Kutumia bil. 600 kwenye sensa ni ufisadi

Unitman

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
511
Reaction score
671
Habari ndugu wadau.

Mimi nimehesabiwa jana.Lakini nilichokiona kwa karani na taarifa tulizompatia haikuchukua ata dakika 5 na tulikuwa kaya ya watu 9.

Sasa nikajiuliza hii ndo kazi watu wamefanya semina wiki 3 kweli??Hakika sijaamini nilichokiona.

Hii inamaana tungekuwa makini tungetumia ata billion 80 kuhesabu watu na zoezi likafanikiwa 100%.

Kwa mfumo wa sensa nilivoona mafunzo ingekuwa siku 2 au 3 au maximum 5 lakini hivi ninavyoandika mtaani kwetu hakuna maji kabisa.

Fikiria mtaa mzima hakuna sehemu maji yanatoka ata ya visima ni kuyatafuta kwa tochi.

Sasa wadau tutaendelea kulalamika mpaka lini??
 
Ilikuwa hamna haja hata ya semina mkuu.
Watu wakisha kuwa wezi hutafuta njia za wizi. Ilikuwa rahisi sana. Wange tumika wenyeviti wa mtaa wapitie nyumba zao, wapeleke taarifa Kata, halafu Kati izipeleke wilayani hadi zifike Taifa hatunge tumia hata bilion moja.
Tuliambiwa watatumika vijana wa maeneo husika kuhesabu, leo tunaona wanao hesabu sio vijana wa mtaa husika bali ni wageni wa maeneo husika, na wana zunguka na balozi. Ccm ni ile ile wizi tuu.
 
Akili zile zile za kuazima zinamsumbua huyu mtanzania. Vile vishkwambi vilivyotumiwa na kila afisa wa sensa unajua bei zake?.

Posho wanazolipwa makarani wa sensa kwa siku unazijua ni shilingi ngapi?. Wao jumla yao unajua ni wangapi?.

Achana na hizi akili mgando za malalamiko kuanzia january mpaka desemba.
 
Unahesabu karani na nyumba zenu tisa tu?

Vipi kuhusu, kuandaa dodoso, kuandaa vitabu vya kufundishia, kabrasha, kulisha na kulipia kumbi, kuwalipa wawezeshaji, ni mengi

Hapo hapo wapo waongeza 0
Ni pesa ndogo Sana hata daraja la mita 50 haiwezi jenga.
 
Tanzania bado tuna safari ndefu. Suala la sensa lingeweza kufanywa na viongozi wa sehemu husika kwa gharama ya chini sana kuliko hii kubwa ya zaidi ya bilioni 600.
 
... na kwa kila nyumba/kaya, Mwenyekiti angelipwa posho fulani hivi, say, TZS 5,000 as simple as that! Sema changamoto kubwa ingekuwa CCM kuingilia zoezi na kulivuruga kwa kutaka kuweka watu wao - ni tatizo kweli kweli.
 
Ukweli mchungu hio hela 50% itakuwa imeishi kwa majiziz
 
Hakuna kalani wa kukamilisha kuhoji kaya ya watu 9 ndani ya dk 5.Minimumu ni 30 minutes vinginevyo kalani kalipua kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…