Kutopandisha walimu madaraja kwa kuwa na mashauri ya kinidhamu ni kukiuka katiba ya Nchi, Ibara ya 13: 6(b)

Kutopandisha walimu madaraja kwa kuwa na mashauri ya kinidhamu ni kukiuka katiba ya Nchi, Ibara ya 13: 6(b)

TRAT

Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
73
Reaction score
160
Baadhi ya walimu waliositahili kupanda madaraja ya kiutumishi 2023 hawajapandishwa vyeo vyao kwa sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu ni walioko masomoni, walio likizo bila malipo na walio mashtaka katika kamati za kinidhamu katika wilaya mbalimbali kwa makosa mabalimbali.

Kutompandisha mwalimu daraja la cheo kwa sababu ana kesi ya kiutumishi ni kukiuka katiba ya nchi ibara ya 13 ibara ndogo ya 6(b) inayopiga marufuku mtu aliyeshitakiwa kutendewa kama mtu mwenye kosa mpaka itakapothibitika kuwa ana hatia ya kutenda kosa. Kama akishinda kesi, au akapewa hukumu ndogo tofauti na kutompandisha cheo.

Mtumishi hataweza kuwa tena na daraja sawa na rika ya watumishi alioanza nao kazi kama Raisi Samia anavyotaka watumishi wa rika moja ya kiutumishi kuwa sawa mishahara. Ukiukwaji huu wa katiba ni kanuni mbovu za TSC zinatotungwa na watumishi wake wasio na uelewa wowote wa kisheria. Kwa sababu tume hii inashughulikia zaidi haki za kisheria na kiutumishi za walimu ifike wakati watumishi hawa wa tume wawe wanasheria na maofisa wenye weredi wa maliasili watu.

Waachane na hawa walimu wasio na uelewa wowote wa kisheria. Kanuni zao zinaweza kuwaingiza kwenye mgogoro wa kisheria pindi watumishi wanaotendewa uonevu huu wakiamua kukatwa rufaa.
 
Tsc ni chombo Cha walimu, Sasa wanasheria wataingiaje hapo.
Mkuu unachanganya na CWT. Hiyo ni tume. Mtendaji Mkuu wa Tume ya Utumishi ya Mahakama ni Prof. Elisante Ole Gabriel ni mchumi siyo Jaji wala wakili. Tuwasaidie walimu wetu. Hawajui chochote kuhusu sheria wala masuala ya kiutumishi. Ndiyo maana kwao huko ni shida. Hata CWT yao ni shida kuliko vyama vingine vya wafanyakazi.
 
Katika utumishi wa umma kupandishwa cheo mtumishi ni hisani ya Mwajiri ambaye ni Serikali kupitia taasisi zake mbalimbali.Siyo haki ya mtumishi wa umma, ndiyo maana kwenye mikataba ya ajira hakuna suala ka kupandisha vyeo mtumishi.Ni pale mwajiri anapofurahishwa na kazi za mtumishi ndipo anaweza kumfikiria kumpandisha cheo au kumpatia tunzo nyingine.
Kwa hiyo ni sahihi mwalimu anapokuwa kwenye shauri la kinidhamu kusubirishwa kupandishwa cheo kwa sababu wakati huo anakuwa yuko kwenye kipindi cha mpito cha kati ya kuabidhibiwa au kuachiwa huru.
 
Usiropoke tena utakuja kuumbuka, public standing order inatoa haki ya mtumishi kupanda daraja kila miaka mitatu ukitoa mwaka mmoja wa matazamio
 
Back
Top Bottom