Kashishi yetu
JF-Expert Member
- Mar 22, 2014
- 3,509
- 3,741
Majanga mengi yamekuwa yakijitokeza ya moto.Sasa hivi kuna janga la moto Soko la KARIAKOO, Shule moja huko Morogoro.
Je kutokana na majanga haya na mengine ambayo yalishawahi kutokea huko nyuma na chanzo chake kusemekana ni hitilafu ya umeme, JE KUNA CHA KUJIFUNZA KUHUSU MAJANGA HAYA YA MOTO?NINI KIFANYIKE KUZUIA AU KUPUNGUZA MAJANGA HAYA YA MOTO?
Binafsi nimejifunza yafuatayo:-
Mosi,Kuwepo na ulazima wa majengo kukaguliwa mifumo mizima ya wayaringi kila baada ya kipindi fulani jengo lote kukaguliwa na wataalamu kutoka TANESCO.Hili nliilipata siku TANESCO walipokuja mtaani kwetu baada ya shoti ya umeme kuunguza vifaa na watu kutaka kulipwa fidia.Hivyo TANESCO walihoji lini jengo lako limewahi kukaguliwa na TANESCO kuona ubora wa nyaya?
Pili,Kuzingatia maelekezo ya TANESCO.Siku walipokuja kwetu. TANESCO waliuliza maswali mengi sana,Je Wakati unafanyiwa wayaringi nyumba yako, Je vifaa ulivyoandika utakavyokuwa unavitumia ndivyo hivyo hivyo au uliongeza vingine tofauti na mwanzo? Kama uliongeza vingine je ulienda TANESCO kuomba kibali ili waje wakurekebishie mfumo wako wa wayaring?
Tatu,Kuwasha pale tu unapohitaji kutumia kifaa cha umeme na kuzima mara tu baada ya kumaliza matumizi ya kifaa hicho.Wengi hapa hujisahau.Huacha feni ikiwaka na matokeo yake umeme ukikatika na ukirudi unarudi kwa kasi ya ajabu.
Nne,Kwa upande pia wa mashuleni huko.Umakini unahitajika kwani baadhi ya wanafunzi huenda mashuleni wakiwa na simu.Sehemu ya kuchajia hupanda juu ya Dali na kuchubua nyaya za umeme, wanajua jinsi ya kuunganisha hadi kufanikisha kuchaji simu zao.
Tano, Usalama wa vyombo tunavyovitumia.Visiwe vifaa chakavu sana.Vifaa chakavu husababisha shoti ya umeme.
Sita, Kwenye biashara yako hakikisha kila unapouza pesa peleka benki.Usilaze dukani pesa zako hata siku moja.
Saba, Nimejifunza kuwa na rekodi za biashara yangu sehemu mbili.Yaani uhifadhi wa kumbukumbu za biashara yangu ufanyike sehemu mbili.Dukani niache nakala na nyumbani kwangu ziwepo nakala ili ikitokea janga la moto kama hili wadeni wangu wote au taarifa muhimu au nyaraka muhimu za biashara yangu zisipotee.
Nane,Nimejifunza kuwa nijenge mahusiano mazuri na wenzangu ili ikitokea janga la moto nipate misaada lukuki kutoka kwao.
Tisa,Nimejifunza kuepukana kabisa na mafundi vishoka wa umeme.Niache ubahiri wa kukataa kuwaita Mafundi wa TANESCO kukwepa gharama na kuwatumia vishoka ambao hawana utaalamu wowote zaidi ya kutafuta pesa ya kula na familia zao huku mimi wakiniachia msalaba mzito wa kuunguliwa vitu vyangu vya thamani kubwa kabisa.
Hayo ndiyo niliyojifunza kwa upande wangu.
.Mengi nilijifunza siku TANESCO walipokuja mtaani kwetu walitupatia Elimu.
Je wewe mwenzangu umejifunza nini cha kuongezea au kupunguza katika hayo niliyojifunza?
UPDATE
SOKO LA KARUME LIMEUNGUA TENA MOTO WALOZINGATIA USHAURI WANGU HUU UTAKUWA UMEWASAIDIA WALOUPUUZA IMEKULA KWAO.
SERIKALI IFANYE UCHUNGUZI KWANINI MAJANGA YA MOTO YATOKEE USIKU TU? AU KUNA WAFANYABIASHARA WANAACHA VITU ON KWENYE VIZIMBA VYAO?