hata mimi huwa na tatizo hilo hasa tunapokaribia dar es salaam. njia ninayotumia kupunguza maumivu ni hiyo ya kuziba vitundu vya pua kwa vidole na kuachama mdomo wazi ili uvute hewa kwa kutumia mdomo kama mara mbili au tau then unafunguka mdomo huku ukiwa bado umeziba pua zako kama kwa sekunde arobaini au dakika moja inategemea na pumzi zako kwenye zoezi hilo utaona jinsi upepo (pressure) inatafuta njia ya kutokea kwenye masikio na masikio yakizibuka then unaendele vizuri na safari yako ama utatua bila maumivu makali masikioni.