Kama wewe ni mwanaume basi ni mbeya sana. Unataka kila kitu kiwe kimeandikwa kwenye biblia. Una soma biblia kwa alkili yako au kwa masaburi yako. Kuna kosa gani kama naungama kwa mjumbe wa Mungu ili anipe ushauri kwa dhambi zangu kadiri imani yangu inavyoniruhusu. Kama imani yako inataka umfiche mtumishi wake na kuungama moja kwa moja kwake basi na iwe hivyo.
Huwezi kunifanya niabudu kama unavyotaka wewe. Uheshimu imani ya wenzako. Usiwe kama wazungu waliodharau imani zetu nakuziita za kijinga na sisi tukaziona za kijinga tukafuata imani za kiarabu na kizungu. Kila mwenye imani ya asili leo anaonekana kama mshamba na wewe ukiwaona kama washamba. Mungu hayupo kwa Wakristo tu au kama unavyodhani wewe Mungu yupo kwa walokole kwa sababu hawaungami kwa padri bali Mungu ni wa wote wawe wenye dhambi na wasiona dhambi au wenye imani za kiarabu au imani za kizungu au imani asili; Mungu niwa wote.
Kwa hiyo uwe mstaarabu kwa imani za watu. Kakuambia nani kuwa wewe kujiungamia ndiyo sahihi. Kujikweza ni tabia mbaya sana ambayo mwanadamu anayo na hii usipojichunguza itakutafuna.
Kuna ile ahadi ya mwanaTANU ambayo mi nimeipenda: Binadamu wote ni ndugu zangu. Kwa hiyo kama anaabudu miti au mito mikubwa hawezi kuwa ndugu yako? Au kama ni Mwislamu au Mkatoliki anayeabudu kwa padri si ndugu yako kwa sababu ana imani ya kishenzi.
Ungekuwa umeshika mafundisho ya kiimani vizuri usingemdharau binadamu mwenzako kwa imani yake. Mungu si Mkatoliki, Mlokole, Mwislamu wala imani asili wala Budha wala Saibaba, Mungu ni Mwenyezi. Hajibagui kwa imani zetu kama wanadamu kama wewe unavyofanya.
KUMBUKA: Tutahukumiwa kwa matendo yetu tu wala si kwa imani zetu.