SoC04 Kutumia mfumo wa kielektroniki ili kuboresha huduma za NHIF

Tanzania Tuitakayo competition threads

Novart moses

Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
17
Reaction score
49
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni mpango wa bima ya afya ya umma nchini Tanzania. Mfuko huu ulianzishwa mwaka 2002 kwa Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Sura ya 395 ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za mwaka 2002.

Huduma zitolewazo kwa wanachama wa NHIF ni kama zifuatazo:
Huduma za wagonjwa wa nje, Huduma za wagonjwa wa ndani, Dawa, Vipimo vya maabara, Matibabu ya meno, Huduma za macho n.k

Hospitali mbalimbali nchini, kuanzia ngazi ya hospitali za taifa mpaka zahanati, zimefanikiwa kutoa huduma kushirikiana na NHIF na hospitali nyingine nyingi zikiendelea kuongezeka, lakini utolewaji wa huduma umekuwa duni kwa kiasi fulani, jambo ambalo linaleta changamoto nyingi hasa kwa wagonjwa wanaoenda kupata huduma mbalimbali hospitalini.

Kero hizo ni kama zifuatazo:
1. Muda mrefu wa kusubiri kuhakiki taarifa za kadi ya mwanachama na kuidhinisha matibabu:

Utaratibu uliopo ni kwamba ukifika hospitali, unakabidhi kadi kwa watumishi ambao watahakiki taarifa zako na kadi ili kuona kama ni kweli kadi yako imelipiwa na taarifa zake ni za kweli. Jambo hili husababisha foleni kubwa hasa katika hospitali kubwa ambazo watumiaji wa bima huenda kupata huduma hapo, jambo ambalo husababisha upotevu wa muda kwa wagonjwa kwa sababu njia ya kuhakiki ni duni na haina spidi.

2. Utunzaji duni wa taarifa za mgonjwa kwa wagonjwa na wahudumu wa afya:
Taarifa za matibabu anazobaki nazo mgonjwa, yaani ugonjwa alionao, vipimo alivyofanya, na dawa alizopewa ni kwa njia ya karatasi ambayo hupewa mara baada ya kukamilisha matibabu. Jambo hili linasababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza karatasi hizi ambazo zina taarifa muhimu zinazohusu afya zao na zinaweza kutumika katika matibabu ya awamu ijayo hospitalini hapo au hospitali nyingine ili kujua kama shida hii mgonjwa aliwahi kupata na alihudumiwa kwa kiasi gani na je, huduma alizopata zilimsaidia au kutomsaidia kwa kiasi gani.
Jambo hili linaweza kupelekea watu kugundulika na magonjwa hasa makubwa kama figo, ini, na moyo kufeli katika hatua mbaya (late/end stage) ambayo matibabu yake hayana asilimia kubwa ya kumaliza tatizo. Pia wengi wao hutupa karatasi hizi na kuongeza taka hospitalini au maeneo mengine. Utunzaji huu pia unasababisha usalama mdogo wa taarifa za mgonjwa kwa sababu taarifa za mgonjwa hutunzwa katika karatasi ambayo mtu yeyote anaweza kuisoma na kujua taarifa za mgonjwa husika, ikiwepo jina lake, hospitali aliyoenda, ugonjwa anaoumwa, vipimo alivyofanya, pamoja na dawa alizopewa.

Pia, wahudumu wa afya hubaki na taarifa za mgonjwa kwa njia ya karatasi ambazo hutumiwa na NHIF kulipia matibabu ambayo mgonjwa alipata hospitalini kulingana na taarifa zilizopo kwenye karatasi husika. Jambo hili linaweza kuleta hasara kwa hospitali pale ambapo karatasi hupotea na gharama zile kutolipiwa na NHIF na kubaki juu ya hospitali husika.

3. Matumizi duni ya rasilimali watu na rasilimali kazi: Mfumo wa sasa wa utoaji huduma kwa kutumia bima unahitaji uwepo wa vifaa kama kompyuta, karatasi za kuandikia taarifa za mgonjwa, na watu (wahudumu wa afya) ambao watasaidia kuhakiki taarifa za mgonjwa na kumuweka kwenye mfumo wa hospitali husika wa matibabu. Jambo hili linapoteza wafanyakazi ambao wangesaidia katika huduma nyingine pamoja na vifaa ambavyo pia vingesaidia katika utoaji wa huduma zinginezo na kuongeza ufanisi katika hospitali.

