SoC04 Kuundwa kwa kanzidata ya vyeti vya elimu vya kidijitali; Maboresho ya utunzaji wa taarifa za kitaaluma

Tanzania Tuitakayo competition threads

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2014
Posts
5,909
Reaction score
10,542
Kutokana na uhitaji wa lazima wa mifumo ya kisasa ya taaluma na utoaji wa ajira, ninashauri pawepo na mfumo wa kidijitali wa uhifadhi na upatikanaji wa vyeti vya elimu (accessibility and retrieval) ambao utaunganishwa na taasisi zote za serikali, za binafsi, mashirika binafsi na taasisi zote za ajira.

1. KWAMBA, ili kudhibiti ithibati na uhalali wa taaluma na elimu; Nyaraka, vyeti na taarifa zote za kielimu za muhusika ziunganishwe kwenye mfumo mmoja wa kanzidata ambapo taasisi zote za serikali, taasisi binafsi, waajiri pamoja na muhusika mwenyewe wataweza kutizama taarifa za mtu huyo moja kwa moja kupitia mfumu huo kwa madhumuni ya kuajiri, kutunza kumbukumbu na kulinda ithibati ya vyeti.

2. KWAMBA, ili kudhibiti wizi wa vyeti, ughushaji wa taarifa za elimu na uhalali wa taaluma; Nyaraka, vyeti na taarifa zote za muhusika zitakapowekwa kwenye mfumo mmoja wa kompyuta yaani kanzidata, zitaweza kuunganishwa na taarifa za NIDA na alama za vidole za muhusika wa taarifa hizo, NECTA, vyuo vikuu na taasisi mbalimbali.

3. KWAMBA, ili kuondokana na uharibikaji au upotevu wa nakala ngumu za vyeti, muhusika na taasisi zote mahususi, zitaweza kutizama nyaraka na taarifa za kielimu za muhusika kupitia mfumo wa kati wa kanzidata moja kwa moja bila uhitaji wa nakala ngumu.

4. KWAMBA, taasisi zote za elimu, taasisi za serikali, taasisi za ajira, mashule, vyuo vikuu, vyuo vya kati, NIDA, NECTA, NACTE na TCU zitaunganishwa katika mfumo wa kati wa kanzidata ili kuchangia taarifa hizo kwa pamoja.

5. KWAMBA, muhusika wa taarifa hizo ataruhusiwa kupata, kutizama, kutuma na kutumia nyaraka na taarifa zake za kielimu zilizo katika mfumo wa kati wa kanzidata kwa masharti na vigezo ambavyo vitazingatia usiri na faragha kwa mujibu wa sheria ya Ulinzi wa Taarifa binafsi.

HIVYO BASI:
1. Uundwaji wa kanzidata ya kati (central database), yaani:-

a) Kanzidata ya kati itakayofanya kazi ya kuhifadhi vyeti na taarifa zote za kielimu za wahusika ambazo zitakusanywa kutoka shule za msingi, shule za sekondari, vyuo vikuu, vyuo vya kati na vyuo vya ufundi pamoja na taasisi zingine za kielimu.

b) Matokeo yote ya pamoja ya wahitimu wa ngazi za shule za msingi na za sekondari pamoja na nakala vivuli vya matokeo hayo kuingizwa katika kanzi data ya kati ya wajibu wa BARAZA LA MITIHANI (NECTA) iliyounganishwa na taasisi zingine zote muhumu zitakazokuwa na uwezo wa kutizama taarifa hizo.

c) Vyuo vikuu vyote vya serikali pamoja na vya binafsi VILAZIMIKE kutuma taarifa zote za kielimu za wahitimu pamoja na nakala vivuli vya matokeo yao kwenye kanzidata ya TUME YA VYUO VIKUU (TCU) ili iweze kuhifadhi taarifa hizo kwenye mfumo utakaounganishwa na NECTA pamoja na taasisi zingine zote muhimu.

d) Vyuo vyote vya ufundi, vya kati na taasisi zingine za kielimu ZILAZIMIKE kutuma na kuhifadhi taarifa za kielimu za wahitimu wake pamoja na nakala vivuli vya matokeo yao na kuviwasilisha katika mfumo wa NACTE ambao utaunganishwa na TCU katika mfumo wa pamoja wa kati.

e) Mfumo wa kati wa kanzidata uliounganisha taarifa zote kutoka NECTA, TCU na NACTE uunganishwe na mfumo wa NIDA na RITA ili kuhakiki taarifa zao za uraia na kuzaliwa.

