Elections 2010 Kutumia nguvu (violence) kwenye siasa kunaruhusiwa

Mimi hata vita naona ni sawa maadamu ni kudai haki. Kuna mazingira yanahitaji vita ili ulete mabadiliko. Japo vita ni gharama kubwa
 
Hii inanikimbusha Newton 1st law of Motion 'An Object will continue to be in the state of rest or Uniform motion UNLESS UNBALANCED FORCE ACT UPON IT'

Hii ndio hali halisi ya Tanzania Hakuna kitakachofanyika, Hakuna kitakachobadilika katika Tanzania hii Unless Tumetumia njia Mbadala katika kuondoa udhalimu uliopo. This is the plain reality which we have to face. Unless tukubaliane kuwa tume-give up na tumeamua kuwaachia CCM waendelee kutawala Tanzania milele, waendelee kuindesha hii nchi jinsi wanavyotaka

Sijui kwanini watu mnadhani kuna kitakachobadilika tukiwa na subira na kutimia njia zile zile ambazo hazikuleta mabadiliko. Huu ni mwaka wa 20 tangu multiparty ianze Tanzania watu wamepigia kelele Tume Huru lakini hakuna kilichobadilika, Kama wanaharakati wamepiga kelele kwa miaka 20 bila mafanikio kwanini mnadhani wataweza kwa miaka 5 ijayo? kwanini mnafikiri 2015 kuwa mambo yatakuwa tofauti?

Kenya na Zimbabwe walikua na Subira kama sisi lakini hakuna kilichobadilika mpaka pale Subira ilipowaishia wananchi na kuamua kuchukua hatua ndipo mabadiliko yalipotokea. Kama tungekua tunatumia mbinu za "AMANI" katika kudai uhuru wetu ni dhahiri kua mpaka leo hii tungekuwa chini ya ukoloni.

Mara nyingi sana haki haitolewi, Bali Haki huchukuliwa. Kinachotakiwa ni kujadili mikakati na njia gani zitumike ili kuwafanya hawa mabwana wakubali kuwa na tume huru yenye kutenda haki kwa watanzania.

Ngoja ngoja utamkuta mtoto sii wako.
 

Mkuu Mpayukaji,

Haya unayoyasimamia ndiyo ninayosimamia mimi. Bahati nzuri hapa JF tunawasiliana kwa maandishi ambayo ni ushahidi tosha. Soma tena nilichoandika. Nilipokuwa nasema "Dr Slaa usituharibie nchi yetu" nilikuwa nanukuu kauli za akina Mzee Mwanakijiji (na niliweka quotation marks). Unajua matumizi ya quotation marks katika lugha?

Unanikumbusha kuhusu Marehemu Munga Tehenan alipokuwa akiandika katika gazeti la Majira akijiita "Kibaraka wa Dola" alikuwa akiikosoa Serikali kwa kuigiza kuwa yuko upande wao mfano angeweza kuandika, "Wananchi wakishatoa kodi hawanan haki ya kuhoji matumizi, serikali ina haki ya kula pesa Bwana! kwani inafanya kazi bure?" Wananchi wengi hawakumwelewa wakawa wanaomba Mhariri amfungie!!!!!

Angalia Mkuu mpayukaji, usipayuke tu kumbe hukuelewa.
 

I wonder what stage of grieving this post/thread is. Get on with the program, now you have even bigger ruzuku. Panueni chama. You are wasting a lot of energy and resources in a lost cause. Of which might backfire. Wabongo (wengi wasiopenda confrontational) watawaona mna uchu wa madaraka.

But--you can go ahead and press the issue. We will see where it ends maybe 3 months from today. Hamjaibiwa kura, you guys did not solicit every vote in this country. Ndio maana kura hazikutosha. That is the bottom line. Msitafute mchawi, do internal assessments, what ya' could have right, lesson learned--and move on. Hivi kweli mnaweza kusema mlipiga kampeni za kutosha mikoa ya kusini? au huko maTabora?

The idea kwamba Dr. Slaa akisikilizwa na wananchi, that would be enough kupata kura sio rahisi. People need to be convinced, local campaigners, makatibu kata na wajumbe wa nyumba 10. That is how you build the party network. And we can all agree, Chadema did not do that.

The truth is, hata hivyo viti vya ubunge mmepata kupitia mgongo wa CCM. Watu kama Shibuda, Iringa Mjini, Bukombe and others, mmepata kupitia mgongo wa CCM na sio kukubalika kwa sera zenu. Kama Mwakalebela angepita Iringa Mjini, Shibuda Maswa, na yule wa Bukombe--you guys could have 3 less seats. So stop all this whining and own up your mistakes, and move on. CCM can be defeated, but it won't be easy.
 
3D - Ni mbinu gani za matumizi ya nguvu (violent methods) ambazo unafikiri zinafaa kutumika sasa hivi Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi? Na kati ya hizo ni zipi wewe uko tayari kuzitumia ili kufikia malengo ya kisiasa.

