R U kidding me?!Unless niwe sijakupata point yako ndugu yangu.Kuridhika kwa watanzania kama nilivyogusia huko mwanzo katika posts zangu ndilo hasa tatizo.
Kutembelea nchi za watu na kurudi hakutaleta mabadiliko kama unavyofikiria.Hao viongozi wetu kila leo wako safari hukohuko kwa wenzetu.Ni mabadiliko gani ya ajabu sana wameleta? Ukiacha viongozi, sasa hivi watanzania wengi tu wanasafiri sana kwa shughuli mbalimbali - biashara, mafunzo, kikazi n.k.Wengi wakirudi wanashindwa hata kujiletea mabadiliko kidogo katika ngazi za kaya zao sembuse kuleta katika ngazi ya nchi!
Kama ni exposure - nadhani watanzania haishi tena kwenye closed society ambapo tumejifungia hatujui nini kinaendelea nchi za wenzetu - thanks to media and different forms of communication.Kila kitu sasa kinafanyika na kuonekana kila mahali in real time.Juzi tu wamezindua THIS IS IT YA MJ DUNIA NZIMA na hata TZ watu wamejionea kama wenzao huko kwenye ustaarabu.Ninachotaka kusema ni kuwa the problem isnt so much one of lack of exposure bali kuna laxity at all levels.Gone are the days ambapo you had to wait years kuelewa trends zilizoko kwenye ulimwengu wa kwanza.
Sasa hizi trend za maji safi na salama,umeme,huduma za afya mbona zinachukua light years kutufikia?!
sioni kwamba kuona movie ya "this is it" ya MJ kunamfungua mtu macho kwa njia yoyote ile.
Mfano wangu wa watanzania Millioni 40 ni kuonesha kuwa asilimia kubwa ya watanzania hawana "the right exposure".
Nilikuwa vijiji vya jirani na Kamtimbo,mpanda miezi kadhaa iliyopita na nadiriki kusema kuwa Tanzanaia ya "exposure" iko hapa JF tu.kule kwa wananchi wa kawaida swala zima la Umeme,maji safi na salama,"interenet",huduma bora za afya ni mtego kwao.cha kushangaza wameridhika mno na hali hiyo.kwao Kikwete anaongoza nchi vizuri mno.hawalalamiki kama sie.
Hao viongozi na wakuu wa idara tunawaona wakija huku ughaibuni,wao ni kufikiria per diem,na kushangaa tu,wachache sana wanarudi kuhimiza maendeleo.
Watanzania ninaoongelea kuwa hawana exposure ni wale wanaojaza daftari la wapiga kura huku wakiwa hawajui sifa za mtu wanayempigia kura.
inasikitisha pia kuona kuwa asilimia chini ya 10 ya wananchi ndio wana--enjoy huo umeme na maendeleo' ya Tanzania.
Watanzania waliopata nafasi ya kwenda nchi za watuu kama wewe matunda yake tunayaona hapa JF.kila siku mnakemea maovu na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike.sio kwamba hao viongozi hawajui nini kifanyike ila <<their "love" to greener life is blinding them>>.
Hata wale wananchi wa "mpanda et al" mnawaona wakifika dar,wengi wao hulowea dar,kwani maisha huyaona bora tofauti na walivyoona awali.
Sisi watanzania wengi sasa hivi ni kama vyura ndani ya kisima,tunaiona dunia kupitia upana wa kisima,laiti tungelitoka nje ya kisima' hawa watu wasingetuchezea na mgao wa umeme miaka nenda rudi.