Kuumia kwa Mohammed Salah kuna la kujifunza!

Kuumia kwa Mohammed Salah kuna la kujifunza!

Mohammed Salah ni muumini mzuri wa dini ya kiislamu. Tumemuona mara nyingi akimuomba na kumlilia Mungu katika kila mechi aingiayo uwanjani. Tena muda mwingine husujudu kama ishara ya kumshukuru Muumba wake kwa kutimiza shida zake. Na kweli Mo Salah amekuwa mfungaji bora na mshindi mzuri katika premier league.

Mistake aliyofanya Mo Salah ni hii:
Tunafahamu kwamba kipindi hiki Waislamu tupo kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mwezi ambao Mwenyezi Mungu ameamuru waumini wa dini yetu kufunga ndani ya mwezi huu mtukufu.

Ndani ya mwezi huu kuna rehma na barak nyingi kwa afanyae ibada ya kufunga. Mo Salah ndani ya siku mbili hizi, namanisha siku ya fainali ya UEFA na siku moja kabla ya UEFA hakufunga. Ni jambo linalosikitisha. Mo Salah alihitaji kuvunja rekodi ya kuchukua Kombe la Mabingwa pia kumuweka katika nafasi nzuri ya kuwania Tuzo ya mchezaji Bora wa Dunia.

Mo Salah alimuhitaji zaidi Mungu katika kipindi hiki zaidi. Maana walishamuomba kuwa mfungaji bora akamfanikishia.

Kuacha kufunga Salah kuna maanisha alihofia kudhoofika kiafya katika mashindano haya makubwa. Lakini alisahau kwamba Mungu yule yule aliyemuomba kipindi cha mechi za premier league ndiye Mungu aliyemfikisha fainali ya UEFA ndani ya Ramadhani

Lakini hakufunga ndani ya siku hizi wakati hili jambo lilikuwa la umuhimu pia kwake kwa mujibu wa dini yake.

Matokeo yake amekosa Kombe la Mabingwa na Tumuombee Kwa Muumba walau ashiriki hata kombe la Dunia. Maana Bendera ya Wa afrika inwmuhusu pia.

Binadamu hukosea,,Na Mungu Husamehee.

Ni maoni yangu tu,,,

Ahsanteni
Acha story zako, yule Mo Salah anafanya mambo mema kwa watu maskini kuliko unavyodhani wewe. mtu ukiwa safarini unaruhusiwa kufungua na kulipa baadae. Mo Salah alikuwa safari nchi ya kigeni.
 
Kwani Benzima na zidane wa madrid wenyewe walifunga......au allah kamuona Mo sala peke yake, anyway kuna la kujifunza katika hilo unavo panga na allah anapanga.....ndomaana kila jambo tunatanguliza inishaallah.......
Ahsante kwa neno zuri.
 
Si kila unapofanya ibada ya funga bac Mwenyez Mungu hujibu dua zako muda huo huo..Hapana,na ndio maana tunatakiwa kila siku tufanye ibada na huku tukisema Mwenyez Mungu akijaalia(InshaAllah) atakalo ndo litakuwa japo pia dua na ibada ni dawa zaidi katika maisha yetu ya siku zote co Ramadhan tu
Mo Salah alikuwa Ukraine Siku Tatu kabla,,, by the way ,,
Sema INSHAALLAH TUMUONE KOMBE LA DUNIA
 
Kwani Benzima na zidane wa madrid wenyewe walifunga......au allah kamuona Mo sala peke yake, anyway kuna la kujifunza katika hilo unavo panga na allah anapanga.....ndomaana kila jambo tunatanguliza inishaallah.......
Zidane alishang'atuka
 
Hukumu za kibinadamu zinatisha kuliko za aliyeziweka.

Nguzo za uislam ziko 5 je ? Zinazidiana kwa ubora au zote ni muhimu na zizingatiwe.

Mtoa mada unamaanisha Jana ,mbali ya mpira DINI pia zilishindana, kimtizamo wako BALE Ibada yake ilipokelewa, SADIO alikadhalika bila kumsahau BENZEMA.

MO na KIPA Wa LIVERPOOL walimkosea Mola wao.

Kwangu mmmmh sio sawa.
 
Nakuunga mkono moja kwa moja mtoa mada.

walimpressure sana asifunge nayeye akalegeza msimamo.

Alichokionesha ni udhaifu wa imani.
 
Wabongo bana. Sijui kajuaje kama Salah hakufunga? Sijui kajuaje ile event ni adhabu kutoka kwa Allah? Sijui ile zawadi ya goal la Benzema ni kwa kuwa yeye alifunga? Tunaongea sana. Wajuaji at best.

- watu wa masuala ya afya wa liverpool walithibitisha kama Salah na Mane hawatofunga kuanzia Alhamis. wakati mane hakukua nashaka kame asingelifunga siku ya mechi, kesi ilikua kwa salah amabae alionekanwa asingeliacha kirahisi kufunga, hajapatapo kuacha kufunga kwa mpira.
- Kila anaekua karibu zaidi na Mungu kiimani ndie anaepata majaribio au mitihani zaidi ili kupimwa uzito wa imani yake. Kama ni muislamu basi utafaham hilo, kama sie nakubali itakua ngumu kulielewa. kwaiyo kuhusu kesi ya Benzema huwezi fanananisha na salah hata kama wote ni waislamu.
 
Back
Top Bottom