Kutomuamini Mungu ni ujasiri?

Control ya variables itafanyikaje tukifanya research kwa hii njia yako hii. Mtu anaweza kuumwa tumbo kwasababu ya Escherichia coli aliyekuwa kwenye maziwa lakini akahisi hilo tumbo linatokana na yeye kutokuosha tunda alilokula hapa majibu atakayotoa kwenye questionnaire ni yatakuwa na ukweli ?

Tunatakiwa kufanya vipimo Kwa mtu tumgundue parasite aliyepo na possibility ya huyo parasite kutoka kwenye source fulani. Hii ndo valid research.


Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Kivipi ni pure drink huku source yake kaiwekea uwezekano wa maziwa kuchanganyikana na viumbe ambao hatuwaoni wanaoweza kutuletea magonjwa?

Kuna wanadamu kawaumba ye mwenyewe ni lactose intolerant na hawa kwao maziwa ni pure drink? Shida Iko wapi angesema tu Kwa baadhi yenu sio pure?

Ndio sawa nirushe nyoka ndani ya chumba halafu nikwambie humo pako salama uingie ukutane nae huku mi nilikuwa najua yumo halafu nijitetee kwamba siwezi kukwambia kila detail kuhusu chumba.

Allah alisema "Kuna viumbe ambavyo tunaviona na ambavyo hatuvioni kwa macho yetu" (naomba na reference ya hili andiko kama hutojali)

Ila hakuona ni muhimu kusema hivyo viumbe msivyoviona kwa macho vinaweza kuwa hatari kwa afya yenu? Detail muhimu kama hii kwanini aliiacha? Jibu dogo tu hapa mwandishi alikuwa hafahamu madhara ya hivi viumbe

Na hata ukitumia mfano wa macho, mtu aliyezaliwa kipofu macho hayaoni utamwambia na yeye mungu kampa macho Kwa ajili kuona? Vivyo hivyo maziwa yenye parasites utaniambia ni pure mungu kanipa ninywe tu bila shida ?

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Okay na yeye kwa kuumna ulimwengu mbovu unaosababisha watu wasiokuwa na hatia wafe, siku ya malipo naye atawajibika kwa uzembe huo?

Au kuna double standard?
Onyesha kwanza uzembe uko wapi ili tujadili.

Sio anao sababisha sahihi anaruhusu haya yote yatokee, ndio maana akaitwa muweza wa yote.

Hao waio kuwa na hatia wanakufa sababu muda wao umefika, kifo sio jambo baya kama nyinyi mnavyo dhani, bali kifo ni haki ya kila kiumbe.

Sasa nataka uonyeshe uzembe uko wapi ili ulichokiandika kiwe kweli.
 
Kujiua sio option kwasababu bado kuna watu wananitegemea mimi kama msaada kwasababu Mungu wakuwasaidia hayupo
Basi usahihi ni kuwa ni jambo la msingi. Thibitisha wapi Mungu hakuwasaidia wakati anawapa uhai na mengine yote, kingine usichokijua hata wewe unaweza usiwepo na hao wanao kutegemea wakaishi tena wakaishi maishi mazuri kuliko Sasa, sababu Allah ndio mpangaji na muendesha mambo.
 
Weka mfano halisi mfano ulio utoa ni mfano mfu.

Mola alipo tuumba akatupa uhuru, tukipenda tumshukuru na tukiamua tukufuru, huo uhuru uko nao wewe pia.

Mola hatuangushii tatizo kama unavyo sema, sababu katika utendaji wake una hekima ndani yake, mitihani anayo tupa ni matokeo ya machumo ya Mikono yetu.

Kwahiyo anajua kabisa hata kabla ya wewe kufanya matokeo yake ni nini. Kwahiyo swali lako halina uhalisia.

Kingine usiandike ulimwengu unao ruhusu maovu kutokea, sababu ulimwengu hauwezi kuruhusu bali Allah ndio anaruhusu haya yote kutokea.
 
