mmmuhumba
JF-Expert Member
- Nov 8, 2017
- 493
- 478
Ni ukweli mchungu kuwa ipo siku tutakufa na kila kitu kilichopo katika ulimwengu hakitodumu bali kinapita.
Ni muhimu sana katika shida zote ukatambua na wewe unahitaji kupata muda wa kuyafurahia maisha yako kwa hali yoyote ile iwe kwa kingi ama kidogo ulichonacho.
Katika mahusiano, wapo watu wanaishi katika mazingira magumu ya manyanyaso, kutengwa, kudhalilishwa na kunyimwa haki zao za msingi na wapenzi/ wenza wao lakini bado wanaendelea kukubali kuishi maisha hayo hayo wakiamini ipo siku huyo anaye mtendea mwenza/ mpenzi:
i/ Atabadilika
ii/ Atamheshimisha
iii/ Ataiona thamani yake
iv/ Anacholingia kitaisha na atatulia naye.
Ni kweli tunapaswa kuishi katika imani kama mapenzi yenyewe yalivyo imani lakini kuendelea kukubali kupokea maumivu ya mapenzi kwa mtu ni kosa kubwa ambalo hupaswi kulifanya.
Lazima tujikumbushe, yeyote mwenye kukupenda huwa hakatazwi kwao, kwa lolote jema akupendaye atakubali kufanya awezalo kuwa nawe. Yeyote mwenye kukupenda upenda uwepo wako, hivyo kwa namna awezayo upambana kuhakikisha unaendele kubaki upande wake. Yeyote mwenye kujua maana ya wewe kuwa wake, atakuheshimisha na kukuheshimu.
Maisha yetu huvurugika sana pindi tunapoacha kufikiria kwa kutumia kichwa na kuanza kufikiria kwa kutumia Moyo.
Moyo huwa ni hisia zinazotawala za kufurahisha mwili, mara nyingi ubomoa matarajio ya watu wengi.
Yote, ujasiri katika mapenzi ni afya ya akili, hata kama umependa namna gani kubali ukweli kwamba hupendwi, kubali ukweli wewe siyo wa thamabi tena kwake, kubali ukweli kuwa manyanyasiko yako na maumivu yako siyo bure bali ni kusudio la wewe kutoka na kuelekea sehemu nyingine.
Kukubali kuishi katika mateso unayotendewa na unayesema unampenda ni kujichagulia maisha yako, utateseka hebu shuta.
Ulimwengu wa sasa hauna mwanaume mbaya wala mwanamke mbaya, kila mja upata amfaaye, ukiona ufaani naye na ushajaribu kumjenga na umeshindwa kumbadilisha, tambua huyo siyo wako.
#imarika.