mwehu ndama
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 2,472
- 9,542
Mwaka 2012 nikiwa kidato cha nne nilitumia likizo yangu mkoano mwanza ..Uko nilipata fursa ya kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Jimbo cup yaliokua yakiandaliwa na mbunge wa ilemela kwa wakati ule ndugu Anthony dialo.
Tukiwa hatua ya nusu fainali wakati huo Mimi nikichezea timu inaitwa Fc Jonas ya kirumba , Ghana ,Mwanza..Tulipambana na timu ya shule ya secondary taqwa kutoka Ghana ,Mwanza pia. iliokua imesheheni nyota kibao ambao baadae walicheza ligi kuu ya Tanzania.
Wakati mchezo ukiwa unaendelea nakumbuka aliekua nahodha wa timu ya Taqwa sec ndugu John matei ambaye kwa wakati huo alikua kidato cha sita pale taqwa sec ila kwa sasa ni afisa wa askari magereza baada ya kuitumika Tanzania prison kwa misimu minne, aligongana na mmoja wa wachezaji wa timu yangu . Hali iliyopelekea ndugu John matei kuteguka mguu katika mazingira sawa na pacome , lakini kwa John matei ilikua mbayaa zaidi sababu eneo la mbele la vikanyagio lilirudi nyuma lakini alivunjika eneo la ugoko mara mbili ..!
Lakini kwa mshangao wa wengi alipelekwa kisiwami ukerewe kwa matibabu zaidi na baada ya miezi miwili jamaa alikiwasha Tena mpaka ligi kuu na alifanikiwa kuwafunga Yanga sc katika moja ya mechi dhidi Yao.
Hivyo ninaimani hata pacome nae atarejea uwanjani na kuendelea na majukumu yake ya Kila siku kwa ajili yake na familia yake.
Mpira sio vita!!!!1
Nb : nimelewa