KERO Kutumia Trillioni 1.2 kuijenga Muhimbili ni dhihaka kwa Watumishi wa Afya

KERO Kutumia Trillioni 1.2 kuijenga Muhimbili ni dhihaka kwa Watumishi wa Afya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wizara ya Afya ijitafakari sana katika hili,, watumishi wa afya wanalia na Muundo wa mishahara miaka nenda miaka rudi,, tunaishia kusikia tu waziri akizungumzia kwenye majukwaa ya kisiasa suala la Muundo, Bunge lipo kinywa kujadili na kupitisha muundo Mpya wa Mishahara sekta ya Afya inchini,, leo hii wanapeleka Bajeti ya Trillioni 1.2 kujenga hospitali moja tu,, ili hali watumishi waliopo katika Hospitali za rufaa za Mikoa kuna masilahi Duni kote inchini, watumishi walioko hospitali hizi za Mikoa wanamadai ya malipo mbalimbali ambayo wakifuatilia kwa maofisa utumishi waliopo katika hospitali zao wanaishia kuambiwa madai yao yapo Wizarani yanashughurikiwa miaka nenda miaka rudi hayalipwii.

Na kipindi hiki cha Bunge la Budget utasikia wizara ya Afya imelipa madeni ya Watumishi kiasi kadhaa, ili hali katika uhalisia watumishi hawajalipwa.

Shida iko wapi ??
1. Je!! Ni usimamizi mbovu wa wizara ya Afya inchini ??
2. Je!! Ni usimamizi mbovu wa Maafisa Utumishi walipo katika hospitali hizi ??
3. Je!! Ni kukithili kwa siasa Katika sekta Nyeti kama hii inchini ??
4. Je!! Serikali haioni kua sasa ni wakati muafaka kutekeleza maslahi ya sekta hii nyeti hapa inchini ??
5. Je!! Serikali inasubiri ishuhudie migomo ya watumishi wa Afya ndio itekeleze maslai yao ??

Mtazamo;
1. Ni muda sasa serikali na Wizara ya afya itekeleze maslai ya kimuundo kwa Taaluma zote ndani ya sekta hii nyeti.
2. Serikali na Wizara ya Afya kuweka na kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa hospitali zote za mikoa hapa Inchini.
3. Kuliko kutumia fedha nyingi kufanya maboresho kwenye hospitali moja, ni bora kuimaliza hospitali za Rufaa Mkoa na kanda kutoa huduma ile ile ambayo inapatikana Muhimbili NH.
 
Ni muhimu waiboreshe Muhimbili kwa manufaa ya nchi, lakini pia wazingatie maslahi ya watumishi hususani kwenye ngazi za chini.

Haiwezekani Specialist wa Mkoani na Tamisemi walipwe kama General Practioner wa hospitali kama Muhimbili, MOI, JKCI na BMH.

Vivo hivyo, kwa kada nyingine nazo ambazo kuna utofauti wa malipo na watumishi wa hizo taasisi tajwa.
 
swali langu ni moja tu'

Mapato yanayopatikana muhimbili yanakwenda wapi? Au ndio posho?
 
Back
Top Bottom