Nimeamini kuwa, Uongozi si kitu cha mchezomchezo, Mimi nakubaliana kabisa na wakuu wa nchi wawe wanapokea mkwanja wa juu zaidi, Maana huwenda wanamaisha magumu mioyoni mwao kuliko hata mlala Hoi
Mwaka Jana, Ni dhahiri Shairi kuwa, tuliishinda Korona, na tuliishinda Kwa maombi pekee, na mtu siwezi kumweliewa ati aseme tulikuwa tukinawa Sana, kuvaa barakoa Sana na kutokutengeneza umati wa watu, stamwelewa Kwa sababu, hata nchi nyingine zilifanya huo mtindo lkn Korona haikuwaacha Hadi wimbi la maambukizi ya pili yamekutana na wimbi la maambukizi ya awali
Kipindi hicho, kila mtu alimuunga mkono Raisi na kumpongeza Kwa maono na namna ajabu Korona iliyopotea, nakumbuka kina mh Lissu, alitaka kung'ang'ania agenda ya Corona eti IPO nchini, nakumbuka chama chake chenyewe kilimuonya kuwa hiyo agenda itampotezea wapiga Kura Kwa kuwa Korona haikuwepo
Sasa leo, kila mtu tena anamgeuka Raisi, kila mtu anamnyooshea kidole, kila mtu Anasema lake, kelele nyiiingi Kwa Serikali, unajiuliza, Tulipookoka na wimbi la maambukizi ya awali, mbona tulimwita shujaa, na tumshangilia Mungu?
Inavyotokea sasa, ndivyo ilivyokuwa hata kipindi cha awali, kila mtu alipiga kelele na kurusha kila Aina ya lawama Kwa Rai's
Kama tulipona mwaka Jana, Je, kunachochote tulimtunuku Raisi wetu Kwa kutuongoza vema ktk mapambano hayo licha kwamba nchi nyingine zilibaki Tete?
Rais wangu pole, na Mimi Naamini Kwa Imani yako hiyohiyo, itatuvusha tena, Na Mungu hajawahi kumwaibisha mja wake, najua katika hili kuna watu weengi na mataifa meengi wanaendelea kuucheka huu msimamo wako, na wamejiandaa kukucheka tena Kwa dharau, na huwenda kuna watu wanatamani waone vifo vikizidi kuongezeka Ili tu kukunanga wewe wakidhani wakikunanga wewe inatosha, hawajui pia kwamba watakuwa wakimnanga Yule unayemtegemea!!
Naungana nawe Raisi, kwamba Kwa Mungu pekee tutashinda, Tanzania imeandaliwa kuwa sehemu ya kuleta wokovu duniani
Kama tuliishinda mara ya Kwanza, tutashinda tena hili jaribu la pili,
Hata Ayubu alijaribiwa kwenye Mali zake, Kisha watu wake na Kisha yeye mwenyewe lakini aliahinda
Kila aliyeukimbilia msalaba alipata wokovu