SoC02 Kutumia elimu kupunguza tatizo la ajira

SoC02 Kutumia elimu kupunguza tatizo la ajira

Stories of Change - 2022 Competition

piry Lasway

Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
6
Reaction score
2
Elimu kama kama zilivyo sekta muhimu kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla,ni muhimu sana.Jamii nyingi na mataifa mengine yameitumia vizuri na wamefanikiwa sana.

Ili elimu yetu iweze kutumika kupunguza tatizo la ajira inapaswa kufanya yafuatayo;

(1)Kabla ya kutoa elimu kwa mtoto inapaswa kwanza, kufahamu mtoto huyo anacho kipaji gani,ukishajua kipaji cha mtoto itakua rahisi kupewa elimu ya kile alicho nacho yaani kipaji chake,

(2)Baada ya kujua mtoto anachokipaji gani,baada ya kupata mafunzo ya awali yaaani kusoma, kuandika na kuhesabu,mara moja ataanza kupata mafunzo yanayoendana na kipaji chake,badala ya mtoto kusomeshwa masomo mengi na mwisho wa siku kutokufanya kile alichonacho kwa ndani yaani kipaji chake,imepelekea jamii kua na wasomi wengi lakini wameshindwa kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii.

(3)Mbali na kufundishwa sasa masomo yanayomfaa, yanayofanana na kipaji chake, atafundishwa sasa na masomo ya ziada ili kua na ujuzi mbalimbali kwa ajili ya kumwongezea maarifa.

(4) Sambamba na kufunzwa masomo yanayoendana na kipaji chake,kuwe na mafunzo ya kivitendo, mtoto ajengewe hali ya kufanya kwa vitendo, kuwe na mashindano ya kila watoto wenye ujuzi unaofana, yani wenye vipawa sana na mashindano yawe ya kidarasa, kishule, kiwilaya, kimkoa, kikanda na kitaifa.

Ama kwa hakika,elimu watakayoipata itapunguza tatizo la ajira kwa sababu, mtoto amepata ujuzi sahihi, kulingana na kipaji chake, akimaliza hatasubiria tu ajira, badala yake ataenda kufanya kazi maana anao wigo mpana wa ujuzi na kipaji alichonacho na hatokua na woga, hofu na kua na hali ya kukata tamaa, maana tokea akiwa mdogo amejifunza kwa nadharia na vitendo hivyo atakua na usubiri wa kufanya.

Wakati Misri/Kemet ya kale ikiwa katika kilele cha maarifa na maendeleo, watu wa zama hizo walipendezwa na kuona fahari kwenda kusoma huko, mfano wa wageni hao ni kutoka Ugiriki kama kina Plato na wengine wengi, elimu na maarifa waliyoyapata huko Misri/Kemet walienda kubadilisha na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii yao, leo wengi wanawaona kama jamii iliyostaarabika zaidi na chanzo cha ustaarabu, waliweza kutumia ujuzi na elimu sahihi kutatua changamoto mbalimbali katika jamii yao.

Sisi pia twaweza kubadili elimu yetu na kuzalisha wahitimu watakaoweza kutatua changamoto mbalimbali katika jamii yetu na kupunguza tatizo la ajira kwa kufanya kazi sawasawa na kipaji chake.

Asante,

Priscus Lasway,
Simu namba ni 0752250938/0624873870.
Email ni
piryjacob@gmail.com
 
Upvote 0
Back
Top Bottom