Kuua bila kukusudia.

Kuua bila kukusudia.

The Donchop

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
294
Reaction score
378
Je mfano A na B ni wapenzi WA muda mrefu. Wakiwa mikoa tofauti, B anapata mpenzi C ambapo anaamua kumjulisha A kwa ujumbe wa simu.
Baada ya kupata ujumbe, A anakufa kwa mshituko. Je B atakuwa na kesi ya kujibu? Sharia inasemaje juu ya hili?
 
Hakuna kesi hapo,lazima kuwe na physical contact.
 
Katika kuestablish causation of death,huyu mtu atakutwa kafa Kwa mshtuko au HP
 
swali zuri.

hata lingekuwa kwa upande wa pili kuwa A kamfumania B akafa kwa mshituko, swali linakukuwa vile vile..

Ninanvyoona hapo itakuwa ngumu sana kuthibitisha B ana kesi ya kujibu, labda kama B alikuwa anajua kuwa A ana tatizo labda la moyo ila akaamua kumtumia, vinginevyo katika tukio kama hilo B hatakuwa na kesi ya kujibu maana alichofanya ni jambo la kawaida tu katika mfumo wa maisha wa binadamu ambapo unapokea habari mbaya na nzuri, na huwezi kutegemea habari nzuri kila muda
 
Je mfano A na B ni wapenzi WA muda mrefu. Wakiwa mikoa tofauti, B anapata mpenzi C ambapo anaamua kumjulisha A kwa ujumbe wa simu.
Baada ya kupata ujumbe, A anakufa kwa mshituko. Je B atakuwa na kesi ya kujibu? Sharia inasemaje juu ya hili?
Huyo jamaa atawajibika kwa kuua bila kukusudia ...
kwanza kitendo cha yy kumtumia ujumbe mpenzi wake akijua kua usaliti ni jambo lisilojema ni wazi kua anatambua anachokifanya sio sahihi"actus reus" ....na kufanya hivo anajua kua kitasabbisha hali isio nzuri kwa mpenz wake na kuamua kufanya "mens rea" ...hivyo atawajibika kwa INVOLUNTARY MANSLAUGHTER iliosababishwa na uzembe alioufanya ......
by YUNUS (DIL 2nd Year)
 
Sasa kama kuna Actus reus na Mens Rea si tayari ameshafanya mauaji kwa kukusudia?

Hakuna sheria hapa Tanzania inayokulazimisha uwe na mpenzi fulani hivyo basi alichokifanya huyo ni jambo la kawaida kwa sababu hakuwa na malice, labda kama alikuwa anajua jamaa ana tatizo halafu ampe taarifa mbaya makusudi vinginevyo huwezi kuthibitisha kama kulikuwa na malice au vinginevyo.

Habari mbaya tunazipokea kila siku katika maisha yetu, mfano mwingine ni kama wewe ni kiongozi labda kwa mfano mkuu wa mkoa , halafu umtumbue mtu kazini(fukuze) baada ya hapo mtu huyo afe kwa mshtuko/presha... ja utakuwa umemuua?

Nachotaka kumaanisha mtu kupokea taarifa mbaya au nzuri ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, sasa matokeo yake kwa kiasi kikubwa hayazuiliki na mto taarifa labda kama atakuwa anafahamu una tatizo fulani au nia fulani ovu ya kumdhuru kiafya, vinginevyo hakutakuwa na uthibitisho wowote ule
 
Kesi hapo itatoka wapi wakati mtu A yuko mbali kiasi hicho na mtu B yuko mbali pia hapo mtu B hata wakienda kumpima watakuta alikufa sababu ya mshituko na hata wakiamua kufatilia mshituko umetokana na nini hawana ushaidi Wa kutosha hivo hutafungwa
 
Labdaa transferd malice mkuu
Hata uzembe.

Mfano nyumbani kwako umezungushia shoti ya umeme lakini hujaweka maneno wala kiashiria chochote cha mtu kuchukua tahadhari halafu akaja mtu akagusa ukuta wako akapigwa shoti mpaka kufa utakuwa umemuua bila kukusudia japo hakuna physical contact baina yenu
 
Sasa kama kuna Actus reus na Mens Rea si tayari ameshafanya mauaji kwa kukusudia?

