Kuumia kwa Mohammed Salah kuna la kujifunza!

Najaf

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2015
Posts
1,505
Reaction score
2,393
Mohammed Salah ni muumini mzuri wa dini ya kiislamu. Tumemuona mara nyingi akimuomba na kumlilia Mungu katika kila mechi aingiayo uwanjani. Tena muda mwingine husujudu kama ishara ya kumshukuru Muumba wake kwa kutimiza shida zake. Na kweli Mo Salah amekuwa mfungaji bora na mshindi mzuri katika premier league.

Mistake aliyofanya Mo Salah ni hii:
Tunafahamu kwamba kipindi hiki Waislamu tupo kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mwezi ambao Mwenyezi Mungu ameamuru waumini wa dini yetu kufunga ndani ya mwezi huu mtukufu.

Ndani ya mwezi huu kuna rehma na barak nyingi kwa afanyae ibada ya kufunga. Mo Salah ndani ya siku mbili hizi, namanisha siku ya fainali ya UEFA na siku moja kabla ya UEFA hakufunga. Ni jambo linalosikitisha. Mo Salah alihitaji kuvunja rekodi ya kuchukua Kombe la Mabingwa pia kumuweka katika nafasi nzuri ya kuwania Tuzo ya mchezaji Bora wa Dunia.

Mo Salah alimuhitaji zaidi Mungu katika kipindi hiki zaidi. Maana walishamuomba kuwa mfungaji bora akamfanikishia.

Kuacha kufunga Salah kuna maanisha alihofia kudhoofika kiafya katika mashindano haya makubwa. Lakini alisahau kwamba Mungu yule yule aliyemuomba kipindi cha mechi za premier league ndiye Mungu aliyemfikisha fainali ya UEFA ndani ya Ramadhani

Lakini hakufunga ndani ya siku hizi wakati hili jambo lilikuwa la umuhimu pia kwake kwa mujibu wa dini yake.

Matokeo yake amekosa Kombe la Mabingwa na Tumuombee Kwa Muumba walau ashiriki hata kombe la Dunia. Maana Bendera ya Wa afrika inwmuhusu pia.

Binadamu hukosea,,Na Mungu Husamehee.

Ni maoni yangu tu,,,

Ahsanteni
 
Kwani Benzima na zidane wa madrid wenyewe walifunga......au allah kamuona Mo sala peke yake, anyway kuna la kujifunza katika hilo unavo panga na allah anapanga.....ndomaana kila jambo tunatanguliza inishaallah.......
 
Kwani Benzima na zidane wa madrid wenyewe walifunga......au allah kamuona Mo sala peke yake, anyway kuna la kujifunza katika hilo unavo panga na allah anapanga.....ndomaana kila jambo tunatanguliza inishaallah.......
Benzema ni malaya malaya tu,zidane hajali dini..salah ni mshiruka wa karibu wa allah..kama hakufunga kisa fainali atakua kapata somo
 
We mleta Uzi mnafiki sana

Mungu amekuambia hayo uloaandika?

jinga sana wewe

Chambalani naye alimkosea nini Mungu?
 
Wewe mleta Mada hujui ata soccer n nini hili si jukwaa la dini Liverpool wameshndwa kwa sabubu walifanya makosa yao ya kijinga
 
Wabongo bana. Sijui kajuaje kama Salah hakufunga? Sijui kajuaje ile event ni adhabu kutoka kwa Allah? Sijui ile zawadi ya goal la Benzema ni kwa kuwa yeye alifunga? Tunaongea sana. Wajuaji at best.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…