MFUMO WA KANZI DATA WA KATI NA TAASISI ZOTE ZA AJIRA
Taarifa zote zilizohifadhiwa kweye kanzidata ya kati ziingizwe kwenye mfumo wa SEKRETARIETI YA AJIRA (ajira portal) ili kwamba, kila muajiri kutoka taasisi za serikali au binafsi alazimike kuajiri kupitia SEKRETARIETI YA AJIRA ambayo imeshahifadhi taarifa zote za kielimu za wahusika.

Taarifa hizi ziwe ni taarifa za matokeo pamoja na nakala za vyeti vyake (scanned copies) zitakazokuwa kwenye mfumo maalumu.

MALENGO NA MADHUMUNI
1. Taasisi zinazoajiri hazitalazimika kuomba nakala za vyeti. Zitaingia katika mfumo wa ajira na kuona sifa za muhusika.

2. Wahusika hawatakuwa na haja ya kubeba vyeti kwenda navyo kwenye usaili kwa sababu vyeti vyote viko kwenye mfumo.

3. Wahusika wakipoteza nakala halisi za vyeti hawatakuwa na ulazima wa kutafuta vyeti vipya. Watapewa namba maalumu ya kuingia katika mfumo na kutazama vyeti vyao au kupakua nakala zake.

SULUHU YA TATIZO LA KUPOTEA NA KUCHAKAA KWA VYETI
KWA KUWA taarifa zote za kielimu zenye ithibati zimekwisha kuhifadhiwa katika mfumo maalumu wa kanzidata, hapatakuwa na haja ya kuhofu pale ambapo vyeti halisi vimepotea au kuharibika. Waajiri watatizama taarifa zake za kielimu katika mfumo wa kidijidali pasipo ulazima wa kuangalia nakala halisi.

Nakala halisi zinaweza kutumika kama chaguo la pili tu au pale ambapo mfumo una matatizo au changamoto zingine.

Changamoto ya vyeti kuharibika au kupotea au kuliwa na panya nu changamoto inayowakumba wengi. Kupata cheti kipya ni mchakato mrefu unaogharimu pesa na wakati na hata mara nyingine kushindwa kabisa kupata nakala mbadala wa kwa sababu kadha wa kadha. Hivyo, vyeti vya kidigitali vitakuwa ni suluhu ya kudumu.

CHANGAMOTO YA VYUO KUFUNGWA, KUFUTWA AU KUFUTIWA USAJILI
Kupata cheti kipya si jambo rahisi, na hasa pale ambapo unakutana na vikwazo visivyotatulika. Mara kwa mara tumesikia vyuo kufungwa au kufutiwa usajili kwa sababu mbalimbali, jambo ambalo linaweza kuwaathiri wahitimu wake na haswa katika jitihada za kupata vyeti vipya baada ya kupoteza vyeti vya awali.

Haiwezekani kurudi katika chuo kilichofutwa ili kupata cheti kipya. Hivyo, vyeti vya kidigitali vitakuwa suluhu ya kudumu na vitasimama hata kama chuo hakipo au kimefutwa.

TATIZO LA KUGHUSHI VYETI
Kuna makanjanja wengi wasio na vigezo vya kitaaluma walioghushi vyeti na kufanya udanganyifu au hata kuajiriwa katika nafasi ambazo hawastahili. Jambo hili linawanyima fursa wale wenye uhalali wa kuajiriwa. Vilevile serikali hupoteza mapato kwa kuwalipa mishahara VISHOKA.

Kwa madhumuni ya kulinda ithibati ya vyeti, waajiri wote watalazimika kutizama taarifa za kielimu kupitia kanzidata maalumu ambayo ina picha za wahusika, serial numbers na taarifa za NIDA.

WAHUSIKA KUPATA TAARIFA ZAO PALE WANAPOZITAKA
Mfumo huu wa kanzidata utawaruhusu wahusika kuweza kutizama taarifa zao au nakala vivuli za matokeo kwa kutumia msimbo maalumu au nywila ya kidijitali.

Pia, muhusika atapewa fursa ya kuzipakua taarifa hizo pamoja na nakala zake kwa madhumuni ya kuzitumia kwa jinsi anayoona inafaa. Au, aweze kuzifungua, kuzipakua na kuzituma kwenye mtandao kwenda mahali pengine.

MWISHO.

Naomba kuwasilisha. Ahsante.
 
Upvote 5
Kutokana na uhitaji wa lazima wa mifumo ya kisasa ya taaluma na utoaji wa ajira, ninashauri pawepo na mfumo wa kidijitali wa uhifadhi na upatikanaji wa vyeti vya elimu (accessibility and retrieval) ambao utaunganishwa na taasisi zote za serikali, za binafsi, mashirika binafsi na taasisi zote za ajira.