Suluhisho!

1. Kuanzisha mfumo (mashine) wa NHIF

Mfumo huu utakua mithili ya mashine za benki (ATM) utakaochakata taarifa za wagonjwa kutoka kwenye kadi zao za uanachama zenye chip na mfumo huu utahakiki kadi na mtumiaji wa kadi kama ni yeye ili kuzuia wizi wa kadi na kuazimana bima kwa kutumia kamera ndogo iliyopo kwenye mashine hiyo. Mashine itatoa risiti kwa mgonjwa ili kumuwezesha aendelee na matibabu na taarifa itaenda kwa daktari kwenye kompyuta yake iliyoungwa na mfumo huu na kumruhusu aendelee na matibabu ndani ya muda mfupi na haraka.
Pia, mifumo ikiunganishwa na kompyuta, daktari ataweza kuona matibabu yaliyopita ya mgonjwa na kufanya tathmini juu ya hali ya sasa na iliyopita ili kupata matibabu sahihi na kuzuia ugonjwa kukua kwenye hatua mbaya, mfano kansa. Pia mfumo utaungwa na vitengo vingine hospitali kama maabara na famasi ili daktari aweze kutuma vipimo maabara na dawa famasi kwa kutumia mfumo na sio karatasi kama ilivyo awali.

Aidha, kuwe na miundombinu ya kiteknolojia ya kukusanya maoni ya wagonjwa baada ya kupatiwa huduma na maoni hayo yatafanyiwa tathmini baadae ili kuboresha huduma zaidi. Pia, mifumo iwekewe uwezo wa kuandaa ripoti ndani ya wiki hadi mwezi mfano, idadi ya wagonjwa waliohudumiwa ndani ya muda huo, dawa zilizotumika ikiwepo zilizotumiwa sana, vipimo vilivyofanywa, idadi na matokeo, pamoja na magonjwa yaliyoshamiri kwa muda huo ili kusaidia kufanya utafiti wa chanzo cha magonjwa yaliyoripotiwa sana ngazi ya hospitali husika, wilaya, mkoa na taifa zima, ili kuboresha afya za watu mfano, kutoa elimu kujikinga, namna ya kutumia dawa kwa usahihi ili kutibu n.k

Hospitali ndogo zenye huduma ya NHIF zipewe mashine ndogo mithili ya mashine ndogo ya ATM ya wakala zitakazotumia betri zinazoweza kuchajiwa au kubadilishiwa ili kuwezesha huduma sehemu zenye changamoto ya umeme.

ATMs-thegem-blog-timeline-large.jpg

Google Image Result for https://www.paycorp.co.za/wp-content/uploads/2015/09/ATMs-300x225.jpg
Screenshot_20240616_130520_Google.jpg

Mfano wa mfumo Source: Google

2. Kutunza taarifa za mgonjwa kwenye kadi ya NHIF yenye chip
Taarifa zote za mgonjwa zitaendelea kuwekwa kwenye kadi yake kila akitibiwa, kukusanya taarifa za mgonjwa, ikiwepo shida alokujanayo mgonjwa, vipimo, dawa, n.k., na taarifa hizi zitabaki kwenye kadi ya mwanachama yenye chip na nywila mfano alama za vidole na nenosiri ili kulinda usalama wa taarifa za mgonjwa. Taarifa hizi pia zitabaki kwenye mfumo wa hospitali ili kuwezesha NHIF kufuatilia dawa na huduma zilizotolewa na kuilipa hospitali husika badala ya kubaki kwenye karatasi kama awali.
evm-chip-credit-card-y2payments-2000x1200.jpg

Mfano wa kadi yenye chip Source: Google

3. Kuboresha applikesheni ya NHIF
Kwa kuifanya iweze kuwa na taarifa zote za matibabu ya mgonjwa aliyofanya. Pia, iwekewe uwezo wa kumkumbusha mgonjwa kama ana dawa za kunywa au kurudi kwa daktari kama alipangiwa, pia iwe na dondoo za afya kulingana na hali ya mgonjwa, mfano magonjwa ya kudumu kama, kisukari, presha, na dondoo nyinginezo.
Applikesheni iwe na nywila sawa na kadi ya mwanachama kwa ajili ya usiri wa taarifa za mgonjwa.

