Kutumbuliwa Balozi Katanga na Diwani Athumani kuna uhusiano wowote na mkataba wa Bandari

Shakari

Senior Member
Joined
Jul 6, 2022
Posts
188
Reaction score
570
Nimekuta mahali mjadala mkubwa kuhusiana na kuondolewa kwenye nafasi zao Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Katanga na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Kamishna Diwani Athumani ikidaiwa kuwa kuna uhusiano na misimamo waliyokuwa wameweka kuhusu mkataba wa Bandari.

Baadhi ya Viongozi na watendaji wa Nafasi za juu serikalini kuondolewa kwenye Nafasi zao bila Maelezo yoyote akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Eric Hamis aliondolewa tarehe 4/7/2022, Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Kamishna Diwani Athumani ambao waliondolewa kwa pamoja tarehe 3/1/2023. Viongozi wote hawa waliondolewa ndani ya kipindi cha
mchakato wa MoU na Kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge.

Kuchukua kipindi kirefu cha miezi 8 kuingia Mkataba tangu kusainiwa MoU na katika kipindi hicho Serikali haikufanya tathmini wala feasibility study kujua mahitaji na manufaa ya mradi.









Kamishna Diwani Athumani





Erick Hamis
 
Kuna mambo yanapita hakuna maelezo ya kutosha.
But what goes around comes around.
 
huyo katanga ni mtu mmoja smart mno alinyoosha sana mahakama
 
Visiki na miiba huondolewa kabla ya shamba kulimwa
 
Mmehamia huku tena baada ya kuonq cd ya baraza la mawaziri kugawanyika imedoda??

Kweli ujinga kipaji🤣🤣🤣
 
Inaleta sense. Nina hakika, ndani ya TISS kuna watu bado wana royalty kwa Diwani. Na hawa ndio waliovujisha mkataba kwa umma.

Na baadaya huu, vumbi likitulia, watavujisha ile mingine 30 iliyosainiwa kwa siri.
 
Ndugai,
Diwani.
Katanga,
Erick Hamis.
Wote hawa hawakutaka bandari za Tanganyika ziuzwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…