Nadhani hapa pana tofauti kidogo kati ya 'NYA' na 'NYE' hapa, mfano mtoto kaniNYEA au kaNYA. Naenda chooni kuNYA au kuNYEA! Kwahiyo utaona pana TENDA na TENDEWA hapo au sio wajuzi?Basi mtu anaweza akasema mvua imeninyenyekea. Na mwingine aweza kusema naenda msalani kunyenyekea.
Kwa hiyo sisi tunafanya COMMON MISTAKES kuwa ndio HALALI, kwa mfano naenda kwenye MAONESHO ya sabasaba wengine (hasa wanaandishi) wanasema MAONYESHO ya sabasaba!Katika kuzungumza ama kuandika lugha huwa kuna:
- Matumizi ya maneno ipasavyo (appropriate wording), ndiyo maana huwezi kusema kumtongoza mwana
- Matumizi ya maneno ili jambo lieleweke zaidi (clear wording)
Kwa hiyo, nadhani wabunge wana ufinyu wa kuelewa lugha.
Basi mtu anaweza akasema mvua imeninyenyekea. Na mwingine aweza kusema naenda msalani kunyenyekea.
Sina tatizo na wabunge hawa wanaoshindwa kujua tafsiri sahihi ya maneno ya kiswahili achilia mbali kiingereza, kifaransa, kijerumani, kichina n.k., tatizo kubwa ni KWETU tuliowachagua kwani MBUNGE ni kielelezo cha WAPIGA kura wake, je hiyo mikataba wanavolilia kuiona na kuipitia SI itakuwa kichekecho na AIBU kwa taifa!Jacobus wabunge wa CCM ni mafisadi viwembe, wasikutishe wala usiwashangae
Juzi katika bunge letu mheshimiwa Tundu lisu alitumia neno 'kutongoza wapiga kura', sasa baadhi ya wabunge wa CCM wakamshutumu kwa kutumia neno hilo.
Nawaomba wajuzi wa kiswahili kuliweka neno hili sawa kwa wanaJF.
Liwe tusi au lisiwe tusi, sitalitumia kwa ndugu wa karibu (kaka/dada/mama/baba/nk). Kinachofanya liwe na ukakasi katika kulitumia, kunafanya lisiwe halali kutumika kwa jamii. Ki-uhalisia, Mh. alilitumia ili kuleta maudhi kwa mtendewa. Hivyo mazingira ya matumizi yake, yanafanya liwe tusi.
Viungo vyetu vya uzazi, si tusi. ila kiuhalisia havitakiwi kutajwa hadharani. basi vinapotajwa hadharani, huleta maana ya tusi.
Kutongoza siyo tusi. Ni kiswahili sanifu cha zamani sawa na shawishi