OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Mafanikio ni nini?
Mafanikio ni hatua ya kufikia au kuzidi malengo uliyojiwekea. Kwa lugha ya kigeni tunaita Goal Achievement.
Simba tumekuwa na malengo kadhaa kila mwaka. Moja ya malengo yamekuwa ni kufanya vizuri kimataifa na kwa kiwango kikubwa tumekuwa tukifanikiwa kifikia malengo yetu. Huu ni mwaka mwingine tena wa kuthibitisha umwamba wetu kama Tanzanian Giants.
Kama ilivyo ada ukifanikiwa unavuta maadui wengi. Wengi wao wanakuwa hawana sababu za msingi za kuchukizwa na mafanikio yako.
Sisi hatuna habari tunafikiria jinsi ya kujikita juu. Tunaumizwa vichwa na robo fainali za Ligi ya Mabingwa.
Kwenye hatua hii hakuna mnyonge.
CR Belouzdad amecheza robo fainali mbili ya ligi ya mabingwa hii ni robo fainali yake ya tatu (3).
Esparance ametwa Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mara nne (4).
Js Kabylie ametwaa ubingwa wa Afrika mara mbili (2).
Raja Casablanca amechukua Ubingwa wa ligi ya mabingwa Afrika mara tatu (3).
Wydad Athletics Ndo bingwa Mtetezi wa kombe hili na ametwaa Ubingwa mara tatu.
Mamelod ametwaa ubingwa mara moja na amecheza fainali mara moja.
Al Ahly hili ndo balaa kuu la Afrika kachukua Ubingwa huu mara mara 10.
Al Hilal ya amecheza fainali mara mbili (2).
Halafu kuna sisi hapa Simba Sports tumecheza nusu Fainali moja na tuna robo Fainali 3 za Ligi ya Mabingwa Afrika.