Asante Mkuu MM,

Swali lako ni sawa na kumuuliza mtu, "Una maoni gani ya kipuuzi uliyonayo kuhusu......." So ni swalia ambalo tayari liko biased. Ni sawa na watu wanaotoa hoja humu JF halafu wanasema, "Nasubiri maoni tofauti ya wasiopenda maendeleo."

Sasa nitajibu swali lako (sitajibu kuwa njia zangu ni violent):

Nashauri pawepo (na nitashiriki) na maandamano ya amani nchi nzima kupinga haya matokeo. Maandamano haya yaendelee hadi pale jumuiya ya Kimataiifa na serikali yenyewe itakapokuwa tayari kukaa chini kujadili hali iliyopo. Wasomi wa vyuo vikuu, sekondari wasiingie madarasani hadi pawepo na mazungumzo juu ya uchaguzi huu.

Nikumbushe tu kuwa violence hutokea pale serikali zinapowanyima wananchi haki ya kupinga kile wasichokiafiki. Kama violence itatokea katika mchakato huu itakuwa imesababishwa na serikali. Siungi mkono mawazo ya "Acha tu."
 

Asante Mkuu, nashangaa kwanini akina MM hawaoni mambo rahisi kama haya!!
 
Ningependa mwanakijiji angekuja na angalau mfano hai wa nchi gani iliyokuwa ya kidikteta ilitumia njia mbadala zaidi ya nguvu ya uma kuingiza serikali halali ya wanainchi bila mizengwe?

Asante Mkuu, nami nasubiri atoe mfano tuujadili.
 
Mimi hata vita naona ni sawa maadamu ni kudai haki. Kuna mazingira yanahitaji vita ili ulete mabadiliko. Japo vita ni gharama kubwa

You are not serious. Vita vya Kagera tu ambavyo tulipigana kwa muda mfupi cost us a decade of development. Ushawahi kufika South Sudan, DRC, Liberia? Ukipata nafasi japo youtube uone mziki wa vita ukoje.

POa basi, unataka vita. Sasa nani apigane na nani? Chadema na CCM? with your 20% of 5 millions you think you have enough to kukusanya jeshi. Poa, let say unalo jeshi--mimi shemeji zangu ni Chadema damu, ingawa tunalewa Bar moja, sasa hapo vita itaanzaje? Acha mawazo haya babu.
 
Hakuna amani palipo na dhuluma. Hakuna njia yoyote ya amani katika kuleta mustakhbali mwema wa nchi yetu. CCM na serikali haiwezi kusimamia haki katika chaguzi kwa kuwa haina dhamira ya kweli, tena kwa kauli zao kukubaliana na matakwa ya wananchi. Kumbuka tahariri ya daily news, kuwa hata iweje, Slaa hawezi kuwa Rais wa awamu hii. Hii ni kauli ya serikali ya chama cha mapinduzi. Na hadi leo, hakuna kiongozi yeyote wa CCM aliyekaripia kauli hii, ama kumchukulia hatua mhariri huyo.

Naomba yeyote mwenye kuona mbali, aniambie ni njia gani ya amani ambayo wananchi waitumie, au vyama vya siasa vitumie ili kuleta haki hadi NEC na serikali hii, iheshimu matakwa ya wananchi?

Kwa mujibu wa mjadala huu, kimantiki wasemaji wa mwanzo wamejikita katika kutaka haki ipatikane mahakamani. Kuna haki gani katika mahakama zetu wakati zinaongozwa kwa shinikizo na matakwa ya watawala? Kumbukeni kesi ya mgombea binafsi. Mahakama si vyombo huru, polisi si chombo huru, NEC si chombo huru, takukuru si chombo huru na hata ofisi ya msajili si chombo huru.

Nionavyo mimi, haki itapatikana kwa njia nyingine za shinikizo za wananchi. Tuanze kushinikiza!!
 
mkuu hakuna anayepinga wazo lako hujasema tunataka violence sisi tumeesema tunahitaji kufanya maandamano na migomo ya amani,LAKINI KUMBUKA kuwa selikali hutumia jeshi kusawazisha mambo hapa ndipo NINAPOTAKA WATANZANIATUAMUE KAMA WALIVYOWAHI KUAMUA WATU WA THAILAND HAPO TUTAFANIKIWA.KUMBUKA UPOLE WETU UNALETA DHULUMA KWETU NA SUBIRA YETU YA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI NDO KASI YA KUIBIWA KWA RASILIMALI ZETU.TUUNGANE PAMOJA TUFANYE MAAMUZI YA PAMOJA ILI TUSHINDE KWA PAMOJA.
MUNGU IBARIKI AFRIKA,
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
AMEN!
 
COST of development mkuu ni siyo sababu ya vita ila ni matatizo ya mipango yetu na matumizi mabaya ya rasilimali zetu hebu ona aibu kwa huo usemi wako RWANDA wametoka kwenye mapigano juzi tu mbona leo wako juu zaidi yetu? mkuu fikiri kwa kina utaona nguvu ya umma ndo italeta suluhisho la kweli.
 
Asante Mkuu, nashangaa kwanini akina MM hawaoni mambo rahisi kama haya!!