Allah anajua hata kile ambacho hakipo kikiwepo kingekuwaje.

Ana njia nyingi za kuwazindua watu bali hata angetaka wote tumuamini angefanya hivyo, ila ameweka utaratibu huu ili tufikie lengo la kuwepo duniani.
 
Imani haina kanuni.

Unaweza kuamini hata mende tu kuwa inawaka mwamga au ndiyo iliumba ulimwengu

Huwa nashangaa sana napoona mtu anaamini katika Mungu!!

Huwa naskitika napoona mtu mmoja akimshangaa au kumkosoa mtu wa imani nyingine (imani tofauti).

Kwasababu wote hawa ni wavunjaji wa kanuni.

Wote hawalazimiki kufuata kanuni.

Wewe uko katika mtazamo wa kwamba watu wote lazima waamini katika Mungu.

Japo ukweli ni kwamba M{i}ungu [hi]huyo ha{i}yupo.

Unawezaje kutaka watu waamini tu hata vya uongo!?

Self delusion is a gift of natural selection.
 
Siyo kwamba mtu anayeamini kwa hofu ya kutishwa na jambo ndiye mtu hatari zaidi katika uso wa dunia hii ukilinganisha na mtu aliye mwema na anafanya yaliyo mema pasipo kuwekewa vitisho?

Viongozi Wangapi wanaamini Mungu na wanahudhuria msikitini na makanisani lakini ni mafisadi na wanatenda yasiyo mazuri!?

Main issue is to respect humanity.

Watu hawaamini kwasababu Mungu hayupo tu, wala siyo issue ya maadili!!

Hata kama nkikubali idea yako ya kwamba watu wawe na hofu ya Mungu ili wawe wema

Swali linabaki habari ya Mungu ni kweli au si kweli!?
 
Anaendesha haya mambo, kuumba, kutoa uhai na mengine mengi.
Mengine mengi ukiwa na maana kuwa yeye ndio controller wa kila kitu?

Au kuna vitu vinafanyika bila ridhaa yake?
 
Onyesha kwanza uzembe uko wapi ili tujadili.
Uzembe ni kuumba ulimwengu mbovu unaoweza kuruhusu watu kufanya maovu ilihali uwezo wa kuumba ulimwengu ulio bora alikuwa nao.

Uzembe wa Mungu ni kuwa na fikra ndogo za kufikiria kuwa lengo la ulimwengu huo mbovu ni kipimo cha kuwapima ili ajue imani zao hao viumbe wake, ilihali yeye ni mjuzi wa kila kitu asiye hitaji kipimo cha aina yeyote kujua chochote.

Uzembe wa Mungu ni kuumba binadamu mwenye madhaifu akaishi kwenye ulimwengu wenye madhaifu, akiwa na mategemeo ya kumuona binadamu akifanya mambo kwa ubora.

Uzembe wa Mungu ni yeye kuona jambo rahisi kwa binadamu ambaye ni dhaifu kuweza kuishi bila kufanya ubaya, ilihali yeye mwenyewe ambaye ni mkamilifu anafanya ubaya kwa kulete mafuriko yanayoua hadi watoto wasio na hatia.
 
Sio anao sababisha sahihi anaruhusu haya yote yatokee, ndio maana akaitwa muweza wa yote.
Kama kuweza kila kitu ni pamoja na kufanya mabaya, vipi bado ataendelea kuhesabika kuwa ni mwenye upendo wote?
 
Hao waio kuwa na hatia wanakufa sababu muda wao umefika, kifo sio jambo baya kama nyinyi mnavyo dhani, bali kifo ni haki ya kila kiumbe.
Leo hii jambazi akaja akambaka mwanao wa miaka mitatu kisha akamuua.

Utaweza kusema kuwa siku yake ilikuwa imefika?

Na kama siku yake ilikuwa imefika, je hiyo haita maanisha kuwa mbakaji hana kosa kwasababu mpangaji wa siku za kuishi sio yeye ni Mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…