Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Kuuawa kwa kiongozi wa Hamas 'haisaidii' mazungumzo ya kusitisha mapigano, asema Biden
Rais wa Marekani Joe Biden amesema kuwa mauaji ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh "hayasaidii" mazungumzo kuhusu uwezekano wa kusitisha mapigano huko Gaza.
Rais wa Marekani Joe Biden amesema kuwa mauaji ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh "hayasaidii" mazungumzo kuhusu uwezekano wa kusitisha mapigano huko Gaza.
Haniyeh aliuawa katika ziara yake katika mji mkuu wa Iran, Tehran siku ya Jumatano. Iran na washirika wake wameilaumu Israel, ingawa Israel bado haijatoa maoni yoyote kuhusu kifo chake.
Haniyeh alikuwa afisa mkuu wa Hamas na alihusika sana katika mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka kutoka kituo chake nchini Qatar.
Bwana Biden alisema "ana hofu sana" kuhusu kuongezeka kwa mvutano katika Mashariki ya Kati. "Tuna msingi wa kusitisha mapigano. Yeye [Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu] anapaswa kuendelea nao [Hamas] wanapaswa kuendelea nao sasa."
Israel na Hamas hivi majuzi walianza tena mazungumzo ya muda, yasiyo ya moja kwa moja ili kujaribu kufikia usitishaji wa vita huko Gaza, ingawa kumekuwa na maelezo yanayokinzana kuhusu mafanikio ya mazungumzo hayo.
Mwishoni mwa mwezi Mei, Bw Biden alielezea kile alichosema kuwa ni masharti ya pendekezo la Israeli la kusitisha mapigano. Huu umekuwa msingi wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Hamas na Israel tangu wakati huo, huku Qatar, Misri na Marekani zikiwa wapatanishi.
Mapema wiki hii, Israel na Hamas zilishutumu kila mmoja kwa kukwamisha maendeleo ya mazungumzo.
Hamas ilisema Israel imeanzisha masharti mapya, huku ofisi ya Bw Netanyahu ikisema Hamas imetaka kufanyika kwa mabadiliko 29 kwenye pendekezo hilo.
Chanzo: BBC