Elections 2010 Kutumia nguvu (violence) kwenye siasa kunaruhusiwa

Asante mkuu. Je unayo hotuba nzima ulikonukuu kipande chekundu hapo juu?
Nukuu hii imebeba maana nzito....hivyo nadhani na hotuba yote ilikuwa na ujumbe mzito!!
 

HAKIKA, HAKIKA, HAKIKA... WENYE MASIKIO na WAONE. WENYE KUSOMA NA WASOME. Ujumbe umefika, kama ni kisu KIMEKITA MFUPA. Ndiposa mimi hukubali kutokubaliana kwa hoja na mantiki.:smile-big:
 

Tazama ramani ya Africa. Maji mengi yako Tanzania (Lakes Nyasa, Victoria, Tanganyika, etc pamoja na mito miiiingi tu). Kwa nini hadi leo tuna shida ya umeme, kwa nini hadi leo hatutumii maji hayo kwa irrigation, kwa nini matunda yanaoza Lushoto wakati watu wana import matunda hayo hayo, ndizi Bukoba na Moshi zinaoza hakuna prosessing industries, etc etc, na wakazi wa huko wanaendelea kuwa masikini, etc, etc, etc...Wewe umebanwa kwenye attitute kwamba matatizo ya Tanzania hayawezi kuisha wakati mimi naona mabadiliko yanawezekana. Kuacha hizo reservations za Kagame ulizosema, hali za wananchi wake zinaendeled kuboreka kwa kasi kuliko sisi na hii ni aibu kwa nchi iliyopitia migogoro yote hiyo. Sisi kwa sasa tunaelekea kwenye botton si kwa duniani tu hata kwa East Africa
 
.

Mkuu 3D,
1.Tunashukuru kwa post yako.
Nafikiri tukichapana kidogo,itapunguza madudu yote haya.vita ni vibaya sana, lakini ufundisha.

2.Walianza kufanyiana wenyewe ccm kwenye kura zao za maoni na watu tuliandika,lakini JF mkayapuuza.Ata reseachers waliokuja hapa kyela,nao waliandika,lakini watu kama KAIL ambaye ni negative na close minded aliishia kufananisha ID za watu na ya kwangu.

3.Kwa mtindo huu,tusitegemee mageuzi ya kweli kutokea Tanzania.Tena uchaguzi ujao, upinzani utakuja kuanguka vibaya sana.CCM watakaa na kupata mbinu zaidi za kuiba.
 
heshima zenu wazee. tunahitaji kujenga hoja kama wachangiaji wa hapo juu. big up.
 
3D - Ni mbinu gani za matumizi ya nguvu (violent methods) ambazo unafikiri zinafaa kutumika sasa hivi Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi? Na kati ya hizo ni zipi wewe uko tayari kuzitumia ili kufikia malengo ya kisiasa.
Ndugu Mwanakijiji,
Kumbuka kuna watu/wanaharakati wengi sana duniani waliobadili mwelekeo wa nchi zao/Dunia. Mfano mzuri ni Marehemu Dr. Martin Luther King Jr. Huyu jamaa "Mungu amlaze mahali pema peponi" alipambana na uhafidhina/ubaguzi wa rangi Marekani na mpaka leo anaheshimika Duniani kwa kukemea ubaguzi wa rangi na uhafidhina duniani. Kufumbia macho wizi na ubakaji wa demokrasia ni upuuzi ambao haukubaliki. Watanzania tuamke huu ni wakati wa kupinga vitendo viovu vinavyofanywa na watu wachache kwa maslahi ya matumbo yao na watoto wao. Kumbuka kwamba maandamano sio violent methods inakuwa violent pale tu serikali inapotumia nguvu kuzuuia maandamano ya wananchi.
Jiulize ni kwa nini mpaka leo sisi ni masikini wakati tuna rasilimali za kutosha???
Ifikie wakati watanzania tuamke kudai ukombozi wa nchi yetu kutoka kwa watu wachache wanaofurahia rasilimali za nchi hii huku idadi kubwa ya wananchi wakielea kwenye dimbwi kubwa la umaskini.
 