Hivyo mfuko wa bima (NHIF) kushirikiana na hospitali, na wizara ya afya zinaweza kuboresha zaidi huduma.
 
Upvote 190
Mfumo wa kutuma taarifa kutoka kwa daktari kwenda Maabara, Famasi upo na unatumika kwa sasa. Taarifa za kumbukumbu ya matibabu pia hubaki kwenye mfumo wa Hospital pindi ukipata matibabu ndio maana huwa kuna kadi ndogo unaandikiwa namba ya usajili na kwenye hiyo kadi pameandikwa pindi unaporudi hospital, rudi na hiyo kadi.

Kuhusu taarifa za huduma kuandikwa kwenye karatasi ambapo zitatumwa kwenda BIMA kwa ajili ya malipo wakati tayari hizo taarifa zishatumwa kupitia mfumo wa NHIF, hapo inabidi uendelee kwani bado hali ya udanganyifu ipo endapo utatumika pekee pasipo na fomu za karatasi.

Suala la uhakiki wa Kadi naliunga mkono pawe na mfumo ulioupendekeza, yaani kadi iwe na Chip ambapo ikiwa imelipiwa ndio inakuwa na status ya ACTIVE, kama haijalipiwa au kuisha muda wa matumizi inabaki kuwa INACTIVE. Ili uweze kuitumia kwenye mashine ya kuhakiki ndio inabidi utumie Fingerprint/Nywila kama ilivyo ATM. Nywila ikikubali(hapa napendekeza pawe kwa fingerprint maana nywila inaweza kujulikana kwa third part) ndipo kadi iingie/uweze kuaccess mashine ili isome kama Kadi ni ACTIVE/INACTIVE, baada ya hapo ndio upate risiti ya kwenda kupata matibabu.
 
Ahsante sana mheshimiwa lakini baadhi ya sehemu mfumo hutumiwa na watu wa cash tu na sio wa nhif
Ndio maana nimependekeza uungwe na wa hospitali ili kama wanatenga uwepo wa nhif peke ake na wa cash na kwa hospitali ambazo wote cash na bima wanawekwa kwenye mfumo wauboreshe uwe unatenga nhif na cash ili nhif wajue watu wao ni wapi
Na hivi karibuni wizara ya afya imeanzisha mfumo ambao serikali zote zitatumia hivyo wakishirikiana wanaweza kuboresha zaidi
Ahsante kwa maoni yako pia
 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni mpango wa bima ya afya ya umma nchini Tanzania. Mfuko huu ulianzishwa mwaka 2002 kwa Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Sura ya 395 ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za mwaka 2002.

Huduma zitolewazo kwa wanachama wa NHIF ni kama zifuatazo:
Huduma za wagonjwa wa nje, Huduma za wagonjwa wa ndani, Dawa, Vipimo vya maabara, Matibabu ya meno, Huduma za macho n.k

Hospitali mbalimbali nchini, kuanzia ngazi ya hospitali za taifa mpaka zahanati, zimefanikiwa kutoa huduma kushirikiana na NHIF na hospitali nyingine nyingi zikiendelea kuongezeka, lakini utolewaji wa huduma umekuwa duni kwa kiasi fulani, jambo ambalo linaleta changamoto nyingi hasa kwa wagonjwa wanaoenda kupata huduma mbalimbali hospitalini.

Kero hizo ni kama zifuatazo:
1. Muda mrefu wa kusubiri kuhakiki taarifa za kadi ya mwanachama na kuidhinisha matibabu:

Utaratibu uliopo ni kwamba ukifika hospitali, unakabidhi kadi kwa watumishi ambao watahakiki taarifa zako na kadi ili kuona kama ni kweli kadi yako imelipiwa na taarifa zake ni za kweli. Jambo hili husababisha foleni kubwa hasa katika hospitali kubwa ambazo watumiaji wa bima huenda kupata huduma hapo, jambo ambalo husababisha upotevu wa muda kwa wagonjwa kwa sababu njia ya kuhakiki ni duni na haina spidi.