1. KWAMBA, ili kudhibiti ithibati na uhalali wa taaluma na elimu; Nyaraka, vyeti na taarifa zote za kielimu za muhusika ziunganishwe kwenye mfumo mmoja wa kanzidata ambapo taasisi zote za serikali, taasisi binafsi, waajiri pamoja na muhusika mwenyewe wataweza kutizama taarifa za mtu huyo moja kwa moja kupitia mfumu huo kwa madhumuni ya kuajiri, kutunza kumbukumbu na kulinda ithibati ya vyeti.

2. KWAMBA, ili kudhibiti wizi wa vyeti, ughushaji wa taarifa za elimu na uhalali wa taaluma; Nyaraka, vyeti na taarifa zote za muhusika zitakapowekwa kwenye mfumo mmoja wa kompyuta yaani kanzidata, zitaweza kuunganishwa na taarifa za NIDA na alama za vidole za muhusika wa taarifa hizo, NECTA, vyuo vikuu na taasisi mbalimbali.

3. KWAMBA, ili kuondokana na uharibikaji au upotevu wa nakala ngumu za vyeti, muhusika na taasisi zote mahususi, zitaweza kutizama nyaraka na taarifa za kielimu za muhusika kupitia mfumo wa kati wa kanzidata moja kwa moja bila uhitaji wa nakala ngumu.

4. KWAMBA, taasisi zote za elimu, taasisi za serikali, taasisi za ajira, mashule, vyuo vikuu, vyuo vya kati, NIDA, NECTA, NACTE na TCU zitaunganishwa katika mfumo wa kati wa kanzidata ili kuchangia taarifa hizo kwa pamoja.

5. KWAMBA, muhusika wa taarifa hizo ataruhusiwa kupata, kutizama, kutuma na kutumia nyaraka na taarifa zake za kielimu zilizo katika mfumo wa kati wa kanzidata kwa masharti na vigezo ambavyo vitazingatia usiri na faragha kwa mujibu wa sheria ya Ulinzi wa Taarifa binafsi.

HIVYO BASI:-

1. Uundwaji wa kanzidata ya kati (central database), yaani:-

a) Kanzidata ya kati itakayofanya kazi ya kuhifadhi vyeti na taarifa zote za kielimu za wahusika ambazo zitakusanywa kutoka shule za msingi, shule za sekondari, vyuo vikuu, vyuo vya kati na vyuo vya ufundi pamoja na taasisi zingine za kielimu.

b) Matokeo yote ya pamoja ya wahitimu wa ngazi za shule za msingi na za sekondari pamoja na nakala vivuli vya matokeo hayo kuingizwa katika kanzi data ya kati ya wajibu wa BARAZA LA MITIHANI (NECTA) iliyounganishwa na taasisi zingine zote muhumu zitakazokuwa na uwezo wa kutizama taarifa hizo.

c) Vyuo vikuu vyote vya serikali pamoja na vya binafsi VILAZIMIKE kutuma taarifa zote za kielimu za wahitimu pamoja na nakala vivuli vya matokeo yao kwenye kanzidata ya TUME YA VYUO VIKUU (TCU) ili iweze kuhifadhi taarifa hizo kwenye mfumo utakaounganishwa na NECTA pamoja na taasisi zingine zote muhimu.

d) Vyuo vyote vya ufundi, vya kati na taasisi zingine za kielimu ZILAZIMIKE kutuma na kuhifadhi taarifa za kielimu za wahitimu wake pamoja na nakala vivuli vya matokeo yao na kuviwasilisha katika mfumo wa NACTE ambao utaunganishwa na TCU katika mfumo wa pamoja wa kati.

e) Mfumo wa kati wa kanzidata uliounganisha taarifa zote kutoka NECTA, TCU na NACTE uunganishwe na mfumo wa NIDA na RITA ili kuhakiki taarifa zao za uraia na kuzaliwa.

MFUMO WA KANZI DATA WA KATI NA TAASISI ZOTE ZA AJIRA:-

Taarifa zote zilizohifadhiwa kweye kanzidata ya kati ziingizwe kwenye mfumo wa SEKRETARIETI YA AJIRA (ajira portal) ili kwamba, kila muajiri kutoka taasisi za serikali au binafsi alazimike kuajiri kupitia SEKRETARIETI YA AJIRA ambayo imeshahifadhi taarifa zote za kielimu za wahusika.