Ni kosa kukubaliana na hali isiyo sawa kuwa ni sawa ili tu siku ipite. Hakuna mapinduzi yaliyowahi kufanyika kwa watu kufumbia macho vitendo vya ukandamizaji. Na ni kweli hakuna mtu anaependa nnchi yetu iingie katika umwagaji damu kwani madhara ya vita tumeyaona kwa majirani zetu. Lakini kwa kweli inachefua kuona hata wale wanaojulikana kuhusika na utafunaji wa jasho la waTanzania wakihojiwa wanakimbilia kumwagika kwa damu kama ngao ya kuwazuia waTanzania wasihoji hila zao. Kwa mfao ni majuzi tu Dr. Slaa aliweka wazi suala la E. Lowassa kufanya kikao cha siri cha kuhujumu kura za waTanzania lakini katika kujibu hoja hiyo E.Lowassa nae anagusia kuwa kuhoji hoji mambo kama hayo kutaleteleza umwagaji damu...

MBONA SISI KII HAWA VIONGOZI WETU WASHIKA NNCHI WAKISEMA KUWA UDUNI WA MAISHA YA WATANZANIA UKIACHWA BILA KUONDOLOWA UNAWEZA KULETELEZA UMWAGAJI DAMU???...BADALA YAKE UCHAGUZI UKIKARIBIA NDO KILA MMOJA ANAKIMBILIA KUTUMIA UMWAGAJI DAMU KAMA KICHOCHEA CHA KUPATA KURA NA KUWAFUNGA MIDOMO WANYONGE???

Hili linanifadhaisha mno...
 
Safi sana,nimeipenda hoja yako!!lazima haki tuidai.hatutoletewa kwenye kisahani!!
 
Hebu acheni porojo zisizo na maana, uchaguzi umekwisha tuendelee na maisha yetu... maisha sio kucheza bao unasafiri huku umekaa chini, au kujenga nyumba wkt hata kiwanja hujanunua, hivi mtu ulikuwa unaendesha bajaji au mkokoteni ulidhani Chadema wakishinda utaendesha ndege???? maisha ni yale yale hata huyo Silaha angeingia madarakani Im sure Watanzania msivyo na shukurani mwezi mmoja tu mngeanza kumpiga madogo........
 
Mimi hata vita naona ni sawa maadamu ni kudai haki. Kuna mazingira yanahitaji vita ili ulete mabadiliko. Japo vita ni gharama kubwa

Mkuu usemacho ni kweli lakini nadhani MMK hukumuelewa! Kwani MMK anasema badala watu kuanza kupiga mabomu kuna njia bora zaidi za demo. Zikishindikana ndiyo uende huko. Kila kitu kina mwanzo wake. Tuanze kwa kufanya maandamano ya amani kushinikiza NEC irekebishwe n.k. Hivyo wewe na MMK mko kwenye boat moja sema kila mtu kaingilia mlango wake.
 

Mkuu 3D,

Nakushukuru sana kwa tathmini yako nzuri. Mimi moja kwa moja na bila kupinda napingana na yeyote yule anayesema uchaguzi umekwisha, maisha yaendelee. Unajua nchi yetu imefikia kiwango cha juu cha ufisadi kiasi kwamba hakuna njia ya kuwaondoa hawa jamaa isipokuwa kwa nguvu ya umma. Kauli ya Mwanakijiji itatufanya tuingie katika uchaguzi 2015 katika hali hii hii na hakika hata yale majimbo tuliyoyatwaa yatarudi kwa ccm.

Hakuna mapinduziya kweli ambayo hayaendani na umwagaji wa damu hasa nchi inapokuwa katika hali yetu. Nitatoa mifano michache.

1. Ghana. Kama Jerry Rawlings asingetumia nguvu na kuwafurusha mafisadi, leo hii tusingeshuhudia Ghana yenye demokrasia ya kweli.

2. Rwanda. Kama Kagame asingeingia msituni na maelfu ya watu kufa, tusingesika Rwanda yenye amani ya kwel na maendeleo makubwa.

3. Kama Mandela na wa-south africa wasingetumia nguvu kupambana na kaburu, leo bado tungekuwa tunazungumzia ubaguzi wa rangi.

4. Kama Martin Luther King Jr asingehimiza wamarekani kwwa maandamano makubwa na wengine kupoteza maisha, leo hii tungekuwa bado tunazungumzia Marekani yenye ugomvi wa rangi.