Hakuna sheria hapa Tanzania inayokulazimisha uwe na mpenzi fulani hivyo basi alichokifanya huyo ni jambo la kawaida kwa sababu hakuwa na malice, labda kama alikuwa anajua jamaa ana tatizo halafu ampe taarifa mbaya makusudi vinginevyo huwezi kuthibitisha kama kulikuwa na malice au vinginevyo.

Habari mbaya tunazipokea kila siku katika maisha yetu, mfano mwingine ni kama wewe ni kiongozi labda kwa mfano mkuu wa mkoa , halafu umtumbue mtu kazini(fukuze) baada ya hapo mtu huyo afe kwa mshtuko/presha... ja utakuwa umemuua?

Nachotaka kumaanisha mtu kupokea taarifa mbaya au nzuri ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, sasa matokeo yake kwa kiasi kikubwa hayazuiliki na mto taarifa labda kama atakuwa anafahamu una tatizo fulani au nia fulani ovu ya kumdhuru kiafya, vinginevyo hakutakuwa na uthibitisho wowote ule
Kuacha mtu usiempenda sio kosa kisheria ...ila kitendo hicho cha kuacha na namna ambavyo utaamua kumuacha mwenza wako ndio inayoweza kupelekea "UZEMBE" wa ww kuwajibishwa ...kwa sababu "UZEMBE" wa huyo jamaa ame "foresee consiquence" ambayo itatokea na kuamua kuzifikisha habari izo kwa kutojali hali ya mwenza . Kwaio hapo ni juu ya mahakama kuangalia ni jinsi gani habar hizo zimefikishwa...kama itagundua "NEGLIGENCE" ipo basi jamaa anaweza kuwa "Liable"
 
Ndio maana nikasema kwa hii scenario ni ngumu kuthibitisha uzembe labda kama jamaa alikuwa ana matatizo yanayojulikana kwa huyo mwingine tena ithibitishwe kabisa na nia ya kumsababishia tatzo lililopelekea kifo chake.

Ila kama ilikuwa kawaida tuu hata kama mimi nina matatizo tuseme ya moyo ila mpenzi wangu akanitumia message ya kuniacha itabidi upande wa mashtaka uthibitishe kwanza wajibu wa huyo mpenzi wangu kwangu, pili ni hatua gani zilipaswa zichukuliwe na mtu yyte reasonable
 
Sasa kama kuna Actus reus na Mens Rea si tayari ameshafanya mauaji kwa kukusudia?

Hakuna sheria hapa Tanzania inayokulazimisha uwe na mpenzi fulani hivyo basi alichokifanya huyo ni jambo la kawaida kwa sababu hakuwa na malice, labda kama alikuwa anajua jamaa ana tatizo halafu ampe taarifa mbaya makusudi vinginevyo huwezi kuthibitisha kama kulikuwa na malice au vinginevyo.

Habari mbaya tunazipokea kila siku katika maisha yetu, mfano mwingine ni kama wewe ni kiongozi labda kwa mfano mkuu wa mkoa , halafu umtumbue mtu kazini(fukuze) baada ya hapo mtu huyo afe kwa mshtuko/presha... ja utakuwa umemuua?

Nachotaka kumaanisha mtu kupokea taarifa mbaya au nzuri ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, sasa matokeo yake kwa kiasi kikubwa hayazuiliki na mto taarifa labda kama atakuwa anafahamu una tatizo fulani au nia fulani ovu ya kumdhuru kiafya, vinginevyo hakutakuwa na uthibitisho wowote ule
Na hata kama zikiwepo zote mbili ....mazingira hayo alotaja jamaa sio ya nia ya kumuua ..pengine ametaka kumuumiza kuhisia au vyovyote vile ikiwa anajua....jambo hilo halitoweza kupokelewa vzuri...mazingira hayo yanaweza kuwa "Actus reus" na "Mens rea" ipo lkn kosa likashuka na kua "Manslaughter" ...ni kama kule kule kwenye self defence..unajua km ukimpiga adui na silaha kichwani atafariki lkn umefanya hata km kuna "Actus reus" na "Mens rea" kawaida hua ni "murder" lkn ukahukumiwa kwa "Manslaughter" kutokana na defence yko...hivyo "Malice aforethought" inaweza kuwepo kwenye kosa la mauwaji na adhabu ikapungua degree yake kutokana na "circumstance"
 
Back
Top Bottom