Kutoweka vijana watano Dar es Salaam na Uzembe wa Media za Tanzania. Hakuna Muendelezo wala Hitimisho

Kutoweka vijana watano Dar es Salaam na Uzembe wa Media za Tanzania. Hakuna Muendelezo wala Hitimisho

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935
Wanabodi,

Nawasalimia popote mlipo.

Mod's: pia nawasalimia nikiwatakia kazi njema.

Twende kwenye Mada.

Ni takriban wiki moja imepita tangu habari ya kutoweka katika mazingira tata.Kwa vijana watano huko Dar es Salaam.
Tukio hilo liliripotiwa kutokea December 26/2021.

Habari hiyo ilishika kasi mitandaoni kote mpaka kwenye online TV ambao walienda mbele zaidi kwa kutuletea live coverage ya mahojiano na wazazi au walezi wa vijana waliodaiwa kutoweka.

Baadae serikali kupitia jeshi la Polisi nchini.ilitoa taarifa kupitia kamanda wa kanda maalumu ya kipolisi Dar es salaam, Jumanne Muliro Jumanne.

Na alisema wamekwisha pokea taarifa hizo na wanazifanyia kazi, pia alikanusha uvumi kwamba Jeshi hilo linawashikilia vijana hao.

My take:
Baada ya hapo, habari ile ambayo ilitikisa na kuleta mkanganyiko na taharuki ya wananchi kuhusiana na hali ya usalama wao

Kutosikika tena wala hakuna Media yoyote ambayo imetoa muendelezo wala hitimisho lake.

Kwa habari kama ile,ambayo ilikuwa ya kushitua lakini pia kwa upande mwingine ikilipaka matope serikali kupitia jeshi la Polisi.

Tulitarajia waandishi makini wangetumia weredi wao na kuhakikisha wanaifuatilia kutoka kwenye vyombo husika,ikiwa pamoja na familia husika pia.

Hii ingesaidia kuifanya jamii kuwa na taarifa sahihi na kuondoa wasiwasi kwa raia na hofu ya usalama wao nchini.

Lakini pia kwa vyombo vya habari nchini, kufanya hivyo ingekuwa vimetimiza wajibu wao muhimu wa kuihabarisha na kuielimisha jamii ya Watanzania.

Lakini pia kulibana jeshi la Polisi kuwa linatoa mrejesho wa matukio kadhaa yanayoripotiwa kila uchao na kuzimika kifo cha mshumaa.
Huku ikiacha taharuki kwa jamii.

Kinyume chake tunaona vyombo vya habari vikiendelea kuripoti matukio mengine na kwa mfumo huo huo wa zimamoto.

Juzi ilikuwa mrembo auwawa gesti,ikafuatiwa mauaji Mwanza, ikafuatiwa mauaji Dodoma na sasa ni Polisi waliomuua mfanyabiashara Mtwara.

Walau Jeshi la Polisi Mwanza wao wali Update shortly kuhusu yale mauaji ya kina dada watatu baada ya kuwanasa wahusika.

Lakini sio Media za nchi hii.sijui mnakwama wapi?

Kwa nini hamkamilishi content za habari zenu?

Acheni kufukuzana na bahasha kwenye warsha na makongamano kwa maslahi ya wanasiasa.

Bali itendendeeni haki taaluma yenu.

Ahsante.
Nawakilisha.
26/01/2022.
 
Inasikitisha sana aisee...machalii watano wote wanapoteaje kizembe tu na tunakaa kimya? Na kwanini ilipotiwe kwamba walitoa taarifa kwamba wamekamatwa na wazee wa kazi? Kuna kitu wamefanyiwa si bure
 
Inasikitisha sana aisee...machalii watano wote wanapoteaje kizembe tu na tunakaa kimya? Na kwanini ilipotiwe kwamba walitoa taarifa kwamba wamekamatwa na wazee wa kazi? Kuna kitu wamefanyiwa si bure
Ndio maana nasema kwamva vyombo makini vya habari visingeishia kutoa habari nusu.

Na badala yake wangehakikisha kwamba jamii inapata mrejesho mpaka mwisho.
Lakini kwa nchi yetu inakuwa sivyo.
 
Ankoli, hao vijana bado tu hawajapatikana?
 
Back
Top Bottom