5. Kenya. Kama wakenya wasingepinga matokeo ya uchaguzi yaliyochakachuliwa, leo hii tusingesikia Kenya iliyozaliwa upya na katiba ya kupigiwa mfano.

6. Zanzibar. Kama isingekuwa mauaji ya ndugu zetu kule Pemba walioandamana kupinga matokeo ya uchaguzi na wengine kukimbilia Mombasa, leo hii tusingesikia maridhiano yaliyoleta Zanzibar mpya.

Unaweza kuongozea orodha hiyo na ikawa ndefu. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa hakuna mapinduzi ya kweli kwa kukwepa kumwaga damu. Njia pekee inayoondoa wadhalimu ni nguvu ya umma. Kwa namna ya Tanzania kamwe usitegemee kuondoa mafisadi kwa sanduku la kura. Wana mbinu nyingi za kuiba, wanatakiwa watoke kwa lazima.

Mimi sisemi damu imwagike lakini nguvu ya umma itumike kuondoa ufisadi. Na kwa kweli nguvu ya umma ikiinuka wanaoua ni askari wa viongozi madhalimu.

Sasa napendekeza nini? Maandamano ya amani nchi nzima, tuandamane tukiwa tumenyanyua vitambaa vyeupe kashiria amani, nia hasa ni kuuambia ulimwengu kuwa kuna kitu hakikukaa sawa hapa. Tuonyeshe hisia zetu, najua kuwa JK na jeshi lake hawatakubali litokee hapo ndipo damu haina budi kumwagika, na damu hiyo itakuwa mbegu na chachu ya ukombozi wa mtanzania. Vinginevyo tusidanganyane hapa kuwa tutawaweza hawa jamaa. Lugha za mahakamani hizo ni porojo tu, utawala wa sheria kamwe haufanyi kazi katika jamii kama yetu.

Watanzania tuondoe woga, woga utatumaliza sisi na vizazi vijavyo, woga utatukosesha maziwa na asali Mungu aliyotuwekea. Tuache kuli lia ni wakati wa kuchukua hatua kali dhidi ya genge la JK na marafiki zake. Waoga wanyamaze kimya, wawaache makamanda waende vitani.

Tupeni mwongozo. Dr Slaa itisha mkutano wa kuwashukuru watanzania walio kuamini na kukupigia kura. Mikutano hii uifanye kila mji wa Tanzania, hawa mafisadi hawatakiwi walale usingizi kwa hii miaka mitano ijayo.

Mniwie radhi, haya ni mawazo yangu.
 
Amani ya kweli (hatuzungumzii utulivu wa kisiasa ambao hapa TZ unaitwa amani) inakiwepo mahali ambapo haki inatendeka. Usiwalaumu watu ambao wamwamua kufanya vurugu baada ya haki kuonekana haitendeki. Maisha ya wengine yanaweza hata kupotea kwa ajili ya kutafuta amani. Lugha za kuwafanya watun wachachamae wafuatile haki yao ili wapate amani ya kweli ni lugha nzuri (the end justifies the means). Amani yan kwely ina Gharama . tukitaka kuipata yatupasa kulipa gharama.

Mungu iobariki Tanzania na CHADEMA
 
Regemeleza, I may not be very familiar with legal jargons but in my lay-man understanding kuna mwanya wa kupinga udhalimu huu mahakamani. Thanky for enlightment. You must a lawyer!
 

Mkuu nashukuru umetupa mawazo tofauti kuhusu kufunguliwa kwa kesi ya kupinga matokeo ya urais. Wengi wetu si wajuvi wa sheria kama mimi lakini ukweli umetufungua macho. Kwa maelezo ya hiyo kesi ya Attorney General & 2 others VS Walid Kaborou (1996) inawezekana kupinga matokeo ya urais.
Lakini pia tuangalie kama hiyo option itazaa matunda. Kama tunaushahidi inawezekana tukawashitaki kwa watanzania na ulimwengu mzima na ikawa na matokeo mazuri zaidi ya kesi itakayochukua muhula mzima wa miaka mitano.
 
Every man gotta right to decide his own destiny,
And in this judgement there is no partiality.
So arm in arms, with arms, we'll fight this little struggle,
'Cause that's the only way we can overcome our little trouble.
BOB MARLEY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…