Kutumbuliwa kwa Mwigulu Nchemba, Rais hana lawama. Dharau kwa wawakilishi wa wananchi ni dharau kwa wananchi

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Mwigulu Nchemba anatambua kwamba amekosea, lakini anatambua kwamba Rais anamwamini Sana.

Upande wa pili hana taarifa kwamba hata kama Rais angemwamini na kumpenda Sana, kama wawakilishi wa wananchi (wabunge) wanadharaulika basi mpendwa wa Rais amewadharau wananchi.

Kuwadharau wananchi means ni kumgombanisha Rais na wapiga kura Jambo ambalo kisiasa halina tija.

Kauli ya Mwigulu imeibua hasira sana kwa wananchi, angalia majibu wanayotoa kwenye mahojiano na vyombo vya habari utabaini ipo hasira ndani yao.

Hasira hii inaletwa zaidi na njaa, gharama za maisha kuwa juu hata kama ungekuwa na PhD ngapi; kama PhD haziwezi kuwapa chakula wananchi lazima hasira zitawaka juu yao tu.

Mwigulu anachofanya ndani ya Bunge ni kukebei wenye njaa huku akijua wao ndio waliompa kura na wanamfanya aishi kwenye luxury life.

Yeye kwake anunui chakula ananunuliwa na serikali; wananchi wanajitafutia, wanahitaji faraja siyo kebehi.

Kwa ugumu wa maisha uliopo sasa siyo kipindi cha kukimbizana na machinga kuwaondoa mjini, tusubiri kipindi cha shibe tukafanye hayo. Sasa hivi ni kipindi chakuchemsha mawe ukiwadanganya watoto chakula kinaiva.

Mvua hazipo mbali, wakulima watapanda na kuvuna tuombe uzima. Lakini wakati tunaomba uzima tuwape faraja wananchi, tuwachemshie mawe watulie wakisubiri yaive, that's how leadership works.

Tukiendelea na ngonjera za ubobezi wa uchumi Kwa wananchi wenye njaa tutaishia kuwakamata na kuwaweka ndani Kwa kutumia migambo na polisi but truth ni kwamba hali ni mbaya kwenye kaya masikini.

Rais hiki alichofanya Mwigulu katika umaskini huu uliopo sasa kinapswa kulipwa kwa utumbuzi; siyo kwa sababu hakusaidii Ila kwa sababu tu unataka kutuchemshia mawe tutulie tusubiri yaive.

Mwisho nikuombe kwa kutumia mbinu unazozijua waelekeze wateule wako wapunguze kuangaika na wananchi kwa sasa; wasipambane na machinga wala mama ntilie, wavute subira Mwenyenzi Mungu atupe chakula.

Wakiachwa hata kama miji itachafuka jwa kiasi fulani kwa kipindi fulani itasafishwa, tutumie uchemshaji mawe kutuliza wenye njaa.

Tunaweza tukadhani masikini wanahitaji chakula cha msaada kumbe wanahitaji faraja ya Serikali na mfariji mkuu ni wewe.

Nikutakie kazi njema na Mwenyenzi Mungu akusaidie maarifa yakuvuka kipindi hiki chakuchukiwa Kwa majanga yanayoipata Dunia.
 
Kichwa cha habari kiliniaminisha keshatumbuliwa tayari kumbe ni wazo tu.

Nahisi kila awamu inakuwa na viongozi kadhaa wa ovyo wanaokumbatiwa na utawala. Kwa awamu hii Mwigulu ni mmoja wao.
 
Mi nikajua ametunguliwa kumbe ni maelezo tu ambayo hata darasa la kwanza anaweza andika[emoji2957][emoji2957]
Nami nilijua hivyo nikajiandaa kufurahi. Ndio maana tunaambiwa tusome habari kamili maana mtu anaandika kichwa cha habari cha kuvutia wasomaji
 
Kwa ugumu wa maisha uliopo sasa siyo kipindi cha kukimbizana na machinga kuwaondoa mjini, tusubiri kipindi cha shibe tukafanye hayo. Sasa hivi ni kipindi chakuchemsha mawe ukiwadanganya watoto chakula kinaiva.
Hivi wamachinga wanaondolewa ni Dar na Mwanza peke yake au ni operesheni nchi nzima?
 
Mganga wa Mwigulu yule mwenye ziwa moja ni kiboko amemhakikishia kuwa mama hapindui kwake iwe jua iwe mvua ndiyo siri ya kiburi chake
 
Nilifurahi kusoma tu kichwa cha habari KUTUMBULIWA KWA MWIGURU NCHEMBA RAIS HANA LAWAMA. Nimeshangilia kwa sauti. Kumbe maelezo yaliyomo humo ni tofauti na kichwa cha habari. Kama hujui kuandika habari uliza Kwanza. Mnatuchanganya tu. Baki nayo hiyo habari yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…