Kutuliza mzimu wa migawanyiko napendekeza makao makuu ya CHADEMA taifa yahamishiwe Zanzibar

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
51,453
Reaction score
41,274
Hii italeta utulivu na usawa ndani ya chadema na kuondoa dhana ya chuki, dhihaka na ubaguzi dhidi ya viongozi wa kutoka Zanzibar na dhana ya kuitenga Zanzibar katika masuala mbalalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya mgawanyo wa rasilimali za chama hicho.

Zaidi sana,
makao makuu ya chadema kua Zanzibar itapunguza gharama za kukodi ofisi na itasaidia viongozi wengi wa chadema Taifa bara, kujifunza faida za ustahimilivu na subra, hekima na busara kwaa kiongozi katika uongozi, lakini pia itapelekea viongozi wa chadema wajifunze athari za uropokaji katika kuongoza watu na kususia mambo ya msingi.

Si hivyo tu,
makao makuu ya chadema kuhamishiwa Zanzibar kutatanua fursa za utalii wa ndani na kutaimarisha na kudumisha muungano na kuongeza uelewa na ufahamu wa wanachadema dhidi ya manufaa ya maridhiano yenye dhamira njema na heshima ndani yake.

Una maoni gani ndugu mdau wa JF katika hili?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Geroman hulali usingizi unaweweseka na Chadema. 🤣🤣🤣🤣
NRNE
sasa kama umelala usingizi mpaka saiz gentleman, manung'uniko ya ugumu wa maisha yatakuisha kweli gentleman?

fake pastaz bana, kumbe uvivu nao mko nayo? 🐒
 
sasa kama umelala usingizi mpaka saiz gentleman, manung'uniko ya ugumu wa maisha yatakuisha kweli gentleman?

fake pastaz bana, kumbe uvivu nao mko nayo? 🐒

Pigia mstari kuweweseka na CHADEMA .



Si uendelee energy yako kama inakuburudisha ndugu?
 
NO REFORMS, NO ELECTION!
 
Sifikir kama 100% italeta usawa ukiangalia kwa kina zaidi kuna mambo nayaona kwa chadema ambayo ni changa moto kwa upande wa zanzibar au mwenyekiti aliye pita alikosea
1. Chadema inaonekana ni chama cha wakristu
2.kilikua cha ukabila au kanda
3.Kilikua cha mtu na si cha wananchi
Hivyo ilikijiboreshe nakua imara nikua boa sehemu zilizo kua na makando kando nakua chama kisicho fungamana na dini, ukabila au ubinafsi katika uongozi na amini kitakua imara zaidi ya hapa
 
uko sahihi gentleman,
but dhana ya uongozi mpya wa chadema kudhihaki na kuonyesha ubaguzi na chuki za wazi wazi kabisa dhidi ya viongozi kitaifa mathalani rais Dr.Samia Suluhu Hassan, ukiachilia mbali kupuuzwa kwa viongozi wa chadema kwa upande wa zanzibar umekitia doa baya sana chama hicho, na nadhani kabla ya chadema kufikiria kubadili uongozi wa kitaifa ni vizuri ikahamishia kwanza shughuli zake zote za chama kitaifa zanzibar walau kutuliza na kupunguza joto ya dhana hizo za kibaguzi dhidi ya wazanzibari.

mpaka sasa chadema inaonekana ni virus wa muungano
 

Upo sahihi ila kuamisha rasimalii kwa maana ya vitu nakupeleka zanzibar sioni mantiki yake , ila kuna maboresho yana takiwa kufanyika kwanzia kwenye katiba , kiufupi kiwe chama cha watu nasio group ikiwa kitakua cha watu kama kinavyo tume kauri mbiu ya "people power"(nguvu ya uma) hakita tumia nguvu kuitoa ccm madarakina,
Nini kifanyike kwa upande wazanzibar?
Mtazamo wangu kwa uongozi ulipo na utakao kuja.
1.Kujenga vijana na watu wlio na mtazamo chanya na sio uyeye na umimi, udini, ukabira, ukanda au lugha, kua natamaa na vyeo fulani,
2.Mali ziwe za chama nasio mtu au watu,
3.Kutokua na watu wanapenda kufungamana sana na mifumo ya vyama pinzani ,
4.Kua tayari kusikiliza hoja za watu na kuzifanyia kazi
Mambo yafanywe kwa uwazi na ukweli, saiv watu wanapenda ukweli na hii imekuja kutokana teknolojia watu wanapata habari , namiin wakipanda ukweli kwenye mioyo yawatu basi uwezo wa kuchukua dora upo, maan watu wanaumia kwa uongo
 
Haya wahi kasaini malipo yako
 
Hatutaki watovu wa adabu na walevi nchini kwetu wabakie huko huko Tanganyika watekane wao Kwa wao huku wakiisingizia serikali
 
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…