Sasa kama kuna Actus reus na Mens Rea si tayari ameshafanya mauaji kwa kukusudia?
Hakuna sheria hapa Tanzania inayokulazimisha uwe na mpenzi fulani hivyo basi alichokifanya huyo ni jambo la kawaida kwa sababu hakuwa na malice, labda kama alikuwa anajua jamaa ana tatizo halafu ampe taarifa mbaya makusudi vinginevyo huwezi kuthibitisha kama kulikuwa na malice au vinginevyo.
Habari mbaya tunazipokea kila siku katika maisha yetu, mfano mwingine ni kama wewe ni kiongozi labda kwa mfano mkuu wa mkoa , halafu umtumbue mtu kazini(fukuze) baada ya hapo mtu huyo afe kwa mshtuko/presha... ja utakuwa umemuua?
Nachotaka kumaanisha mtu kupokea taarifa mbaya au nzuri ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, sasa matokeo yake kwa kiasi kikubwa hayazuiliki na mto taarifa labda kama atakuwa anafahamu una tatizo fulani au nia fulani ovu ya kumdhuru kiafya, vinginevyo hakutakuwa na uthibitisho wowote ule