Kuumia kwa Erasto Nyoni: Viongozi wa Simba tuliwaonya kupeleka timu A Mapinduzi Cup

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika ni busara kwa Viongozi kuwa na busara ya kuwasikiliza walio chini yao.

Klabu ya Simba ina kabiliwa na Mashindano makubwa barani Afrika.

Mashindano hayo yanahitaji Wachezaji wenye uwezo na uzoefu mkubwa .Kutokana na hali hiyo baadhi ya wapenda soka tulitoa ushauri kwa viongozi wa Klabu ya Simba kutopeleka Timu ya kwanza huko Zanzibar kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup badala yake wapeleke kikosi cha Pili.

Sababu za kuwafanya hivyo ni kuwalinda Wachezaji wa kikosi cha kwanza wasiumie lakini Viongozi hao wamepuuza ushauri huo na kupeleka timu na matokeo yake yameanza kuonekana kwa Mchezaji Erasto Nyoni kuumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nikajua amededi kumbe kaumia tu? Kuumia ni sehemu ya mchezo wa soka. Punguza jazba kijana
 
Hata mazoezini watu wanaumia, wacha uoga wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
poor strategies simba, wakiongozwa na manara!
Manara sio benchi la ufundi yule ni msemaji wa simba...yeye anasema ambacho benchi la ufundi limemwagiza kusema
 
Kibongo bongo Nyoni Jumamosi atalazimishwa kucheza hata kama hajapona! Mikia wanajigamba kuwa na kikosi kipana ila woga umewajaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka Manara mshauri mzungu wenu. Ukishinda kombe la Muungano utatambulika mwisho Kariakoo lakini ushindi na Waarabu dunia nzima utajulikana. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
 
Mazoezini,hata nyumbani mtu anaumia tu.Hata wasingecheza mapinduzi bado angeweza kuugua hata malaria,au siku ya mechi akaugua tumbo la kuhara.Waamini waliopo.
 
Hakuna viongozi, na kocha wabovu duniani kama wa Simba. Huu ulikuwa muda wa kuandaa timu kisaklojia na mazoezi na mifumo mbalimbali baada ya kuangalia kwa umakini video za maadui zao, wachezavyo, ni mchezaji gani hatari na watawadhibiti vipi sasa wanawepeleka kuwaumiza kwenye ligi ya mchangani??? ona sasa mchezaji muhimu hana goti hawa wataiaibisha nchi hawa, watafute pa kwenda mtawapa waaarabu vya kusemea helua...helua wanapowashishia mvua ya magoli. Oneni wenzenu wapo full mzuka
https://www.facebook.com/
 
Kuumia kwenye mpira no kawaida chief. Kama hamtaki kuguswa mkacheze draft. Huko hamna kugusana ni maneno mengi tu kama ya msema ovyo wenu. PUMBAVU SANA
 
Na we Nyoni kiwa mchezaji.
!!!!
Nyoni si ndo yule mchezaji mwenye thamani ndogo kuliko wore pale Mikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…