Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Ikiwa ni siku chache baada ya kuripotiwa kutoweka kwa Kijana Deusdedith Soka ambaye ni Mwanachama wa Chadema mkazi wa Temeke Dar es Salaam pamoja na wenzake wawili, Wakili Paul Kisabo amefungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Hati ya dharura dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) na OCCID Temeke 'aliyewasiliana na Soka'.
Wengine ambao wameunganishwa kwenye kesi hiyo ni DZPC,ZCO,DPP na AG imesajiliwa leo August 23, 2024 kwa No 202408222000023998.
Ambapo kesi hiyo imepangwa kwa Mhe. Jaji Wilfred Dyansobera. Lakini bado haijapangwa tarehe rasmi ya kusikilizwa.
Soka na wenzake Jacob Mlay na Frank Mbise waliripotiwa kutoweka August 18, 2024 wakiwa wanaelekea kituo cha Polisi ikidaiwa kuwa walipigiwa simu kwenda kufuatilia suala la pikipiki ya Soka iliyodaiwa kuibiwa.
Baadhi ya wanafamilia ambao walizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari August 22, 2024 ambapo mzungumzaji Mkuu alikuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, walidai kuwa wameshafutalia kwenye vituo vya Polisi lakini hawajafanikiwa kuwaona wahusika hao, huku taarifa walizonazo ni kwamba wahusika walichukuliwa na Noah wakiwa njiani kuelekea kwenye kituo cha Polisi.
Soma KWELI - Dkt. Slaa asema amepata taarifa kuwa Deusdedith Soka atauawa na kutupwa msituni