Nimesikitishwa sana na kauli ya Mzee Mwanakijiji ya tarehe 5 November, 2010 saa 3:05 asubuhi: "Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi" ambayo katumia muda mwingi kujaribu kujenga hoja kuwa katika ulimwengu wa waliostaarabu lugha "zinazochochea matumizi ya nguvu" hazina nafasi.
Nakubaliana na hoja kuwa nchi yetu kama nchi nyingine yoyote inahitaji kuwa na amani. Lakini natofautiana naye pamoja na watu wenye msimamo kama wake wa "Uchaguzi umeshapita, tuangalie mengine." Huu ni msimamo wa CCM (ambao ni wa hadaa). Nitaeleza.
CCM imekuwa mstari wa mbele kutumia vyombo vya habari hasa magazeti kumchafua Dr. Slaa na kumtusi. Magazeti kama Al-Huda yalifikia hatua ya kuchapisha picha za mafuvu ya binadamu yakidai Dr. Slaa kuchochea mauaji ya Mwembechai dhidi ya Waislamu. Magazeti kama Tazama, Taifa Letu etc yamekuwa yakimtukana Dr. Slaa na baadhi yao kugawiwa bure hasa yakiandika taarifa hasi juu ya Dr. Slaa. Gazeti la Serikali Habari Leo limemchafua sana Dr. Slaa. Gazeti la Serikali la Daily News lilitoa msimamo kuwa Dr. Slaa hatakuwa Rais wa tano wa Tanzania (Serikali kuu haikujitenga na kauli hii).
Mwishowe Magazeti ya Mwananchi na MwanaHalisi ndiyo yaliyotishwa kufungiwa badala ya Al-Huda na mengine. Baada ya Uchafuzi huu Magazeti haya sasa yanaombwa na Kikwete "Kusaidia kutibu vidonda vya Uchaguzi." Ni kweli yatafanya hivyo kwa kuwa Kikwete anajua kabisa kuwa ukihitaji magazeti yabomoe wakati wa uchaguzi yatumie halafu uchaguzi ukiisha yatumie tena kujenga kwa kuwa Watanzania ni mazezeta na wanaamini sana magazeti.
Kikwete anajua kuwa ukitaka kushinda iba kura, tumia majeshi kutisha na kupiga watu, tume ikishakuweka madarakani kwa ghilba wapo akina Mwanakijiji, Pengo, Mokiwa na Getrude Lwakatare ambao wakiongea tu "Kubalini matokeo, tunataka amani" basi Watanzania watakubali. Na akina Mzee Mwanakijiji wanatumia technique ya lugha "Katika ulimwengu wa wasomi" ili ukitofautiana nao uonekane siyo msomi na mpenda machafuko.
CCM wana akili timamu na wanaona kila hatua inavyokwenda. Uchaguzi utakuja, ataibuka Mrema au Slaa au Lipumba, atapigwa zengwe, ataitwa mdini. Kama ni Lipumba akigombea basi magazeti ya Kikristo ya kihafidhina yatamtukana Lipumba na kumwita mdini na mtu asiye na ndoa (Ilitokea year 2000). Kisha kura zitaibwa. Watu wote (including viongozi wa dini na akina Mzee Mwanakijiji) wataona kuwa kura zimeibwa. CCM itashinda. Polisi watapiga watu wanaodaiwa kuwa wapenda fujo na wanaotumiwa na viongozi waroho wa madaraka (Akina Dr. Slaa). Kikwete ataapishwa akiwa amejeruhi nchi.
Watu watabaki na alama za wino wa kura (indelible ink) huku wakizomewa na kutajwa kama wapenda fujo, wasokubali kushindwa, wanaotumiwa na wanasiasa na akina Mzee Mwanakijiji wataenda mbali zaidi na kuwaita "wasioelimika" na "waliojiunga JF juzi tu." Kuna memba wa JF ameshauri wana JF wachanga wapewe muda wa mwezi mmoja wa "Kutazama kwanza hoja zinavyotolewa na wakongwe kabla hawajapewa nafasi ya kuchangia."! Sawa bwana.
Ikumbukwe kauli za kuzuia Watanzania kudai haki yao na kutaka wawe makondoo (siyo kondoo) ni kuzuia mabadiliko. Haisaidii kutumia miaka milioni moja kujadili "nguvu za hoja" wakati inamchukua mgombea siku mbili kuchakachua kura na uongozi.
