Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Ukitembea utaona lakini utajengaje hoja ? anecdotal evidence haina mashiko!
Umesikia budget ya chuo ndugu? ni sawa na seating allowance ya wabunge kwa kikao cha siku moja je wao wanawezaje kufanya kitu kizuri bila resources?..."kitu kizuri gharama" walimu wanahaingaika kutafuta outdoor incomes, (muda mchache kuandaa nondo), wanafunzi wanahangaika kutafuta madawati kabla ya kuingia darasani akipata dawati hakuna nafasi ya kukaa, cycles goes on..wanfunzi wananunua mitihani of course kwa kushirikiana na wazazi wao ambao nao wana vyeti feki...na wa hela na nafasi...maskini wanamshawishi mwalimu ambaye yuko kwenye deep shit...cycles goes on.."bottom line peleka nje system CCM tuanze upya tunaweza kuchelewa lakini ni afadhali kuanza upya na kuweka misingi ya maana before it is too late" I mean 2010 .Hapo nilipokoleza rangi kwa kifupi si kweli kwamba vyuo vyetu vimeshindwa kutoa watu wenye taaluma ambao wanaweza kuwaza na kufanya mambo makubwa na yakaonekana binafsi naona policy za nchi yetu hazijalenga kuwasaidia vijana wengi ili kuweza kutumia taluma zao na matunda yakaonekana.
Nitoe labda mfano mmoja ambao naukumbuka wakati Mkapa akiwa bado madarakani alienda Botswana akapata fursa ya kutembezwa kwenye shamba la mifuko akawaona ng'ombe na wanavutia kuliko wale tunaochunga badala ya kufuga TZ ilimbidi ahoji kwamba wamefanya nini hadi wakafikia mafanikio hayo alishangaa kuambiwa kuwa ni vijana wako waliomaliza VET SUA ndo wanaoweza kujibu hili swali.
Kuna haja ya kujiangalia zaidi kwanini watanzania wengi hatupo productive kwa nchi yetu achilia mbali mafisadi n.k Hapa utaona kwa jinsi gani nchi yetu ilivyo na allergy na wataalamu wake.
Na tufanye nini ili tuweze ku import raw materials na ku export manufactured goods tofauti na kinyume tunavyofanya sasa?
nimeweka hizo takwimu ili kufunua macho tuone kama kweli ni tambarare kama inavyofikiriwa...
Hizi takwimu ni za hali generally.... Vijijini wala usiseme!
Naomba umalizie datas kwa kuonyesha ni aslimia ngapi ya watanzania hawajui kwa nini wawe kwenye daftari la wapiga kura na hawajui kwa nini wapige kura.
Ukitembea utaona lakini utajengaje hoja ? anecdotal evidence haina mashiko!
Ukiishi nchi za watu kwa muda ukirudi TZ.
utaliona hilo.kwa sababu zisizofahamika,watanzania wameridhika na walivyo sasa.natamani watanzania milioni 40 wangepata nafasi 1 tu ya kutembelea EU na kurudi.things would never be the same!
ni kazi kumtambua mwenye virusi sio umasikini wa watanzania
THAT IS SOO OBVIOUS.
88.4 ...ianikumbusha redio ya watu Clouds FM mhh!
Nitajitahidi kuchangia hoja zako kama ifuatavyo na huenda wengine wataongezea:
Kura/kuchagua viongozi
Kura ni nguvu ya mwananchi kuamua hatma ya uongozi kwa taifa na ni silaha kubwa, ila wananchi hawajui ukubwa wa silaha hii.Kura ikitumiwa vizuri inaweza kuleta mabadiliko to the better kwa maana ya kuwaweka madarakani viongozi makini wenye ari ya kuleta mabadiliko ya kweli.Kura hii hii ikitumiwa vibaya inaweza kulididimiza taifa moja kwa moja.Kinachotokea ni kuchanganya kura nzuri na mbaya ambapo tunapata cocktail ya wawakilishi - wema na wabaya na hawahawa wanakuja kuchanganyika kwenye chungu kimoja.Kwa msingi huu hata pawe na jitihada kubwa namna gani kubadilisha maisha ya wananchi, inakuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Chukulia chaguzi zote zinazofanyika, haina maana kuwa wanaochaguliwa wote ni wabaya.,La hasha.Baadhi ni wazuri tena waadilifu.Ila wanapomelt kwenye chungu kimoja...matokeo unaweza kufikiria mwenyewe.
Swali - je mwananchi akishapiga kura yake , what next? Watanzania mara nyingi wakishapiga kura wanajiona wamemaliza kazi.Hawajishughulishi kuwafuatilia wabunge wao na kuwabana mbavu kuhakikisha wanatimiza ahadi walizotoa.Hawajishughulishi kufuatilia shughuli mbalimbali za umma katika ngazi zote kuona je kile serikali ilichoahidi ndicho? NGOs zinajitahidi lakini bado sauti yao ni ndogo.Pia kuna forum mbalimbali ambazo zingeweza kutumika kuwabana viongozi lakini ushiriki wa wananchi bado kabisa - na pia haileti effect kubwa sana pale baadhi ya vikundi au hata forums kama hizi JF na zingine wanapopiga kelele kama tunavyofanya.Hii wakati mwingine inaonekana kama vijikelele vya wakosaji na hupuuzwa.Fikiria hizi kelele zingepigwa na makundi makubwa ya wananchi nadhani effect ingekuwa kubwa na huenda mabadiliko makubwa yangetokea.