2. Utunzaji duni wa taarifa za mgonjwa kwa wagonjwa na wahudumu wa afya:
Taarifa za matibabu anazobaki nazo mgonjwa, yaani ugonjwa alionao, vipimo alivyofanya, na dawa alizopewa ni kwa njia ya karatasi ambayo hupewa mara baada ya kukamilisha matibabu. Jambo hili linasababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza karatasi hizi ambazo zina taarifa muhimu zinazohusu afya zao na zinaweza kutumika katika matibabu ya awamu ijayo hospitalini hapo au hospitali nyingine ili kujua kama shida hii mgonjwa aliwahi kupata na alihudumiwa kwa kiasi gani na je, huduma alizopata zilimsaidia au kutomsaidia kwa kiasi gani.
Jambo hili linaweza kupelekea watu kugundulika na magonjwa hasa makubwa kama figo, ini, na moyo kufeli katika hatua mbaya (late/end stage) ambayo matibabu yake hayana asilimia kubwa ya kumaliza tatizo. Pia wengi wao hutupa karatasi hizi na kuongeza taka hospitalini au maeneo mengine. Utunzaji huu pia unasababisha usalama mdogo wa taarifa za mgonjwa kwa sababu taarifa za mgonjwa hutunzwa katika karatasi ambayo mtu yeyote anaweza kuisoma na kujua taarifa za mgonjwa husika, ikiwepo jina lake, hospitali aliyoenda, ugonjwa anaoumwa, vipimo alivyofanya, pamoja na dawa alizopewa.

Pia, wahudumu wa afya hubaki na taarifa za mgonjwa kwa njia ya karatasi ambazo hutumiwa na NHIF kulipia matibabu ambayo mgonjwa alipata hospitalini kulingana na taarifa zilizopo kwenye karatasi husika. Jambo hili linaweza kuleta hasara kwa hospitali pale ambapo karatasi hupotea na gharama zile kutolipiwa na NHIF na kubaki juu ya hospitali husika.

3. Matumizi duni ya rasilimali watu na rasilimali kazi: Mfumo wa sasa wa utoaji huduma kwa kutumia bima unahitaji uwepo wa vifaa kama kompyuta, karatasi za kuandikia taarifa za mgonjwa, na watu (wahudumu wa afya) ambao watasaidia kuhakiki taarifa za mgonjwa na kumuweka kwenye mfumo wa hospitali husika wa matibabu. Jambo hili linapoteza wafanyakazi ambao wangesaidia katika huduma nyingine pamoja na vifaa ambavyo pia vingesaidia katika utoaji wa huduma zinginezo na kuongeza ufanisi katika hospitali.

Suluhisho!

1. Kuanzisha mfumo (mashine) wa NHIF

Mfumo huu utakua mithili ya mashine za benki (ATM) utakaochakata taarifa za wagonjwa kutoka kwenye kadi zao za uanachama zenye chip na mfumo huu utahakiki kadi na mtumiaji wa kadi kama ni yeye ili kuzuia wizi wa kadi na kuazimana bima kwa kutumia kamera ndogo iliyopo kwenye mashine hiyo. Mashine itatoa risiti kwa mgonjwa ili kumuwezesha aendelee na matibabu na taarifa itaenda kwa daktari kwenye kompyuta yake iliyoungwa na mfumo huu na kumruhusu aendelee na matibabu ndani ya muda mfupi na haraka.
Pia, mifumo ikiunganishwa na kompyuta, daktari ataweza kuona matibabu yaliyopita ya mgonjwa na kufanya tathmini juu ya hali ya sasa na iliyopita ili kupata matibabu sahihi na kuzuia ugonjwa kukua kwenye hatua mbaya, mfano kansa. Pia mfumo utaungwa na vitengo vingine hospitali kama maabara na famasi ili daktari aweze kutuma vipimo maabara na dawa famasi kwa kutumia mfumo na sio karatasi kama ilivyo awali.