Pole Dr. Slaa. Pole sana. Najua hukutaka kugombea Urais. Ulichukua fomu ya Ubunge. Kamati Kuu ya CHADEMA ikakubana sana ugombee Urais. Ukakubali. Umejenga hoja sana katika kampeni (kama akina Mzee Mwanakijiji wanavyodai wanapenda). Kura zako zimeibwa. Sasa akina Mzee Mwanakijiji waliokushangilia wanakwambia "Uchaguzi umeshapita, tugange yajayo." Kwa maana fupi tu Dr. Slaa "usituharibie nchi yetu."
Watanzania wanapenda vitu vizuri lakini hawapendi gharama. Kwaheri Mkoloni Mzungu, karibu Mkoloni Mwafrika. Historia itatuhukumu. Nakubaliana na mawazo tofauti na yangu (kwa hoja lakini).
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania,
Nawasilisha.
Mkuu 3D,
Nakushukuru sana kwa tathmini yako nzuri. Mimi moja kwa moja na bila kupinda napingana na yeyote yule anayesema uchaguzi umekwisha, maisha yaendelee. Unajua nchi yetu imefikia kiwango cha juu cha ufisadi kiasi kwamba hakuna njia ya kuwaondoa hawa jamaa isipokuwa kwa nguvu ya umma. Kauli ya Mwanakijiji itatufanya tuingie katika uchaguzi 2015 katika hali hii hii na hakika hata yale majimbo tuliyoyatwaa yatarudi kwa ccm.
Hakuna mapinduziya kweli ambayo hayaendani na umwagaji wa damu hasa nchi inapokuwa katika hali yetu. Nitatoa mifano michache.
1. Ghana. Kama Jerry Rawlings asingetumia nguvu na kuwafurusha mafisadi, leo hii tusingeshuhudia Ghana yenye demokrasia ya kweli.
2. Rwanda. Kama Kagame asingeingia msituni na maelfu ya watu kufa, tusingesika Rwanda yenye amani ya kwel na maendeleo makubwa.
3. Kama Mandela na wa-south africa wasingetumia nguvu kupambana na kaburu, leo bado tungekuwa tunazungumzia ubaguzi wa rangi.
4. Kama Martin Luther King Jr asingehimiza wamarekani kwwa maandamano makubwa na wengine kupoteza maisha, leo hii tungekuwa bado tunazungumzia Marekani yenye ugomvi wa rangi.
5. Kenya. Kama wakenya wasingepinga matokeo ya uchaguzi yaliyochakachuliwa, leo hii tusingesikia Kenya iliyozaliwa upya na katiba ya kupigiwa mfano.
6. Zanzibar. Kama isingekuwa mauaji ya ndugu zetu kule Pemba walioandamana kupinga matokeo ya uchaguzi na wengine kukimbilia Mombasa, leo hii tusingesikia maridhiano yaliyoleta Zanzibar mpya.
Unaweza kuongozea orodha hiyo na ikawa ndefu. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa hakuna mapinduzi ya kweli kwa kukwepa kumwaga damu. Njia pekee inayoondoa wadhalimu ni nguvu ya umma. Kwa namna ya Tanzania kamwe usitegemee kuondoa mafisadi kwa sanduku la kura. Wana mbinu nyingi za kuiba, wanatakiwa watoke kwa lazima.
Mimi sisemi damu imwagike lakini nguvu ya umma itumike kuondoa ufisadi. Na kwa kweli nguvu ya umma ikiinuka wanaoua ni askari wa viongozi madhalimu.
Sasa napendekeza nini? Maandamano ya amani nchi nzima, tuandamane tukiwa tumenyanyua vitambaa vyeupe kashiria amani, nia hasa ni kuuambia ulimwengu kuwa kuna kitu hakikukaa sawa hapa. Tuonyeshe hisia zetu, najua kuwa JK na jeshi lake hawatakubali litokee hapo ndipo damu haina budi kumwagika, na damu hiyo itakuwa mbegu na chachu ya ukombozi wa mtanzania. Vinginevyo tusidanganyane hapa kuwa tutawaweza hawa jamaa. Lugha za mahakamani hizo ni porojo tu, utawala wa sheria kamwe haufanyi kazi katika jamii kama yetu.
Watanzania tuondoe woga, woga utatumaliza sisi na vizazi vijavyo, woga utatukosesha maziwa na asali Mungu aliyotuwekea. Tuache kuli lia ni wakati wa kuchukua hatua kali dhidi ya genge la JK na marafiki zake. Waoga wanyamaze kimya, wawaache makamanda waende vitani.
Tupeni mwongozo. Dr Slaa itisha mkutano wa kuwashukuru watanzania walio kuamini na kukupigia kura. Mikutano hii uifanye kila mji wa Tanzania, hawa mafisadi hawatakiwi walale usingizi kwa hii miaka mitano ijayo.
Mniwie radhi, haya ni mawazo yangu.