Bubu ataka kusema,
Hivi kweli watu wenye kipato kidogo wanalipa kodi Tanzania? Naomba uziorodheshe kodi wanazolipa na viwango ili tuanze kuzipigania hapa.
Halafu kuna jambo jingine hapa inabidi tuwe wazi, unapokuwa mfanyabishara lengo lako kubwa ni kupunguza gharama na kuongeza kipato. Kama umeweza kupunguza gharama kama Vodacom basi wewe ni mfanyabishara mzuri. Kwa mawazo yangu hapa wa kulaumiwa ni aliyotoa msamaha huo. Jambo jingine la kuangalia ni faida gani taifa limepata kutokana na msamaha huo wa kodi. Kama Vodacom isingekuwepo taifa lingepata faida gani au hasara gani. Lazima tukumbuke ili kuendelea kiuchumi "communication" is no.1 factor.
Hivi ndivyo watanzania wanavyowajaza mapesa mafisadi
Viwango vilivyokuwa vinatumika
Mapato na kodi kwa mwezi
Shilingi 0 mpaka Shilingi 80,000 -Asilimia sifuri
Shilingi 80,001 mpaka Shilingi 180,000 -Asilimia 15 ya kiasi kinachozidi Shilingi 80,000
Shilingi 180,001 mpaka Shilingi 360,000 -Shilingi 15,000 kuongeza asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Shilingi 180,000
Shilingi 360,001 mpaka Shilingi 540,000 - Shilingi 51,000 kuongeza asilimia 25ya kiasi kinachozidi Shilingi 360,000
Zaidi ya Shilingi 540,000 - Shilingi 96,000 kuongeza asilimia 30 ya kiasi kinachozidi Shilingi 540,000
Viwango Vipya
Mapato na kodi kwa mwezi
Shilingi 0 mpaka Shilingi 100,000 - Asilimia sifuri
Shilingi 100,001 mpaka Shilingi 360,000 - Asilimia 15 ya kiasi kinachozidi Shilingi 100,000
Shilingi 360,001 mpaka Shilingi 540,000 - Shilingi 39,000 kuongeza asilimia 20ya kiasi kinachozidi Shilingi 360,000
Shilingi 540,001 mpaka Shilingi 720,000 - Shilingi 75,000 kuongeza asilimia 25ya kiasi kinachozidi Shilingi 540,000
Zaidi ya Shilingi 720,000 - Shilingi 120,000 kuongeza asilimia 30 ya kiasi kinachozidi Shilingi 720,000
Wengine wetu tunalipa kodi mpaka laki tatu na zaidi mtu unashangaa kwa nini kampuni kubwa kama Voda isilipe kodi.