Taarifa hizi ziwe ni taarifa za matokeo pamoja na nakala za vyeti vyake (scanned copies) zitakazokuwa kwenye mfumo maalumu.

MALENGO NA MADHUMUNI:-

1. Taasisi zinazoajiri hazitalazimika kuomba nakala za vyeti. Zitaingia katika mfumo wa ajira na kuona sifa za muhusika.

2. Wahusika hawatakuwa na haja ya kubeba vyeti kwenda navyo kwenye usaili kwa sababu vyeti vyote viko kwenye mfumo.

3. Wahusika wakipoteza nakala halisi za vyeti hawatakuwa na ulazima wa kutafuta vyeti vipya. Watapewa namba maalumu ya kuingia katika mfumo na kutazama vyeti vyao au kupakua nakala zake.

SULUHU YA TATIZO LA KUPOTEA NA KUCHAKAA KWA VYETI:-

KWA KUWA taarifa zote za kielimu zenye ithibati zimekwisha kuhifadhiwa katika mfumo maalumu wa kanzidata, hapatakuwa na haja ya kuhofu pale ambapo vyeti halisi vimepotea au kuharibika. Waajiri watatizama taarifa zake za kielimu katika mfumo wa kidijidali pasipo ulazima wa kuangalia nakala halisi.

Nakala halisi zinaweza kutumika kama chaguo la pili tu au pale ambapo mfumo una matatizo au changamoto zingine.

Changamoto ya vyeti kuharibika au kupotea au kuliwa na panya nu changamoto inayowakumba wengi. Kupata cheti kipya ni mchakato mrefu unaogharimu pesa na wakati na hata mara nyingine kushindwa kabisa kupata nakala mbadala wa kwa sababu kadha wa kadha. Hivyo, vyeti vya kidigitali vitakuwa ni suluhu ya kudumu.

CHANGAMOTO YA VYUO KUFUNGWA, KUFUTWA AU KUFUTIWA USAJILI:-

Kupata cheti kipya si jambo rahisi, na hasa pale ambapo unakutana na vikwazo visivyotatulika. Mara kwa mara tumesikia vyuo kufungwa au kufutiwa usajili kwa sababu mbalimbali, jambo ambalo linaweza kuwaathiri wahitimu wake na haswa katika jitihada za kupata vyeti vipya baada ya kupoteza vyeti vya awali.

Haiwezekani kurudi katika chuo kilichofutwa ili kupata cheti kipya. Hivyo, vyeti vya kidigitali vitakuwa suluhu ya kudumu na vitasimama hata kama chuo hakipo au kimefutwa.

TATIZO LA KUGHUSHI VYETI:-

Kuna makanjanja wengi wasio na vigezo vya kitaaluma walioghushi vyeti na kufanya udanganyifu au hata kuajiriwa katika nafasi ambazo hawastahili. Jambo hili linawanyima fursa wale wenye uhalali wa kuajiriwa. Vilevile serikali hupoteza mapato kwa kuwalipa mishahara VISHOKA.

Kwa madhumuni ya kulinda ithibati ya vyeti, waajiri wote watalazimika kutizama taarifa za kielimu kupitia kanzidata maalumu ambayo ina picha za wahusika, serial numbers na taarifa za NIDA.

WAHUSIKA KUPATA TAARIFA ZAO PALE WANAPOZITAKA:-

Mfumo huu wa kanzidata utawaruhusu wahusika kuweza kutizama taarifa zao au nakala vivuli za matokeo kwa kutumia msimbo maalumu au nywila ya kidijitali.

Pia, muhusika atapewa fursa ya kuzipakua taarifa hizo pamoja na nakala zake kwa madhumuni ya kuzitumia kwa jinsi anayoona inafaa. Au, aweze kuzifungua, kuzipakua na kuzituma kwenye mtandao kwenda mahali pengine.

MWISHO.

Naomba kuwasilisha. Ahsante.
poa sana
 
Wazo zuri ila haiwezekani kufanya hivyo kwa kanzidata moja ilobeba kila entity.

Tatizo ni rushwa na ifisadi lakini kila taasisi ni lazima iwe na mfumo wake wa kanzidata ambayo ndo waangalia mambo kama vyeti.

Endapo kila chuo chaweza kutoa cheti na ikashindikana ni bora kutoa zabuni kwa kampuni zenye uzoefu na masuala ya kuchapisha vyeti.

Juzi kulikuwa na taarifa ya chuo kimoja kuchelewesha vyeti kwasababu mbalimbali jambo ambalo kimaendeleo laonyesha bado tupo nyuma.
 
Back
Top Bottom