya vizuri licha ya kuwa na wachezaji wazuri.
Hakuna ubaya wala kosa kufanya hivyo.
Haya jiandae kuleta ngonjera khs Argentina na Messi wenu, c unaangalia mechi ya leo au?
 
Haya jiandae kuleta ngonjera khs Argentina na Messi wenu, c unaangalia mechi ya leo au?
Kumbe unadhani niko kwenye Messi vs CR7.
Mimi katika Timu ambazo ningefurahi kama wangechukua ni Ureno.
Siko upande wa Argentina hata kidogo.
 
Kumbe unadhani niko kwenye Messi vs CR7.
Mimi katika Timu ambazo ningefurahi kama wangechukua ni Ureno.
Siko upande wa Argentina hata kidogo.
Ndio ujiandae kuleta uchambuzi uchwara, kama huu wa kwenye mada.
 
Back
Top Bottom