Changamoto - kelele kama hizi ziwashirikishe vipi wananchi wengi zaidi? Sina jibu rahisi.
2. High fertility rate
Kama ulivyosema vema, high fertility rate ni kigezo au kiashiria cha umaskini na pia ni matokeo ya umaskini - si unajua tena TAJIRI NA MALI YAKE, MASIKINI NA WATOTO!Huwezi ukawa na rundo la watoto ukategemea uweze kujikwamua na umasikini.Mara nyingi uzazi wa mara nyingi na muda karibukaribu huchukua nguvu, fursa na hata muda wa mzazi hasa mama ambayo angeweza kujishughulisha na uzalishaji au kuongeza kipato.Vile vile kwa sababu ya umaskini, hakuna shughuli za ziada ukiachilia mbali unywaji na kulala ( matokeo ni kuongeza watoto).Ni viscious cycle.Mipango ya kuhamasisha watu wapange idadi ya watoto imekuwepo lakini uitikiaji wake sijui una mashiko kiasi gani.Serikali za nchi mbalimbali kama China na hata India na kwingineko zimewahi kuchukua drastic crude measures kuhakikisha familia zinakuwa na idadi ndogo ya watoto.China ilikuwa na one child policy - na ukizaa zaidi ya mtoto mmojaunawekewa vikwazo hadi uone moto.Swala likwaja, familia zikaanza kushuriki utoaji mimba ili kupata mtoto huyo mmoja wa kiume.Mimba za watoto wa kike zikawa zinatolewa.Huko India hivyo hivyo na hata ukatili kwenye familia kwa wanawake na watoto wa kike uliongezeka kufikia hata kuwaua watoto wa kike kwa njaa ,hawanyonyeshwi, wala kupewa huduma wakiwa wagonjwa!Huko Nigeria waliwahi kuwa na sera ya kila amilia iwe na watoto wanne maximum.Ikawa kwa wanawake kuwa na watoto wanne lakini unakuta mume ana wake zaidi ya mmoja.Mpango ukawa hauma maana yoyote.Hili suala la kupunguza idadi ya watu nalo liko tete.Huko India nako enzi za Indira Gandhi, mpango ukawa lenga wanaume - wanaume hata walifanyiwa vasectomy kwa nguvu ili kuhakikisha idadi ya watoto/watu haiongezeki kiholela.( ukimlenga mama tu , mwanaume atakuwa bado na uwezo kuzalisha! Hivyo target ikawa wanaume na hili lilim cost katika siasa.Nadhani wananchi wanapaswa kutambua kuwa idadi kubwa ya watoto inaongeza adha na mateso na umaskini ili wenyewe wachukue jukumu kujipangia uzazi.Kwamba serikali itaweka umeme kila mahali ili angalau kupunguza adha na shurba za maisha, tusubiri maana kisingizio sasa ni mvua haba, mitambo mibovu, uchumi wa dunia uliodorora nk.Sijui mipango ya umeme wa sola nao iko vipi.
R U kidding me?!Unless niwe sijakupata point yako ndugu yangu.Kuridhika kwa watanzania kama nilivyogusia huko mwanzo katika posts zangu ndilo hasa tatizo.
Kutembelea nchi za watu na kurudi hakutaleta mabadiliko kama unavyofikiria.Hao viongozi wetu kila leo wako safari hukohuko kwa wenzetu.Ni mabadiliko gani ya ajabu sana wameleta? Ukiacha viongozi, sasa hivi watanzania wengi tu wanasafiri sana kwa shughuli mbalimbali - biashara, mafunzo, kikazi n.k.Wengi wakirudi wanashindwa hata kujiletea mabadiliko kidogo katika ngazi za kaya zao sembuse kuleta katika ngazi ya nchi!
Kama ni exposure - nadhani watanzania haishi tena kwenye closed society ambapo tumejifungia hatujui nini kinaendelea nchi za wenzetu - thanks to media and different forms of communication.Kila kitu sasa kinafanyika na kuonekana kila mahali in real time.Juzi tu wamezindua THIS IS IT YA MJ DUNIA NZIMA na hata TZ watu wamejionea kama wenzao huko kwenye ustaarabu.Ninachotaka kusema ni kuwa the problem isnt so much one of lack of exposure bali kuna laxity at all levels.Gone are the days ambapo you had to wait years kuelewa trends zilizoko kwenye ulimwengu wa kwanza.
R U kidding me?!Unless niwe sijakupata point yako ndugu yangu.Kuridhika kwa watanzania kama nilivyogusia huko mwanzo katika posts zangu ndilo hasa tatizo.