Kutumiwa meseji za maombi ya urafiki

Kmmk ungejikoroga ukutane na kitu kizito
 
Ignore wote
Hii ni Spam mpya na ipo mitandao yote.Watu hao mara nyingi lengo sio Urafiki.Mfano kama ni whatsApp kuna group moja ulijoin ukijoin tu wanatuma auto message to all member inawafikia member wote..Mara nyingi wanataka Usave namba zao ili uone status zako ila wengi wanakua na lengo la kukushawishi ujisajili kwenye Network marketing zao ambazo wanadai/watakwambia wanapiga pesa kupitia Website izo..Na wengi ni Wanaume ila wanatumia character ya kike kwasababu ndio rahisi kushawishi

Chakufanya Ignore kisha piga block kwasababu hata ukiwatukana wao hawajali wanapokea message nyingi sana.

Vilevile ukienda Telegram utawakuta/watakufata inbox Mara nyingi wao watakushawishi ujiunge na crypto site walizojiunga hawa usiwajibu wewe piga Tofali au wapuuzie.

Ukienda X utawakuta,Facebook,IG kila mtandao utawakuta ila wengi lengo ni "refarral compaign" wapate maokoto kupitia wewe utakaejoin

Wengine wauzaji watapost viatu,nguo hawa nao piga Tofali tu
 
Hao wahuni tu ntawatwanga block
 
Huko
waja leo waondoka leo sio poa
 
Kuna mmoja alinijia pia. Ni manzi hakusema ametoa namba wapi, nikapiga chini. Wa pili juz kat tu akasema alikotoa namba yangu na mimi nikathibitisha ni kwel tuko wote katika group flan la wauza story wa jamii forum bwana singanojr . Nikasema okay uko wapi, alipojichanganya akasema Mafinga!.

Sasa kutokana na harakat zangi , Mafinga ni moja ya maeneo nayajua nje ndani nikampiga sana maswali na karika maoongez nikaanza kumtajia mpaka chocho za Mafinga na nikamwambia nitakutimbia after simetime nikitia mgui mafinga..

Mmhhh akaona huyu sioo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ , kama mipango ya kuniingiza mjini akaona kama haitakua rahis bile, akawasha gari akateleza!! Mbioool πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Hao kila siku napata wawili au watatu, wanatuma ujumbe hao hawachoki mpaka wengine nimeblock.

Kwa wale wafanya biashara za mtandao ni vyema kufanya matangazo bila kuwa kero kwa wengine.
Hivi ushawahi kufikiria kutafta watu toka kwenye LinkedIn. Like connecting and hookups ila na aina ile ya wanawake the corporate ladies.
 
Tapeli huyo, mi mtu akisema yuko nje ya Dar sihangaiki nae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…