Kaka, migomo ya wafanyakazi na maandamano ya wanafunzi will only work if you get the high turn out. The high turn out depends on the interest ya wanafunzi na wafanyakazi. Kwa Tanzania yetu hii ya leo, unategemea wafanyakazi wangapi ni wanachama wa Chadema? na ni wanafunzi wangapi wanaifagilia Chadema. Your assumption is Chadema is a mighty strong party, which is contrary to the truth. Ukiitisha maandamano, I guarantee you, utapata wahuni tu, who will expect some sort of mshiko at the end. Unless hayo maandamano yawe Jamii Forum, then you have a chance. But Jamii Forum is a virtual world, not the real one.
 

Let us assume kwamba Rwanda wako juu kama unavyodai. That is one county out of how many? Pili, Kagame akifa leo, Rwanda is in chaos. Tatu, hakuna freedom of speech Rwanda. As the matter of fact sisi tungekuwa Rwanda, Dr. Slaa couldn't even get this far. Nne, Rwanda has 6-8 million people, compared to 40 of ours. Tano, Kagame kawekwa na western power as a gateway to get DRC minerals ndio maana he has been given impunity for all repression act against Hutu and we have been fed with this image of a liberator (but in reality, Kagame is a monster) tafuta wahutu wa Rwanda uwaulize leo. And there is no independent journalism in that country.

You still want to take Rwanda's direction?
 
wajerumani ndo waanzilishi wa vita vyote vya dunia lakini leo ndo wana lead economy of euro.pia hata uganda yenyewe walipigana na sisi lakin mbona wao wana uafadhali. kaa chini jiulize kwanini maskini ilhali tuna rasilimali kibao? utagundua hawa watawala na CCM ndo source wala sio vita vya idi amin. pia ninapotoa mfano wa rwanda ninajua kabisa kuwa ina idadi ndogo ya watu kuliko sisi ila kumbuka hapa ninitaka tuangalizie wenzetu imekuwaje wameweza kurecover haraka kutoka vitani wakati sisi miaka hamsini bado tunadidimia tu.
 

Hata maandamano ya wenzetu huwa yanaanza na watu wachache kwa kuwa huwa kuna kundi linakaa pembeni kusoma mazingirra kwanza. Wengi wamechoka na situation ya sasa. Naamini maandamano yakianza yataendelea kukua na kukua, hili wazo la kupata wahuni katika maandamano all the time linatumiwa na wajanja kupandikiza dhana kuwa wanaopinga dhulma ni wahuni tu.
 
namfuu mwandika nsha mwingine ameweza kujibu!!
 
Nina kaugonjwa ka kupitia article ndefu ndefu ila ntajitaidi manake nimefanya kupitia juu juu inaonekana watu wana uzalendo wa kweli.
Tz ni yetu ni lazima tuitetee na kuilinda na kama mambo yanaenda fyongo lazima tuhakikishe yanaenda kwenye mstari as soon as possible
Otherwise watoto na wajukuu wetu watakuja tulaumu na kutuona vilaza kwa kuishi maisha ya bora liende
 
Kuna memba wa JF ameshauri wana JF wachanga wapewe muda wa mwezi mmoja wa “Kutazama kwanza hoja zinavyotolewa na wakongwe kabla hawajapewa nafasi ya kuchangia.”! Sawa bwana.
.

!!!!?????
 
'No Court shall have jurisdiction to inquire into anything done by the Electoral Commission in the exercise of its functions according to the provisions of this Constitution.'

Nashukuru saaana ndugu yangu kwa kipande hiki cha hukumu iliyoko juu. Naamini hii inaweza kuwa ndo sehemu ya kuanzia mjadala. On my views the only solution we have is ammendment of the constitution. Kwa mawazo yangu "ammendment of constitution is posible" under condition that, viongozi wa vyama vibaraka wanadhibitiwa. Watanzania tungeweza kubadili katiba ambayo ingeruhusu kuwa na tume huru ya uchaguzi, lakini viongozi vibaraka (namaanisha waliojitokeza kukubali matokeo na kusaini kwamba wameridhika huku wakijua kuwa yamechakachuliwa. Ni hao hao ambao walikimbilia kukubali kuingia kwenye kampeni ili hali wakijua kuwa wanacheza na refaree. Cha ajabu wengi wameshiriki miaka nenda na wamejitosa tena huku wakijua kuwa hawatapata hata asilimia kumi ya kura. Huku ni kuwahadaa watanzania kuwa wanataka mabadiliko kumbe wana nia zao nyingine na kufanya hapa kuwa kichaka chao. ombi langu tufike mahali tuangalie wasaliti tulio nao kabla ya kuangalia adui tulie nae tutapambana nae vipi. Tena hukumu kama hii bado wanayo na wanafahamu kuwa tume imemaliza na hakuna litakalobadilika hata kama tungeenda mahakamani. ombi langu tuangalie namna ya kuondokana na vibaraka ambao wamekuwa wakirubuniwa na ccm ili kukwamisha mabadiliko yatakayoletea kupata chombo chenye haki katika uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…