Kutunza mazingira: Serikali ivilazimishe Viwanda vya Pombe kali kununua chupa zake zilizotumika

Kutunza mazingira: Serikali ivilazimishe Viwanda vya Pombe kali kununua chupa zake zilizotumika

Anonymous Caller

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
679
Reaction score
870
Salam wakuu.

Nimewaza sana kwanini viwanda vya pombe Kali (Distilled spirits) kama konyagi, kvant, vodka, dompo, wana design chupa nzuri sana tena zenye mionekano bomba.

Lakini cha kushangaza chupa hizo baada ya matumizi hutelekezwa na kuwa kero kwa uchafuzi wa mazingira yetu.

Sasa sijui kwanini viwanda hivi visije na utaratibu wa kurudisha ganda mara baada ya wateja wao kununua vinywaji hiyo ambao kwanza utapunguza gharama za kufyatua mavyupa mengine (returnable) na kutumia maganda hayohayo.

Pili probably hata bei itapungua? Mathalani chupa ya kvant kubwa ni roughly ni elfu kumi.je utaratibu ukiwa wa kurejesha ganda si bei itashuka? Mbona soda tunarudisha maganda kwanini ishindikane kwenye vinywaji vingine.

Binafsi nina kibanda changu huwa nauza vinywaji hivyo sasa kinachoniboa nina chupa takribani bajaji nne, sijui pa kuzipeleka wanunuzi hamna.

Viwanda havinunui, Watu hawanunui, sasa mavyupa haya yamegeuka kero na kibaya zaidi huwezi kuyachoma maana hayaungui moto.

Wito wangu kwa serikali ivilazimishe viwanda husika wawe wananunua chupa zao hata kwa kupima kwa uzito.
 
Ninachojua, hata hizo chupa za soda na bia ambazo ni "returnable" zina life cycle yake ambayo pengine ni mizunguko miwili tu sokoni(bia)

Bei ya chupa ni ndogo sana kama ilivyo kwa plastic; mchanga wa kuzalisha chupa unapatikana hapo Chamazi, caustic soda n.k si bei kubwa, hivyo kuyeyusha chupa zilizotumika na kuziondoa rangi ili uweze kutengeneza nyingine ni ghali zaidi kuliko kuanza upya.

Tani 1 ya chupa chakavu inanunuliwa kwa sh 70,000/= ahahahahahah
 
Kuna sababu imeipata kwanini kioo Ltd walisitisha ununuzi wa vigae. Kumbe walipiga hesabu zao, kununua vigae na kubadirisha rangi ni ghali mnoo bora wakachukue Mchanga chamazi
 
Hata hao wanaouza maji chupa ni nyingi mno zinazagaa, kasi ya kusikusanya, kama ipo, ni ndogo sana
 
Back
Top Bottom