Kuuawa kwa Wanajeshi wetu wawili Congo. Je, kuna haja ya TISS na JWTZ kuiga utendaji wa MOSSAD na Jeshi la Israel?

Kati wa watu wanaothamini sana uhai wa watu wao hapa duniani ni Israel. Ikitokea raia wa Israel au Mwanajeshi wa Israel amefariki kwenye mapigano au tukio lolote lile la Kigaidi haijalishi inapita muda gani, Israel ni lazima walipize kuuliwa kwa mtu wao.

Tabia hii ya Israel inapekea sio tu kuheshimiwa na mahasimu wao bali kuogopewa sana duniani katika medani za intelejensia na vita. Shirika lao la Ujasusi (MOSSAD) pamoja na vikosi vya jeshi lao wanafahamika sana kwa kutekeleza mission mbalimbali kwa ajili kulipiza vifo vya watu wao ili kutuma ujumbe kuwa wao sio watu wa kawaida.

Sote tumesikia kuwa Wanajeshi wetu 2 wameuwawa huko Congo pamoja na wengine 25 kujeruhiwa. Mauaji hayo yamefanywa na wanamgambo wa M23 ambao wanaungwa mkono na Rwanda.

Mbaya zaidi tumesikia kuwa Rwanda imefanya vitendo vya kuwadhalilisha kisaikolojia wanajeshi wetu wakati wanavuka mpaka wakiwa na Wanajeshi wa SADC ambao pia wamejeruhiwa kwa kuwachelewesha masaa kadhaa mpakani.

Baada ya matukio haya ambao sio tu yameliumiza Jeshi letu bali Watanzania wote tunaoipenda na kuijali kweli nchi yetu, Swali langu ni Je, kuna haja kwa Shirika letu la Ujasusi na Jeshi letu kulipa kisasi kutokana na mauaji na kujeruhiwa kwa ndugu zetu kama wanavyofanya Mossad na IDF?

Hawaoni kuna haja ya kufanya hivyo au ndo tumeshakubali rasmi sasa kuwa Rwanda ndo mtabe wa Afrika kwamba tumemshindwa na wanaomuweza ni Wazungu tu?
waache kumlipa Mond 300m kukatika mauno kwenye kampeni , waje waige Mossad , hv hujui kipaumbele cha ccmu ?
 
Wanajeshi wetu walikuwa wanalinda maslahi ya nani? Kama taifa tulikuwa na taarifa kuwa tuko vitani?
Kuna nationalism kwa majority ya raia? Ni kama wengine wako sidelined katika ugawanaji keki ya taifa ila mnataka muwavalishe wote gunia la responsibilities za revenge huku keki 'openly' ikiliwa na wachache.
Huyo unayewaza kumuendea kwa MOSSAD style ni mbobezi katika mambo hayo, do your research utagundua ni kitu gani kinachomfanya ajiamini. Iwe conventional au non-conventional means jamaa ni MAFIOSO mbobezi, Nyerere ndiyo aliweza mbinu hizo na kulikuwa na uzalendo to the extent that the majority of the population walikuwa tayari ku-sacrifice kwa lolote.
Ndio maana niliwahi kuandika humu kuwa katika kipindi hiki nchi yetu is very vulnerable kwasababu majority ya wananchi hawana Imani na Samia na serikali yake!! Wananchi are not sympathetic na what happened; may be a few ccm CHAWA!
 
TISS waache wahangaike na rasilimali watu,uchumi na huduma za jamii.
JWTZ wanacho kitengo chao kinafanyakazi vyema kabisa. kitengo cha usalama cha JWTZ kinaweza tu kuwaelekeza TISS kama kuna cha kufanya/kufuatilia.
 
Kati wa watu wanaothamini sana uhai wa watu wao hapa duniani ni Israel. Ikitokea raia wa Israel au Mwanajeshi wa Israel amefariki kwenye mapigano au tukio lolote lile la Kigaidi haijalishi inapita muda gani, Israel ni lazima walipize kuuliwa kwa mtu wao.

Tabia hii ya Israel inapekea sio tu kuheshimiwa na mahasimu wao bali kuogopewa sana duniani katika medani za intelejensia na vita. Shirika lao la Ujasusi (MOSSAD) pamoja na vikosi vya jeshi lao wanafahamika sana kwa kutekeleza mission mbalimbali kwa ajili kulipiza vifo vya watu wao ili kutuma ujumbe kuwa wao sio watu wa kawaida.

Sote tumesikia kuwa Wanajeshi wetu 2 wameuwawa huko Congo pamoja na wengine 25 kujeruhiwa. Mauaji hayo yamefanywa na wanamgambo wa M23 ambao wanaungwa mkono na Rwanda.

Mbaya zaidi tumesikia kuwa Rwanda imefanya vitendo vya kuwadhalilisha kisaikolojia wanajeshi wetu wakati wanavuka mpaka wakiwa na Wanajeshi wa SADC ambao pia wamejeruhiwa kwa kuwachelewesha masaa kadhaa mpakani.

Baada ya matukio haya ambao sio tu yameliumiza Jeshi letu bali Watanzania wote tunaoipenda na kuijali kweli nchi yetu, Swali langu ni Je, kuna haja kwa Shirika letu la Ujasusi na Jeshi letu kulipa kisasi kutokana na mauaji na kujeruhiwa kwa ndugu zetu kama wanavyofanya Mossad na IDF?

Hawaoni kuna haja ya kufanya hivyo au ndo tumeshakubali rasmi sasa kuwa Rwanda ndo mtabe wa Afrika kwamba tumemshindwa na wanaomuweza ni Wazungu tu?
Hawa mossad na idf wanaopigana na watu wasiokuwa na silaha na kushindwa kuokoa mateka zaidi ya miaka kwenye kieneo sawa na kijiji ndio tuwaige?
Watu wengi hamjui sheria na kazi ya jeshi la kulinda amani, mnadhani wameenda kupigana
 
Back
Top Bottom