Aidha, kuwe na miundombinu ya kiteknolojia ya kukusanya maoni ya wagonjwa baada ya kupatiwa huduma na maoni hayo yatafanyiwa tathmini baadae ili kuboresha huduma zaidi. Pia, mifumo iwekewe uwezo wa kuandaa ripoti ndani ya wiki hadi mwezi mfano, idadi ya wagonjwa waliohudumiwa ndani ya muda huo, dawa zilizotumika ikiwepo zilizotumiwa sana, vipimo vilivyofanywa, idadi na matokeo, pamoja na magonjwa yaliyoshamiri kwa muda huo ili kusaidia kufanya utafiti wa chanzo cha magonjwa yaliyoripotiwa sana ngazi ya hospitali husika, wilaya, mkoa na taifa zima, ili kuboresha afya za watu mfano, kutoa elimu kujikinga, namna ya kutumia dawa kwa usahihi ili kutibu n.k

Hospitali ndogo zenye huduma ya NHIF zipewe mashine ndogo mithili ya mashine ndogo ya ATM ya wakala zitakazotumia betri zinazoweza kuchajiwa au kubadilishiwa ili kuwezesha huduma sehemu zenye changamoto ya umeme.

View attachment 3018724
Google Image Result for https://www.paycorp.co.za/wp-content/uploads/2015/09/ATMs-300x225.jpg
View attachment 3018729
Mfano wa mfumo Source: Google

2. Kutunza taarifa za mgonjwa kwenye kadi ya NHIF yenye chip
Taarifa zote za mgonjwa zitaendelea kuwekwa kwenye kadi yake kila akitibiwa, kukusanya taarifa za mgonjwa, ikiwepo shida alokujanayo mgonjwa, vipimo, dawa, n.k., na taarifa hizi zitabaki kwenye kadi ya mwanachama yenye chip na nywila mfano alama za vidole na nenosiri ili kulinda usalama wa taarifa za mgonjwa. Taarifa hizi pia zitabaki kwenye mfumo wa hospitali ili kuwezesha NHIF kufuatilia dawa na huduma zilizotolewa na kuilipa hospitali husika badala ya kubaki kwenye karatasi kama awali.
View attachment 3018756

Mfano wa kadi yenye chip Source: Google

3. Kuboresha applikesheni ya NHIF
Kwa kuifanya iweze kuwa na taarifa zote za matibabu ya mgonjwa aliyofanya. Pia, iwekewe uwezo wa kumkumbusha mgonjwa kama ana dawa za kunywa au kurudi kwa daktari kama alipangiwa, pia iwe na dondoo za afya kulingana na hali ya mgonjwa, mfano magonjwa ya kudumu kama, kisukari, presha, na dondoo nyinginezo.
Applikesheni iwe na nywila sawa na kadi ya mwanachama kwa ajili ya usiri wa taarifa za mgonjwa.

Hivyo mfuko wa bima (NHIF) kushirikiana na hospitali, na wizara ya afya zinaweza kuboresha
 
Great idea
 
Kwanza hongera kwa chapisho zuri linalolenga kuboresha mifumo ya afya,.... Lakini kwa upande wangu nngependa kushauri kwa kipengere cha utunzaji wa taarifa ni kwamba ili kupunguza udanganyifu ni heri mfumo wa karatas ungeendelea ambapo taarifa za mgonjwa huandikwa papo kwa papo anavofanyiwa matibabu, lakini ingependeza zaidi Kama kungekuwa na karatas au hata kijitabu ambacho atapewa mgonjwa ukiachana na zile karatas laini ambazo ni rahisi kuwa destroyed,...... Wangejitahid kutoa at least sehemu ambayo itakuwa ni imara zaidi na ambayo itakuwa rahisi kutunzika mfano ni hvyo vijitabu instead of zile karatas Kama nilivosema hapo awali
All the best,...... Naomba kuwasilisha.
 
Nimeweka pale kwamba mashine itoe risiti kabla ya matibabu...baada ya matibabu pia mfumo utatoa risiti iliyo na taarifa za matibabu pia karatasi hio inaweza boreshwa na kua ngumu kuliko hizi za awali
Ahsante kwa mawazo yako mazuri🔥🔥🔥
 
Back
Top Bottom